Israel is committing War Crimes

Israel is committing War Crimes

Leo nimeona kuna myahudi wa miaka 50 ameuawa na roketi iliyorushwa na magaidi ya kipalestina kwanini duniani inaacha kukemea huu unyama unaofanywa na wapalestina kurusha maroketi na kuuawa Waisraeli?

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Umeona myahudi mmoja tu ujaona watoto chini ya miaka 8 walivyouliwa uko Gaza?

Eti na wewe ni baba wa familia
 
Juzi tu mlikuwa mnawasifia wapalestina kuwa tumefanikiwa kurusha makombora yalioingia kwenye makazi ya Izrael na kufanya uharibifu pamoja na mauwaji. Leo baada ya Izrael kuanza kujibu mashambulizi mmasema sijui War Crimes
Nilijua tu mdaa si mrefu furaha ya kuishangilia Palestina inaporusha maroketi itageuzwa kilio na Israel mda si mrefu walioishabikia Palestina inaporusha maroketi sasa hivi wanasema israel inawaonea wapalestina baada ya israel kujibu mapigo

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
Upumbavu nao ni kipaji. Watanzania kama wewe ni wa kudharau kabisa mnafurahia udhalimu wa kutisha dhidi ya binadamu wengine bila hata kujua kiini cha tatizo husika.
Nina uelewa mpana wa mgogoro huo na Mashariki ya Kati kwa ujumla. Ila nasema Israeli apige na kuvunja vunja vyombo vya kikuda vya habari kama alivofanya majuzi ili ngozi nyeusi akili ziwarudi kuwa ICC hufanya kazi kwa kuchambua wahanga.
 
Huo ujasiri unaouheshimu hamasi na kuwapa big up. Ndiyo unaosababisha unaona watoto wanaokolewa kwenye majengo yanayoanguka kwa kudunguliwa na mabom
Ni heri uwe na ujasiri ulio na gharama kuu kuliko uoga usio na gharama!

Against all odds…Hamas wanapambana na jeshi la Marekani kupitia Israel!

Nuff respect to them.

Wanaume wa Dar wakisikia tu maneno ‘Panya Road’, wanakimbia!

🤣
 
Unaposema Israel bila Marekani haina chochote, it's because you're not seeing the bigger picture!

Huyuhuyu Biden ambaye ni rais wa Marekani (Israel's no. 1 ally) unategemea amkemee ama amfokee Netanyahu? Urusi hii ya Putin ambaye amezungukwa na Wayahudi katika power circle yake, unategemea amkemee Netanyahu ambaye pia ni swahiba wake?

Kilichopo hapo ni masilahi tu. Mataifa makubwa na yenye nguvu karibu yote tunayoyafahamu duniani yana masilahi na Israel zaidi kuliko Wapalestina katika hili.

Marekani, Uingereza, Urusi, Ufaransa, Ujerumani n.k. zote zinakubaliana kwamba Israel ina haki ya kujilinda, unategemea kitu gani?

Hiyo ndiyo hali halisi!
Israel ina haki ya kujilinda ila Wapalestina hawana haki hiyo?

Israel ina haki ya kuwafukuza Wapalestina toka kwenye ardhi yao?

Wapalestina hawana haki ya kujilinda?

Hayo maslahi ambayo hizo nchi ulizozitaja ni maslahi gani hasa mpaka yazidi maslahi ya uhai wa binadamu wa Kipalestina?

Bullshit way of thinking!

Haina tofauti na kuhalalisha biashara ya utumwa na kusema ilikuwa ni ya maslahi ya Wazungu kuliko maslahi ya heshima na ubinadamu wa Mwafrika, na hivyo ndo maana ilikuwa ni sawa tu ilipofanyika wakati huo.

Hakuna maslahi yoyote hapa duniani yaliyo na thamani kushinda uhai wa binadamu wasio na hatia yoyote ile.

Hakuna. Period, end of sentence!
 
Leo nimeona kuna myahudi wa miaka 50 ameuawa na roketi iliyorushwa na magaidi ya kipalestina kwanini duniani inaacha kukemea huu unyama unaofanywa na wapalestina kurusha maroketi na kuuawa Waisraeli?

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
Mimi nakemea uovu wowote ule unaofanywa dhidi ya mtu asiye na hatia.

Na kwa msingi huo, nawakemea pia Hamas kwa kuwalenga raia wa kawaida wa Israel wasio wanajeshi!

Mtu ukiwa unasimamia kanuni huwa hakuna shida ya kuukemea uovu popote pale unapotokea maana sisukumwi na dini, jinsia, utaifa, ukabila, wala rangi ya ngozi.

Comparative condemnation…
 
Israel bila Marekani haina chochote!

Biden…huyo Democrat mpenda amani asiye mbaguzi wa rangi, dini, wala jinsia…yeye kama kiongozi wa taifa kubwa linalolikingia kifua Israel, kwa nini aachie huu unyama wa Israel dhidi ya Wapalestina uendelee?

Leo nimeona kuna kabinti kameokolewa kutoka kwenye jengo lililopigwa mabomu na hao wahalifu wa Israel. Imeniuma sana.
Lakini unajua nini…fcuk Biden!

Hawezi kumfokea huyo Netanyahu na kumwambia akome huo unyama wake?

Wachina na Warusi kwa nini wanaachia huu uhalifu uendelee? Au hawana ubavu kama wanavyodai?

Massive big up kwa Hamas. Ujasiri wao nauheshimu sana.
Wajinga kama wewe wanaongea upumbavu mtupu.. leo Bennet kawauliza RT kama gaidi alipiga bom Moscow au London au Washington watachekelea tu bila kufanya chochote? Sasa Hamas anavyofyatua rocket unataka Israel atulie tu na hao watoto wanatumiwa kama human shield ni ungese wa hamas wanataka huruma kama zako.. ila ujinga ulishapitwa na wakati Waziri wa ulinzi wa zamani kasema... kama ni kuvunja haki za kibinadamu wakachunguze location zote hamas wanazotumia kirusha rockets zao.. ndipo mtapata akili nyie majinga.. vita fuatilieni matukio sio kujiongelea tu hovyo kama maarabu majinga
 
"Israel is using bombs to protrct civilian mean while Hamas are using civilian, mosques, news room, hospital and refugee camps to protect BOMBS" Izrael un ambassador
 
Binadamu huwa hatueleweki kabisa tunataka nini?
Si humu humu kuna watu walikuwa wanatoa kashfa juu ya Israel?Sasa inakuwaje tena hao wanaopigika wanaonewa huruma ,je wakati wanarusha ya makombora kule Israel hawaishi wamama na watoto?Au watoto wapo tu Palestine?
Hamas ni wahuni kama wahuni wengine tu kwa mtindo huo...tuache unafiki kidogo mbele ya hilo.
 
Israel ina haki ya kujilinda ila Wapalestina hawana haki hiyo?

Israel ina haki ya kuwafukuza Wapalestina toka kwenye ardhi yao?

Wapalestina hawana haki ya kujilinda?

Hayo maslahi ambayo hizo nchi ulizozitaja ni maslahi gani hasa mpaka yazidi maslahi ya uhai wa binadamu wa Kipalestina?

Bullshit way of thinking!

Haina tofauti na kuhalalisha biashara ya utumwa na kusema ilikuwa ni ya maslahi ya Wazungu kuliko maslahi ya heshima na ubinadamu wa Mwafrika, na hivyo ndo maana ilikuwa ni sawa tu ilipofanyika wakati huo.

Hakuna maslahi yoyote hapa duniani yaliyo na thamani kushinda uhai wa binadamu wasio na hatia yoyote ile.

Hakuna. Period, end of sentence!
Sawa! Uhai wa binadamu ni wa thamani. Lakini, tazama uhalisia wa mambo jinsi ulivyo katika dunia kwa ujumla. Dunia ina mataifa mengi na kila taifa lina masilahi yake na watu wake.

Uhai wa binadamu hauwezi kuwa na thamani sawa dunia nzima kama kila nchi na jamii za watu zina masilahi yao tofauti. Huo utofauti wa kimasilahi ndiyo unaoleta vita baina ya nchi mbalimbali. Huo utofauti wa kimasilahi ndiyo unaosababisha vifo vya "watu wasio na hatia".

Unauliza kama Wapalestina wana haki ya kujilinda lakini, wanajilinda kupitia nani? Hamas? Kundi ambalo nchi kadhaa za jumuiya ya kimataifa zinalitambua kama kundi la kigaidi?

Tunarudi palepale kwenye masilahi. Haya ambayo unayaona Israel inayafanya kwa masilahi ya watu wake, yamekwishafanywa pia na mataifa yote makubwa na yenye nguvu hapa duniani kwa masilahi ya mataifa yao na watu wao.

Kamwe, dunia haiwezi kuwa na kauli moja kuhusu thamani ya binadamu endapo kila jamii na nchi itapigania masilahi yake. Hiki ni kikwazo kikubwa!
 
Wajinga kama wewe wanaongea uoumbavu mtupu.. leo Bennet kawauliza RT kama gaidi alipiga bom Mosqow au London au Washington watachelelea tu bila kufanya chochote? Sasa Hamas anavyofyatua rocket unataka Israel atulie tu na hao watoto wanatumiwa kama human shield ni ungese wa hamas wanataka huruma kama zako.. ila ujinga ulishapitwa na wakati Waziri wa ulinzi wa zamani kasema... kama ni kuvunja haki za kibinadamu wakachunguze location zote hamas wanazotumia kirusha rockets zao.. ndipo mtapata akili nyie majinga.. vita fuatilieni matukio sio kujiongelea tu hovyo kama maarabu majinga
Kuandika tu kwa usahihi kunakushinda, halafu unathubutu kuniita mjinga?

Ni wazi hujui maana ya ujinga ni nini!

Sina hata haja ya kuvipangua viroja vyako kwa kutumia hoja!
 
Israel has destroyed the tower block housing Al Jazeera and the Associated Press news agency in Gaza.

They are doing this for one reason - to stop the truth being known about their assault on the Palestinian people. Share this and show the truth!
View attachment 1786517
Hamas started this war!! I am wondering why you are not blaming them instead your spreading propaganda against Israel??
 
Naona dunia imeamua kuvaa miwani ya mbao kana kwamba kinachoendelea kwa ndugu na binadamu wenzetu wa Palestine hatukioni, Hata mataifa yanayoweza kutunishiana msuli kidogo na marekani nayo yapo kimya hamas wanapambana na hata Communities za kimataifa hazitaki kuwatambua badala yake wamewapa jina la waasi, Israel anafanya yote hayo kwa vile Marekani yupo nyuma yake, Hata mifumo kama iron dome ya ku intercept Missle amepewa huko, Sio UN wala nini kila mtu kimya
 
Sawa! Uhai wa binadamu ni wa thamani. Lakini, tazama uhalisia wa mambo jinsi ulivyo katika dunia kwa ujumla. Dunia ina mataifa mengi na kila taifa lina masilahi yake na watu wake.

Uhai wa binadamu hauwezi kuwa na thamani sawa dunia nzima kama kila nchi na jamii za watu zina masilahi yao tofauti. Huo utofauti wa kimasilahi ndiyo unaoleta vita baina ya nchi mbalimbali. Huo utofauti wa kimasilahi ndiyo unaosababisha vifo vya "watu wasio na hatia".

Unauliza kama Wapalestina wana haki ya kujilinda lakini, wanajilinda kupitia nani? Hamas? Kundi ambalo nchi kadhaa za jumuiya ya kimataifa zinalitambua kama kundi la kigaidi?

Tunarudi palepale kwenye masilahi. Haya ambayo unayaona Israel inayafanya kwa masilahi ya watu wake, yamekwishafanywa pia na mataifa yote makubwa na yenye nguvu hapa duniani kwa masilahi ya mataifa yao na watu wao.

Kamwe, dunia haiwezi kuwa na kauli moja kuhusu thamani ya binadamu endapo kila jamii na nchi itapigania masilahi yake. Hiki ni kikwazo kikubwa!
Maslahi ya uhai wa binadamu wasio na hatia hayana mjadala!

Hata sheria za kimataifa zinalitambua hilo.

Uhai wa binadamu kwanza, halafu mengine ndo yanafuatia.

Huwezi kuhalalisha ukiukwaji wa haki na uhai wa binadamu kwa kisingizio cha maslahi yako.
 
Back
Top Bottom