Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Acha ujinga kwanza huyo rubani kaanguka mkoa ambao ni mipakani huko kama km30 mpaka 50 tu kutoka mpakani?
Alafu kingine ni rahisi kwa marekani kumpata kwasababu anamawasiliano maalumu yanayo onesha alipo hivyo marekani walikuwa wanajua ni wapi alipo kuwa wanamtafuta labda changamoto ilikuwa ni kumfikia tu.
Wakati Iran wao walikuwa wana bahatishaa tu na ndio maana waliwaambia wananchi wa kawaida wasaidie kumtafuta lakini inavyo onekana aliangukia milimani mbali na makazi ya watu.
 
ITR upo sawa iyo Sehemu kaangukia lazima wao wametumia GPS kujua aliko!!.

Na wakishajua yupo wp jambo linakuwa ni dogo kumuokoa kwamaana wanagawanya vikosi viwili kimoja kinaenda kumtafuta eneo lengine mbali na Sehemu usika.!!!

Kuwazuga pande za mbali kikosi B kinaenda mchukua Sehemu usika.

Jamaa kimemsaidia kuangukia kwenye milima. kaweza kujificha.
 
Sidhani kama walikuwa na mawasiliano, inaonekana kabisa alipoteza mawasiliano alipoanguka maana zile ndege zisingepta chinichini vile kuwatafuta na isingechukua siku mbili wala vikosi vingi kiasi kile, ifikie hatua mkubali Iran ana operations na ujasusi mbovu
 
Mipaka sio kila Sehemu inakuwa na ulinzi mkubwa!!!

Hata iyo Marekani yenyewe ipo mipaka ipo wazi ndio mana Trump alitaka kujenga Ukuta mkubwa Kwenye baadhi ya Mipaka.

Mipaka ipo wazi Sehemu nyingi tu uwezi kudhibiti Mipaka yote labda intelligence kuwe na taarifa za uvamizi wowote kwenye eneo usika.

Lkn uyu rubani niwazi Iran inamtafuta wakiwa vipofu !!!

tofaut na USA wenye Askari wao wanatumia GPS kumsaka wanatafuta chip. Ya uyo rubani.
 
Iranian kwasasa mawasiliano ni shida wamezuiwa ndiomana kwakutumia GPS bado imewapa ugumu kumpata kwa wkt!!!!
 
Chopper 2 zilidunguliwa na pia walipoangukia ni maeneo ya mipakani. Embu chukulia wangeangukia walau Isfahan kingewakuta nini.
 
Wacha wajisifie Iranian upendaga sana mtu mwenye Sifa !!!

sio muda tutasikia story tofaut zitapigwa tena izo ndege!!!

Na Marubani watakamatwa tujipe muda tu!!!

Iranian ndio mwisho wa jeuri mwisho wa nyodo✍️
 
R Rubani ana umuhimu upi kuliko ndege iliyo tunguliwa!?
 
Hivi kwa akili yako unadhani kila sehemu ya nchi inakuwa na wanajeshi wapo wamekaa?
Huyo rubani kaanguka huko milimani mbali kabisa na makazi ya watu hivyo kumpaka bila siginal maarumu ni ngumu sana.
Hivi ulisha wahi kujiuliza Ukrain ilipo ivamia krusk ni kwa nini Urusi ilichukua zaidi ya wiki kujipanga ili kuvizuia vikosi vya ukraine visiendelee kusonga mbele?
Hivi umesha jiuliza hamas walipo ivamia Israel ni kwanini Israel ilichukua zaidi ya masaa 12 kuanza kujibu mapigo ya hamas?
Hivi nyinyi mnadhani vita ni rahisi kama kucheza sindimba eti?
 
Sasa nini cha ajabu? Ulitegemea raia wote wa USA wataunga mkono vita hii? Au wote wampende Trump? Tofauti ni kwamba hapo USA wasiokubalianq na Trump na vita yake wanaweza kuongea ila Iran wasiokubalianq na Ayatollah hawawezi kusema.
 
Hao Wamarekani wawe makini sana maana incident kama hizi zitajitokeza sana kama wakiendelea kusogeza ndege zao karibu na Iran
Ajabu ni kwamba ndege inapigwa inaanguka ndani ya Iran ila Marekani anaingia na kuchukua watu wake! Sasa hio nchi ina keshi kweli? Rubani wa ndege mlioipigia mnashindwa kumpata ila USA anatoka huko ndege zake anakuja kumchukua huyo rubani.
 
Hao wenzako Iran wamekiri kuwa sasa WANAANZA KUPATA CONTROL YA AIRSPACE baada ya kuimarisha kwa mifumo mipya. Maanake ni kweli USA na Israel walitawala anga la Iran ila nyie waajemi mlikuwa mnabisha. Na USA wamekiri ndege hizi zimepigwa ila zile zingine mlikuwa mnalazimisha kitu ambacho hakipo.
 
Ajabu ni kwamba ndege inapigwa inaanguka ndani ya Iran ila Marekani anaingia na kuchukua watu wake! Sasa hio nchi ina keshi kweli? Rubani wa ndege mlioipigia mnashindwa kumpata ila USA anatoka huko ndege zake anakuja kumchukua huyo rubani.
Sasa kama soko linaungua katikati ya mji na zimamoto ndio wanakimbizana kwenda mtoni kuchota maji na soko zima linateketea unapaita ujasiri wapi wa kusema nchi ya Iran Haina jeshi?

Sio eneo lote la nchi Lina coverage ya wanajeshi na pengine haikuwa kipaumbele chao kutumia wanajeshi ambao wako bize MAENEO mengine ya kimkakati kwenda kumsaka mtu mmoja ambae mwisho wa siku asinge saidia kuzuia marekani na Israel kushambulia Iran
 
Bora ungenyamaza TU
Kuliko huu utetezi unaonyesha Jeshi la Iran lilivyo uchi
 
Hii ni Ishara kwamba Jeshi la Iran halina chochote ni aibu tupu hii
 
Jeshi la Iran wanachoweza wao ni kuchamba tu! Hii proof tosha ground operation Iran inawezekana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…