Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mnamo taehe 29 Agosti ndege ya abiria ya Sychelles ikiwa na abiria 128 ilipata matatizo ya kiufundi ikiwa angani eneo la Saudi Arabi. Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na abiria watalii wa kiyahudi wakiwemo maofisa wa serikali waliokuwa likizo.
Ndege ilipofika uwanjani abiria wote wakapatiwa huduma muhimu za ukarimu mkubwa na mamlaka ya uwanja wa ndege.
Hilo tu likamfanya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa anaangalia ramani ya eneo la mashariki ya kati aseme:“I greatly appreciate the warm attitude of the Saudi authorities to the Israeli passengers whose flight was in distress,”
Siku mbili nyuma yake waziri wa mambo ya nje wa Israel Eli Cohen alimnyemelea waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Libya Najla al-Mangoush walipokuwa pamoja kwenye hoteli nchini Italia na kuanza kuzungumza naye mambo ya urafiki wa nchi yake na nchi hiyo ya kaskazini ya Afrika.
Kibaya zaidi Eli Cohen alichukua selfie na Najla na kuirusha kwenye mitandao. Picha hiyo ilisababisha vurugu kubwa Libya kutoka kwa wananchi walioandamana kupinga mahusiano na Israel.
Dada Najla ikabidi asimamishwe kazi kwa muda na kuitwa kujieleza.Maskini dada Najla anasema wala hakukusudia kufanya mazungumzo na waziri huyo.Yeye ndiye aliyelazimisha mazungumzo hayo na kumtangaza vibaya.
Pamoja na hivyo Naija Mangoush akasema hakuwahi kukubaliana na Eli chochote na hawezi kufanya hivyo kinyume na sera ya Libya kutokuwa na uhusiano na Israel mpaka suala la wapalestina litakapopatiwa ufumbuzi.