GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Angalia!
~ Nchi yetu ni kubwa mara kadhaa kuizidi. Tanzania ina kilomita za mraba 945,087 wakati Israel ina kilomita za mraba 22,145 tu.
~ Sehemu kubwa ya ardhi ya nchi yetu inafaa kwa kilimo wakati kwa Israeli, nusu ya ardhi ni jangwa. Ni asilimia ishirini tu ya ardhi yote ya Israel ndiyo ifaayo kwa kilimo.
Ingawa asilimia 49.7 ya ardhi yetu inafaa kwa kilimo, inayotumika kwa kilimo ni chini ya asilimia 35.
~ Wakati Israel inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya chakula chake, Tanzania ingali ikikabiliwa na upungufu wa chakula. Kuna miaka iliilazimu Serikali kutoa chakula cha msaada kwa baadhi ya raia wake kwa ajili ya kukabiliana na baa la njaa.
Kwa jinsi tulivyo na ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo, vyanzo vya uhakika vya maji kama maziwa, mito, n.k., ilistahili Tanzania iwe na uwezo wa kuihudumia alau Afrika Mashariki yote kwa chakula.
Hata Israel, ilipaswa kuja kujifunza masuala ya kilimo Tanzania, lakini imekuwa kinyume chake.
Miaka ya sabini, Israel ilianzisha skimu ya umwagiliaji nchini Tanzania, mradi ambao ulisitishwa baadaye baada ya baba wa Taifa, Mwl J. K. Nyerere kuuvunja uhusiano na Israel.
Hata sasa, kuna Watanzania nchini Israel wanaojifunza shughuli za kilimo na ufugaji wa kisasa.
Kwa nini imekuwa hivyo?