Israel inatambulika kwenye Biblia na Quran, Palestina hatajwi popote

Israel inatambulika kwenye Biblia na Quran, Palestina hatajwi popote

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
9,818
Reaction score
14,585
Screenshot_20260309_093113_Google.jpg


Uchambuzi wa maandiko matakatifu ya Biblia na Quran unaonyesha kuwa neno Israel lina mizizi ya kina na ya wazi katika vitabu vyote viwili, huku neno Palestina likikosekana kama jina la nchi au taifa ndani ya maandiko hayo ya asili.

Katika Biblia, neno Israel linatokea zaidi ya mara 2,500. Jina hili lilianza kama utambulisho wa Nabii Yakobo (Mwanzo 32:28) na baadaye likawa jina la taifa la "Wana wa Israel." Biblia inataja nchi hiyo kama "Ardhi ya Israel" (Eretz Yisrael). Kwa upande mwingine, neno Palestina linatokea mara chache kama "Ufilisti," likimaanisha eneo dogo la pwani na si nchi nzima.

Katika Quran, neno Israel linatajwa mara nyingi, likimrejelea Nabii Yaqub (A.S) na uzao wake unaojulikana kama Bani Israil. Quran inatambua ukoo huu na kuelezea safari zao za kiimani na kisheria. Hata hivyo, neno "Palestina" halijatajwa hata mara moja ndani ya Quran. Badala yake, Quran inatumia sifa kama "Ardhi Takatifu" (Al-Ard al-Muqaddasah)

Israel inatambulika kimaandiko katika Biblia na Quran kama jina la mtu na taifa teule la kale. Palestina, ingawa ni ukweli wa kijiografia na kihistoria wa baadaye, haikutajwa kwa jina hilo ndani ya maandiko hayo ya kidini.
 
Huo ni ukweli kabisa. Neno "Palestina" linatokana na neno la Kiebrania "Peleshet", ambalo linamaanisha "nchi ya Wafilisti." Katika tafsiri za kale za Kigiriki (Septuagint) na baadaye Kilatini (Vulgate), neno hili lilirekodiwa kama Palaestina.

Mwaka 135 BK Warumi walilibadilisha jina la mkoa mzima wa Yudea na kuuita "Syria Palaestina" ili kufuta utambulisho wa Kiyahudi baada ya uasi. Hapo ndipo jina "Palestina" lilipoanza kutumika kuelezea eneo lote kati ya Mto Yordani na Bahari ya Mediterania

Cc Malaria 2, Ritz FaizaFoxy, Mohamed Said
 
Hao waisrael wa sasa mnao sema wametajwa katika QURAN na Biblia wgao hawazitambui hivyo vitabu. na ieleweke israel hii inayoifahamu imeundwa mwaka 1948
 
Ni uzi wa kuelimishana ila subiri nikavae talawanda zangu nije nikubishie tu bila sababu wala uhakika.
 
Sasa wewe hata elimu ya hao watu huna .
Hao ni Jewish population, qur an imezungumzia Israelites.

Watofautishe kwanza halafu uje tuendelee.
 
Hao waisrael wa sasa mnao sema wametajwa katika QURAN na Biblia wgao hawazitambui hivyo vitabu. na ieleweke israel hii inayoifahamu imeundwa mwaka 1948
Waisrael hawaitambui Aganonla Kale lililoko kwenye Biblia? Au unajiropokea tu.
 
Back
Top Bottom