Israel sio mtu wa Mazungumzo na magaidi. Kama Iran iliua muisrael yoyote hiyo imekula kwao. Mazungumzo ya Marekani na Iran si chochote kwa Israel.
Waziri mkuu kashawapa funguo Wanajeshi wake waue gaidi popote watakapo muona. Yaani Wasisubiri ruhusa. Marekani anakubalije Mazungumzo wakati Israel hajafiikia Malengo?
Iran wakae chonjo. Israel si muumini wa Mazungumzo kama hajafikia malengo
Sijui umeandika hii thread kwa sababu ya upeo mdogo wa Kutojua kile ulichoandika, au ni kwa sababu ya mahaba yako kwa Israel!!
Kila mtu anajua kwamba bila Marekani Israel haiwezi kamwe kupambana na Iran. Na hilo lilithibitishwa mwaka jana na mwaka huu.
Mwaka jana Israel ilianzisha mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya Iran, lkn baada ya Iran kuiangamiza Israel kwa muda wa siku 12, Israel iliiomba Marekani ije kuisaidia kushambulia eneo la vinu vya nuclear pale Iran. Ambapo kweli Marekani baada ya kuona Israel imeomba msaada na inapumulia machine ikaja kusaidia na kisha kuomba usitishaji wa vita. Kumbuka mpaka hapo ni Marekani na Israel kupitia Trump ndio walioratibu ceasefire mwaka jana, na sio Iran.
Mwaka huu ndo kabisa Israel iliogopa kui face Iran peke yake, Netanyahu akapiga trip zaidi ya 6 Marekani kuomba msaada wa kusaidiwa kupambana na Iran. Yule bwege kiazi Trump akakubali na kufikiri kuwa wakiwa nchi 2 pamoja wataweza kuipiga Iran na kumuweka yule puppet wao mtoto wa mfalme madarakani na kuliangamiza jeshi lote la Iran kama Gaza.
Lakini pia na huku mambo yamekwenda vibaya zaidi kuliko mwaka jana, kwa Iran kuishangaza dunia kuhusu uwezo wake wa kushambulia nchi zaidi ya 7 zikiwemo Israel na Marekani, kila siku kwa muda wa siku 40 bila kulalamika kuishiwa silaha, wala kuomba msaada wa kijeshi kutoka nchi nyingine.
Ni Israel na Marekani ndio zilizokuwa zinaomba msaada wa kijeshi kutoka nchi nyingine za NATO. Na vyombo vya ulinzi vya Israel kuanza kulalamika kuhusu upungufu wa mifumo ya ulinzi, pamoj na silaha kwa ujumla. Hii imesababisha Trump mwenye jeshi kubwa duniani kuomba poo kwa nguvu ili vita iishe. Iran ilikataa katakata kusimamisha nguvu lkn Marekani ikalazimisha kutumia mpaka nchi zenye uhusiano mzuri na Iran ziishawishi ikubali kusimamisha vita ili Marekani na Israel wapate pa kutokea kwenye vita hiyo ngumu kwao.
Kuna msemo unaosema mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni.
Kwa aina ya vita ilivyokuwa kama ingekuwa ni Israel ndio imevamiwa na nchi mbili mfano Iran ijiunge na China kuivamia Israel nakuhakikisha saa hizi Israel ingekuwa imeshatekwa zamani.