Israel kuivamia Iran, imefanya uamuzi wa kijinga

Yaan unajifanya una akili na unajiona umefanya uchambuzi bora kabisa kuliko waisrael wenyewe wanaopigana dhidi ya adui aisee
Taifa lolote lenye viongozi makini haliwezi kuingia vitani kwasababu za kijinga kama za Israel
 
kwahiyo mtu akiwa muuza vitumbua hawezi kuwa mtaalamu wa jambo fulan
 
Kwa hiyo wewe ndiye umeishi muda mrefu kuliko taifa la Israel,ulionao hatari ya Iran kuwa tishio kwa Israel,umetafakari sana kuliko Israel,ukachambua faida na hasara za vita hiyo kuliko Israel na ulishayajua malengo halisi ya Israel kuhusu hiyo vita?
ukisoma tena na tena nilichokiandika utaelewa
 
Ukifuatilia historia kati ya Israel na Iran utagundua kuwa ugomvi wao ni wa kihistoria,kama utakuwa umesoma kisa cha Hamani aliyetoa waraka wa kuwaangamiza wayahudi wote,utagundua kuwa Iran ndiye mchokozi na mwanzilishi wa vita vyote vinavyoendelea.

Kuanzia kipindi hicho cha akina Haman mpaka sasa Iran hajawahi kuacha nia yake ya kulifuta taifa la Israel,mashambulizi yote yanayofanywa na vikundi vyote vya Hezbollah, Hama's,na kile cha Yemen vinavyoishambulia Israel,ni Iran inaishambulia Israel kwa kutumia vikundi hivyo.

Kwa nia ileile ya kutaka kuwaangamiza wayahudi Iran imekusudia kutengeneza silaha za nuclear ambazo ni hatari zaidi na zinazoangamiza zaidi ya silaha zinazoipiga Israel hivi sasa.

Israel imeamua kujibu kile kinachofanywa na Iran kupitia nyuma ya mgogo wa Hama's,Hezbollah na Yemen kwa kuishambulia Iran moja kwa moja kwa ajili ya kujihami na kyama cha kushambuliwa na silaha za nuclear endapo Iran ambayo adhima yake ni kulifuta taifa la Israel itaachiwa nafasi ya kumiliki silaha hizo.
 
sina hakika kama jamaa ametaja dini kabisa.
 
Natanyahu kaivamia irani ili ajiokoe yeye mwenyewe maana alikuwa afungwe kwa kesi ya ufisadi,sasa njia ya kujiokoa ndio hiyo kuzusha nita isiyokuwa na msingi wowote
 
Umeropoka sana tena uongo mwingi.
Mie nitakurekebisha huko chini tu,maafisa wa IAEA wamesema Iran Haina haja ya kuunda silaha za nuke.
Na Ayatollah Khamenei alikataa kutoa ruhusa ya kuunda silaha za maangamizi alidai dini airuhusu.
Muwe mnafanya tafiti kabla ya KUROPOKA.
 
Nilichosema kwa kuropoka kwa mjibu wako ndio ukweli wenyewe ulichosema we we pasipo kuropoka ndio uongo wenyewe,kama unashindwa kujua hata hili la Iran kufadhiri vikundi vya ugaidi kuishambulia Israel ukweli wako uko wapi?hill la kusema kuwa Ayatollah alikataa kutoa ruhusa ya kuunda silaha za maangamizi kwa madai kuwa dini hairuhusu ndio ukweli wako?wakati zipo nchi za dini ya Ayatollah zinamiliki silaha za nuclear.
 
Wewe na Mr.Grossi mkuu wa IAEA nani anasema ukweli??
Embu nenda kamsome Grossi hata asubuhi hii aliongea niliyosema hapo juu.
Endelea kuropoka tena,ukikosea kubali kuelekezwa.
Grossi alisema wazi kabisa Iran ilikatazwa na Supreme leader kuunda Nuke weapons na hiyo ripoti ndio wako nayo sasa IAEA.
Nenda kabishane nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…