Israel haiwezi kaa wiki mbili bila kufanya tukio Iran

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Israel sio mtu wa Mazungumzo na magaidi. Kama Iran iliua muisrael yoyote hiyo imekula kwao. Mazungumzo ya Marekani na Iran si chochote kwa Israel.

Waziri mkuu kashawapa funguo Wanajeshi wake waue gaidi popote watakapo muona. Yaani Wasisubiri ruhusa. Marekani anakubalije Mazungumzo wakati Israel hajafiikia Malengo?

Iran wakae chonjo. Israel si muumini wa Mazungumzo kama hajafikia malengo
Your browser is not able to display this video.

​
 
Sijui umeandika hii thread kwa sababu ya upeo mdogo wa Kutojua kile ulichoandika, au ni kwa sababu ya mahaba yako kwa Israel!!

Kila mtu anajua kwamba bila Marekani Israel haiwezi kamwe kupambana na Iran. Na hilo lilithibitishwa mwaka jana na mwaka huu.

Mwaka jana Israel ilianzisha mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya Iran, lkn baada ya Iran kuiangamiza Israel kwa muda wa siku 12, Israel iliiomba Marekani ije kuisaidia kushambulia eneo la vinu vya nuclear pale Iran. Ambapo kweli Marekani baada ya kuona Israel imeomba msaada na inapumulia machine ikaja kusaidia na kisha kuomba usitishaji wa vita. Kumbuka mpaka hapo ni Marekani na Israel kupitia Trump ndio walioratibu ceasefire mwaka jana, na sio Iran.

Mwaka huu ndo kabisa Israel iliogopa kui face Iran peke yake, Netanyahu akapiga trip zaidi ya 6 Marekani kuomba msaada wa kusaidiwa kupambana na Iran. Yule bwege kiazi Trump akakubali na kufikiri kuwa wakiwa nchi 2 pamoja wataweza kuipiga Iran na kumuweka yule puppet wao mtoto wa mfalme madarakani na kuliangamiza jeshi lote la Iran kama Gaza.

Lakini pia na huku mambo yamekwenda vibaya zaidi kuliko mwaka jana, kwa Iran kuishangaza dunia kuhusu uwezo wake wa kushambulia nchi zaidi ya 7 zikiwemo Israel na Marekani, kila siku kwa muda wa siku 40 bila kulalamika kuishiwa silaha, wala kuomba msaada wa kijeshi kutoka nchi nyingine.

Ni Israel na Marekani ndio zilizokuwa zinaomba msaada wa kijeshi kutoka nchi nyingine za NATO. Na vyombo vya ulinzi vya Israel kuanza kulalamika kuhusu upungufu wa mifumo ya ulinzi, pamoj na silaha kwa ujumla. Hii imesababisha Trump mwenye jeshi kubwa duniani kuomba poo kwa nguvu ili vita iishe. Iran ilikataa katakata kusimamisha nguvu lkn Marekani ikalazimisha kutumia mpaka nchi zenye uhusiano mzuri na Iran ziishawishi ikubali kusimamisha vita ili Marekani na Israel wapate pa kutokea kwenye vita hiyo ngumu kwao.

Kuna msemo unaosema mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni.

Kwa aina ya vita ilivyokuwa kama ingekuwa ni Israel ndio imevamiwa na nchi mbili mfano Iran ijiunge na China kuivamia Israel nakuhakikisha saa hizi Israel ingekuwa imeshatekwa zamani.
 
🤣🤣🤣 Tatizo ni kwamba Israel anakubali vip wakati makubaliano ni Iran na USA ,hapo ndipo dharau inapokuja🤣🤣.. Israel kumvaa Iran peke yake hawezi na hapo Trump katishwa sana mpaka akashikiri mashambulizi.

Yeye aendelee tu bila ya USA aone ..Kama ikipita wiki mbili basi Iran atakuwa amerudisha nguvu zake upya kwa aslimia 70. Kitu ambacho Israel hataki kabisa.


 
Hiyo kusitisha vita yeye ndiye aliyeomba huyoo, kapigwa kapigika akili zake zimerudi, alitaka mabadiliko ya utawala Iran ameyapata mabadilikoo yakutosha kabisa akaondoe vifusi
 
Ukipunguza mihemko unaweza kujenga hoja ikajibiwa. Huna haja ya kutumia matusi na lugha chafu ili uelweke.

Ila kwa ufupi sitisho ni la Marekani si Israel. Utaona.. Viongozi wa Iran wajiachie kwa kuamini sitisho
 
Upo sahihi. Israel aungwe mkono au asiungwe mkono, akishaamua mpango wake lazima autimize.
 
Hiyo kusitisha vita yeye ndiye aliyeomba huyoo, kapigwa kapigika akili zake zimerudi, alitaka mabadiliko ya utawala Iran ameyapata mabadilikoo yakutosha kabisa akaondoe vifusi
Una uhakika wa kupigwa akapigika? Mtu anapigana vita na watu wanne kwa wakati mmoja. Uzuri Israel aliweka wazi mapema. Atadeal na viongozi pamoja miundombinu ya kijeshi. Pia madaraja yote yyanayopitisha Silaha yatalipuliwa
 
Una uhakika wa kupigwa akapigika? Mtu anapigana vita na watu wanne kwa wakati mmoja. Uzuri Israel aliweka wazi mapema. Atadeal na viongozi pamoja miundombinu ya kijeshi. Pia madaraja yote yyanayopitisha Silaha yatalipuliwa
Hii ni mara ya 2 Netanyahu anajaribu kucheza kamari kwa Iran na mara zote ameomba poo, Netanyahu anashirikiana na jeshi la US mkuu, yeye kama yeye hawezi kumudu ata vita ya masaa 24., na uliona wewe kwenye uwanja wa vita hata US ilibidi aombe msaada kutoka Nato.

Vita si maneno tunaangalia ukiwa field uwezo wako ni upi ni kama vile mpira ongea utakavyoongea lakini pitch ndio itaamua, Uwezo wa Iran siku zote waemkuwa wakisema hauko kwa mtu mmoja mmoja/kiongozi individual, Iran ni Taasisi kubwa ambayo wamejiandaa zaidi ya miaka 47, aliuliwa Khomeney lakini je uliona kuyumba kwa jeshi la Iran? wale jamaa achana nao wameishangaza dunia hizo siku 38

Imagine wewe unasema Israel na US wamepigana na nchi 4, kwani Iran 1 amepiga nchi ngapi? Amewapiga Israel, US, Bahrain, Saudia, Qatar, Kuwait huko Gulf kote mpaka Trump alipoomba kusitisha vita kwa lazima.
 
Ukipunguza mihemko unaweza kujenga hoja ikajibiwa. Huna haja ya kutumia matusi na lugha chafu ili uelweke.

Ila kwa ufupi sitisho ni la Marekani si Israel. Utaona.. Viongozi wa Iran wajiachie kwa kuamini sitisho
Hakuna sehemu jamaa aliyotumia lugha chafu,bali ukweli umekugusa.
Una uelewa finyu kuhusu haya mambo.
Kwani vita ya siku 12 mwaka jana iliishaje? Si Israel aliomba USA amsaidie ceasefire!?
Na hata vita hii ni vivyo hivyo,hata hiyo Israel inafahamu Iran sio nchi ya kucheza nayo,hiyo nchi ikisema inapigana hata miaka 10 inakatika na hawasimami. Embu kaisome vita ya Iraq 1980 iliyoisha 1988. Ndio utaijua Iran vizuri.
 
Una uhakika wa kupigwa akapigika? Mtu anapigana vita na watu wanne kwa wakati mmoja. Uzuri Israel aliweka wazi mapema. Atadeal na viongozi pamoja miundombinu ya kijeshi. Pia madaraja yote yyanayopitisha Silaha yatalipuliwa
Embu wacha kudanganya kama hujui kitu. Israel ni watu gani wanne anaopigana nao!?? Hao Hizbollah na Houthi waliojiunga na Iran ama!??
Pia usitudanganye,lengo la Israel lilikua ni total decapitation of Iran. Ndio maana amelipua mashule,vyuo vikuu,vyuo vya elimu ya kati,viwanda vya kiraia,viwanda vya madawa,vituo vya afya na hospitali zaidi ya 30. Lengo lao yeye na USA ilikua kuivunja mazima Iran kiuchumi.
Na walijiandaa kulipua visiwa vya hifadhi ya mafuta vya Kharg,ndipo Iran ikawatishia ndio maana wakaogopa na kuacha.
Embu fanyeni utafiti kabla hamjaongea huwenda mkapunguza kuongea uongo.
 
Njoo na ID zote. Lakini ukweli nimekuambia
 
Njoo na ID zote. Lakini ukweli nimekuambia
Bado unadhihirisha upeo wako finyu. Kwahiyo mtu akikupinga unamjumuisha na huyo jamaa kuwa anatumia ID tofauti!??
Hakuna ukweli wowote ulioongea,pale hakuna lugha chafu iliyotumika,kama ipo embu i bold tuione.
 
The war has started again.
The US and Israel have reportedly broken the ceasefire and attacked an oil refinery in southern Iran, according to Iranian television station Press TV.
Your browser is not able to display this video.
 
Ukipunguza mihemko unaweza kujenga hoja ikajibiwa. Huna haja ya kutumia matusi na lugha chafu ili uelweke.

Ila kwa ufupi sitisho ni la Marekani si Israel. Utaona.. Viongozi wa Iran wajiachie kwa kuamini sitisho
Tatizo lenu nyinyi hata kitu msichokijua hampendi kufunzwa. Na mkiambiwa ukweli mnadai mmetukanwa. Hivi unaelewa maana ya tusi kweli?

Unaweza kuniambia au kunionesha tusi nililokutukana? Au siku hizi mtu kuambiwa ukweli na kufunzwa kile asichokijua ni tusi?

Kifupi Marekani ndio kiongozi wa vita, na hiyo Israel yako ni kakimvuli tu kalikojificha nyuma ya dubwasha linaloitwa Marekani. Nakuhakikishia kuwa Marekani akijitoa kweli kwenye vita hii. Basi Israel haitokuwa na uwezo wa kuingia vitani na Iran hata kwa week 2 bila kuomba msaada mungine Marekani, au kumuomba Trump aitishe ceasefire nyinyine kwa ajili yao.

Iran ni taifa ambalo limeshakutana na vita nyingi toka miaka 6000 iliyopita. Na hakuna vita hata 1 iliyowahi kushindwa na nchi kuingia kwenye mikono ya adui.

Hii ndio sababu maraisi wote wa Marekani hawakuwahi kukubali kuingia vitani na Iran, japo Israel ilikuwa inalia lia kila siku ipate msaada wa wa kuivamia Iran kupitia usaidizi wa Marekani. Hilo liko wazi na viongozi wengi wameliongelea.
 
Ila israel kuanzia raia wao hadi viongozi wao muda wote wanatamani kuendelea kuchapana tu na maadui wao...nimeona kuna kiongozi wao mmoja wa upinzani anammaindi hatari Netanyau kwanini amekubari kusitisha vita kupisha maridhiano.
 
Mtoa Mada acha kula nguruwe ili minyoo isiendelee kuharibu ubongo wako sehemu iliyobakia tafadhali,vita ni mchezo wa wazi sote tumeona piga nikupige.

Ile dhana ya taifa teule haliguswi kwisha habari yao,kama yeye taifa teule ana hiyo jeuri basi atupe hata jiwe Iran aone moto wake.

Shoga huwezi kushindana na mwanaume ambae aliekamilika,nguvu ya mwanaume inaanzia matakoni sasa ikiwa watu washayapukutisha hiyo kuvu utaitoa wapi.

Muda aa kuwaambia wachunga wenu kwamba hadith za taifa teule kwisha.
 
Iran hii iliyomalizwa viongozi wote?

Hii ya magaidi ?

Iran hii ya sasa imevamiwa na waislamu mwaka 651AD ,
 
Dah ubarikiwe san mkuu kwa kusimamia ukweli na kumfunza jamaa mengi asiyoyajua. Vijana wanakutana barabarani na kuja na taarifa za hovyo jukwaani. Afu tukiwaelimisha wanadai wametukanwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…