Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mateka wa Israel aliyetajwa kwa mbwembwe nyingi kwamba aliokolewa hapo juzi amekuwa kama yule bibi wa kifaransa aliyeachiliwa huru na wanamgambo wa Mali miaka miwili iliyopita.Bibi huyo alimfanya Macron afupishe muda wa kumpokea uwanjani pale alipowasifia wanamgambo wa Mali na kuahidi kurudi tena Mali kuendelea na kazi zake za huduma kwa jamii.
Kwa upande wa ndugu Kaid Farhan Elkadi mwenye umri wa miaka 52 ilitangazwa na jeshi la Israel kwamba aliokolewa katika jaribio lililokuwa la kiufundi sana.Baada ya hapo jeshi likasema halitaendelea kutoa taarifa zaidi juu ya uokoaji wake kutokana na kulinda usalama wa mateka waliobaki mikononi mwa Hamas.
Kwa kadri taarifa zinavyoendelea kuvuja inaonesha mateka hiyo aliachiliwa kwa makusudi ili awe kama mjumbe kwa Israel.Kaid ni muislamu na muarabu wa kabila la Bedui kutoka jangwa la Negev maeneo ya kusini ya Israel.
Mateka mwenyewe huyo tangu alipofika kwa watu wake amekuwa akitoa sizi hizo za uokolewaji wake.Anasema muda mwingi alikuwa yuko huru huko chini ya ardhi na siku hiyo alikuwa amewachwa peke yake kabla kukutana na askari wa IDF ambao hawakupata shida kushuka chini na kupanda naye ardhini.
Kaid alipopewa fursa kuzungumza na Benjamin Netanyahu alimwambia wazi kuwa afanye linalowezekana ili afikie makubaliono na Hamas na ili mateka wenzake wengine waweze kuachiwa huru na salama.Katika mazungumzo hayo hakuwalaumu Hamas na wala hakumpongeza Netanyahu na askari wake kwa kumuokoa.