Israel: Muswada watinga bungeni ukisema kumtaja Yesu kuwa kosa la jinai. Waziri mkuu asema hawana mpango wa kuendelea nao

Israel: Muswada watinga bungeni ukisema kumtaja Yesu kuwa kosa la jinai. Waziri mkuu asema hawana mpango wa kuendelea nao

Hakika mkuu,
Waarabu na wazungu wameharibu sana fikra za mtu mweusi. Afadhali kwa jamii za watu wa 🇨🇳, Japan nk wao huu upuuzi hawautilii manani.
Ijumaa ni mwendo wa kutangaza vivutio vya utalii vya Saudi Arabia,Jumamosi na Jumapili ni zamu ya vivutio vya utalii vya Israel, Palestine, Jordan, Italy, Greek, Turkey, Macedonia tena kwa kutoa kiingilio kiitwacho sadaka!
Huu mfumo wa unyonyaji iko haja ya kuondokana nao. Kuna muda utafika watu watapeleka kokoto Saudi Arabia kwa gharana zao wenyewe kuanzia usafiri,malazi,baunsa na chakula.
 
Hao jamaa wanamuona Yesu kama nabii Tito tu.

BTW: Kumpuuza tu haitoshi hadi wamtungie na sheria juu?
 
Kwa wasomi wa Biblia hiyo habari siyo mpya. Toka mwanzo hawa jamaa hawakumtaka Yesu. Swali linakuja, kwanini hawakumtaka na hawamtaki? Biblia inajibu. Ukisoma barua kwa WARUMI sura za 10, 11. utaona kwanini wayahudi hawamtaki Bwana Yesu. 10:2.. "wana juhudi kwaajili ya Mungu, lakini si ktk maarifa". Mungu aliwafanya wayahudi wamkatae Yesu ili neema ya wokovu ije kwetu mataifa (mataifa tofauti na Israel) tunasoma WARUMI 11:8 "....Mungu aliwapa (wayahudi) roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie hata SIKU HII YA LEO." Swali, 11:11 Je, (wayahudi) wamejikwaa hata waanguke kabisa? JIBU, 11:11 Hapana, lakini kwa kosa lao, wokovu umewafikia mataifa. Kwa maelezo hayo mtu mwenye ufahamu mzuri anatambua kwanini wanamkataa Yesu. Kwa nyongeza tena kidogo tumalizie. Mwisho wa mambo yote, Mungu atawafumbua macho wayahudi ili wampokee YESU KRISTO BWANA. Tunasoma, WARUMI 11:25...."kwa sehemu ugumu umewapata Israeli mpaka utimilifu wa mataifa uwasili. 11:26 hivyo Israel wote wataokoka. Mwisho. 11:28-32.
 
Hii comment inaonyesha humjui kabisa Mungu ni nani?

"Na tumfanye mtu kwa mfano wetu" ..ungeelewa maana ya hii sentensi ungeelewa Mungu ni Nani na mtu Ni nani. 'Mtu' siyo binadamu ni mtu.

"Na tumfanye mtu kwa mfano wetu"
Yohana 5:37

Naye Baba aliyenituma amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote, wala sura yake hamkuiona.
 
Back
Top Bottom