Kwa wasomi wa Biblia hiyo habari siyo mpya. Toka mwanzo hawa jamaa hawakumtaka Yesu. Swali linakuja, kwanini hawakumtaka na hawamtaki? Biblia inajibu. Ukisoma barua kwa WARUMI sura za 10, 11. utaona kwanini wayahudi hawamtaki Bwana Yesu. 10:2.. "wana juhudi kwaajili ya Mungu, lakini si ktk maarifa". Mungu aliwafanya wayahudi wamkatae Yesu ili neema ya wokovu ije kwetu mataifa (mataifa tofauti na Israel) tunasoma WARUMI 11:8 "....Mungu aliwapa (wayahudi) roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie hata SIKU HII YA LEO." Swali, 11:11 Je, (wayahudi) wamejikwaa hata waanguke kabisa? JIBU, 11:11 Hapana, lakini kwa kosa lao, wokovu umewafikia mataifa. Kwa maelezo hayo mtu mwenye ufahamu mzuri anatambua kwanini wanamkataa Yesu. Kwa nyongeza tena kidogo tumalizie. Mwisho wa mambo yote, Mungu atawafumbua macho wayahudi ili wampokee YESU KRISTO BWANA. Tunasoma, WARUMI 11:25...."kwa sehemu ugumu umewapata Israeli mpaka utimilifu wa mataifa uwasili. 11:26 hivyo Israel wote wataokoka. Mwisho. 11:28-32.