Iran anaivua nguo US..
Trump ni rais flani ambaye vitendo vyake na maneno yake anataka uelewe kwamba ,
- US ndio taifa linaloweza kuamua chochote na wakati wowote wakitaka,
- ndio taifa lenye nguvu za jeshi kuliko taifa lolote,
- ndio taifa linapaswa kunyeyekewa na mataifa yooote duniani,
- US ikitaka chochote kutoka taifa lolote lazima ikipate hata kama ni kwa nguvu.
- US inaweza kuadhibu taifa lolote endapo ikitaka, muda na wakati wowote.
- Hakuna taifa linapaswa kuwa juu zaidi kiuchumi kuliko US.
- US ndio taifa linapaswa kutoa masharti kwa taifa lolote.
Kama kauli mbiu yake isemayo MAGA , Sasa kwa huu mgogoro unavyoendelea US inavuliwa nguo, Trump anaona yote anayotaka kuaminisha watu si kweli na hapo ndipo anajitutumua kuanza kuandika mipasho mitandaoni na kufanya press na waandishi. Alivyo mjinga anasema wanaofuata ni Cuba.