Israel haina hamu na mateka mpya waliyesema wamemuokoa

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Mateka wa Israel aliyetajwa kwa mbwembwe nyingi kwamba aliokolewa hapo juzi amekuwa kama yule bibi wa kifaransa aliyeachiliwa huru na wanamgambo wa Mali miaka miwili iliyopita.Bibi huyo alimfanya Macron afupishe muda wa kumpokea uwanjani pale alipowasifia wanamgambo wa Mali na kuahidi kurudi tena Mali kuendelea na kazi zake za huduma kwa jamii.

Kwa upande wa ndugu Kaid Farhan Elkadi mwenye umri wa miaka 52 ilitangazwa na jeshi la Israel kwamba aliokolewa katika jaribio lililokuwa la kiufundi sana.Baada ya hapo jeshi likasema halitaendelea kutoa taarifa zaidi juu ya uokoaji wake kutokana na kulinda usalama wa mateka waliobaki mikononi mwa Hamas.

Kwa kadri taarifa zinavyoendelea kuvuja inaonesha mateka hiyo aliachiliwa kwa makusudi ili awe kama mjumbe kwa Israel.Kaid ni muislamu na muarabu wa kabila la Bedui kutoka jangwa la Negev maeneo ya kusini ya Israel.

Mateka mwenyewe huyo tangu alipofika kwa watu wake amekuwa akitoa sizi hizo za uokolewaji wake.Anasema muda mwingi alikuwa yuko huru huko chini ya ardhi na siku hiyo alikuwa amewachwa peke yake kabla kukutana na askari wa IDF ambao hawakupata shida kushuka chini na kupanda naye ardhini.

Kaid alipopewa fursa kuzungumza na Benjamin Netanyahu alimwambia wazi kuwa afanye linalowezekana ili afikie makubaliono na Hamas na ili mateka wenzake wengine waweze kuachiwa huru na salama.Katika mazungumzo hayo hakuwalaumu Hamas na wala hakumpongeza Netanyahu na askari wake kwa kumuokoa.

Rescued Israeli pleads for hostage deal with Hamas

.
Kwa kadri taarifa zinavyoendelea kuvuja inaonesha mateka hiyo aliachiliwa kwa makusudi ili awe kama mjumbe kwa Israel...
Angekosa sifa hizi then saa hizi angekuwa sehemu fulani anahadithia ancestors wake kilichomkuta kwenye mikono ya hao mabwana.
 
Hata IDF huwa wanawaandama wenye sifa kinyume na wao
 
Hichi ulicho andika unakiri mwenyewe kuwa aliokolewa. Iv unadhani angeweza kuwatoroka hamasi. Kwani hujui baada ya Hamas kujua kuwa wamefikiwa walitoroka angalia unavyojichanganya

" na siku hiyo alikuwa amewachwa peke yake kabla kukutana na askari wa IDF ambao hawakupata shida kushuka chini na kupanda naye ardhini"

Kwani ukikubali aliokolewa unapoteza nini?.
 
Hichi ulicho andika unakiri mwenyewe kuwa aliokolewa. Iv unadhani angeweza kuwatoroka hamasi. Kwani hujui baada ya Hamas kujua kuwa wamefikiwa inawezekana walitoroka angalia unavyojichanganya

" na siku hiyo alikuwa amewachwa peke yake kabla kukutana na askari wa IDF ambao hawakupata shida kushuka chini na kupanda naye ardhini"

Kwani ukikubali aliokolewa unapoteza nini?.
 
Hichi ulicho andika unakiri mwenyewe kuwa aliokolewa. Iv unadhani angeweza kuwatoroka hamasi. Kwani hujui baada ya Hamas kujua kuwa wamefikiwa walitoroka angalia unavyojichanganya

" na siku hiyo alikuwa amewachwa peke yake kabla kukutana na askari wa IDF ambao hawakupata shida kushuka chini na kupanda naye ardhini"

Kwani ukikubali aliokolewa unapoteza nini?.
Wewe ndio umechanganyikiwa.Kikawaida Hamas wanapofikiwa kwenye mateka wao huwa wanarusha risasi.Sasa huyu kwanini wakamuacha aende tu.
 
Sijajua mantiki ya mleta mada anataka nini. Ni mjinga tu ambaye anaweza kuwasifu hamas kwa kuua watu na kuwakamata mateka, hamas na wapalestina wamepata faida gani kwa mashambulizi ya October 7?

Huki wapalestina Elfu 40 wameuliwa, huku elfu 70 wameumizwa, elfu 6 wametekwa, Gaza imeharibika kwa kiwango cha 80%, tunaomba vita viishe ili amani itawale pale Gaza.
 
Mkuu milio ya risasi inaonyesha kirahisi alipo adui kuondoka kimya kimya Kuna wapa usalama wa kutokungundulika kirahisi. Hivi wafyatue risasi hovyo wao ni machizi?. Hiyo mbwa anakufukuza unadondosha pande la nyama aangaike nalo wewe unazidi kupotelea kusikojulikana. Wameachia mtu Israel waangaike nae wao wasepe. Wewe usiyejua kuwa vita ni akili unawaza kufyatua risasi tu hovyo hovyo.
 
Kwa kawaida?Ulikuwa nao siku hiyo na ukaona walivamiwa katika mazingira yepi?
 
Mateka wa Israel aliyetajwa kwa mbwembwe nyingi kwamba aliokolewa hapo juzi amekuwa kama yule bibi wa kifaransa aliyeachiliwa huru na wanamgambo wa Mali miaka miwili iliyopita.Bibi huyo alimfanya Macron afupishe muda wa kumpokea uwanjani pale alipowasifia wanamgambo wa Mali na kuahidi kurudi tena Mali kuendelea na kazi zake za huduma kwa jamii.

Kwa upande wa ndugu Kaid Farhan Elkadi mwenye umri wa miaka 52 ilitangazwa na jeshi la Israel kwamba aliokolewa katika jaribio lililokuwa la kiufundi sana.Baada ya hapo jeshi likasema halitaendelea kutoa taarifa zaidi juu ya uokoaji wake kutokana na kulinda usalama wa mateka waliobaki mikononi mwa Hamas.

Kwa kadri taarifa zinavyoendelea kuvuja inaonesha mateka hiyo aliachiliwa kwa makusudi ili awe kama mjumbe kwa Israel.Kaid ni muislamu na muarabu wa kabila la Bedui kutoka jangwa la Negev maeneo ya kusini ya Israel.

Mateka mwenyewe huyo tangu alipofika kwa watu wake amekuwa akitoa sizi hizo za uokolewaji wake.Anasema muda mwingi alikuwa yuko huru huko chini ya ardhi na siku hiyo alikuwa amewachwa peke yake kabla kukutana na askari wa IDF ambao hawakupata shida kushuka chini na kupanda naye ardhini.

Kaid alipopewa fursa kuzungumza na Benjamin Netanyahu alimwambia wazi kuwa afanye linalowezekana ili afikie makubaliono na Hamas na ili mateka wenzake wengine waweze kuachiwa huru na salama.Katika mazungumzo hayo hakuwalaumu Hamas na wala hakumpongeza Netanyahu na askari wake kwa kumuokoa.

Rescued Israeli pleads for hostage deal with Hamas

Mbona tuliambiwa lile tukio la utekaji lilikua la uongo, ni Israeli alikua anatafuta sababu ya kuingia Gaza?
 
Mkuu milio ya risasi inaonyesha kirahisi alipo adui kuondoka kimya kimya Kuna wapa usalama wa kutokungundulika kirahisi. Hivi wafyatue risasi hovyo wao ni machizi?. Hiyo mbwa anakufukuza unadondosha pande la nyama aangaike nalo wewe unazidi kupotelea kusikojulikana. Wameachia mtu Israel waangaike nae wao wasepe. Wewe usiyejua kuwa vita ni akili unawaza kufyatua risasi tu hovyo hovyo.
Walichokusudia chenye faida ilikuwa ni kumwachia Kaid arudi nyumbani akapeleke salamu kwa Netanyahu.
IDF walichungulia chini kwenye handaki kwa darubini wakamuona Kaid kakaa bila ulinzi ndio wakaamua kuteremka wakambebe.Kama Hamas huko chini kwenye malazi yao wangetaka hao IDF wala wasingefika chini kabla ya kuwapiga.
 
Mbona ni akili ndogo tu kwamba hawezi kuwa mjinga kuwaponda magaidi wa Hamas wakati wenzao bado wanashikiliwa na hao magaidi.
 
Sijajua mantiki ya mleta mada anataka nini. Ni mjinga tu ambaye anaweza kuwasifu hamas kwa kuua watu na kuwakamata mateka, hamas na wapalestina wamepata faida gani kwa mashambulizi ya October 7?

Huki wapalestina Elfu 40 wameuliwa, huku elfu 70 wameumizwa, elfu 6 wametekwa, Gaza imeharibika kwa kiwango cha 80%, tunaomba vita viishe ili amani itawale pale Gaza.
Kwa sababu hujajua sababu ya mapigano hayo ndio maana unawaona viongozi wa Gaza na sisi tunaowaunga mkono ni wajinga.
Ismael Haniye familia yake yote iliuliwa kabla ya kuuliwa mwenyewe na siku alipokufa mchana wake alikuwa ni mwenye furaha sana.Msimamo wake ni kuendelea na vita mpaka dakika ya mwisho na ndio msimamo wa wote waliomrithi kiti chake.
Tafuta mantika ya jambo hilo
 
Mbona ni akili ndogo tu kwamba hawezi kuwa mjinga kuwaponda magaidi wa Hamas wakati wenzao bado wanashikiliwa na hao magaidi.
Na kwanini wote wanaochiwa huru wanataka makubaliano na Hamas ili wenzao nao waachiliwe kama wao na wala hawataki vita viendelee.Sasa kama wakiendelea kufa nani atakuwa wa kulaumiwa.
 
Back
Top Bottom