Israel walikua nje ya Ardhi yao Kwa miaka 1878 , wakarudi mwaka 1948 Kwa azimio la UN, maajabu ni kua hawakupoteza chochote kuwahusu wao !!.

Israel walikua nje ya Ardhi yao Kwa miaka 1878 , wakarudi mwaka 1948 Kwa azimio la UN, maajabu ni kua hawakupoteza chochote kuwahusu wao !!.

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Watu wengi hawajui Historia ya hili Taifa la Mungu.

Israel ndio waliokabidhiwa Nchi ya Kanani , miaka zaidi ya 1800 kabla ya kurudi kwao Kanani mnamo mwaka 1948, walitawanyika katika mataifa mbalimbali kufuatia Uvamizi wa Rumi .

Uvamizi huo uliwafanya Waisrael kukimbilia uhamishoni, wapo waliokimbilia bara la Ulaya, wengine Marekan, wengine Urusi, Wengine Ethiopia n.k.

Ajabu la Mungu , waliporudi mwaka 1948, wakarudi vilevile kama walivyoondoka, walirudi wanajua kuongea Kiebrania ( kiyahudi), walirudi wanajua kuandika kiyahudi, walirudi wana Imani yao ileile ya kiyahudi, walirudi wakiendeleza misingi ya torati ileile.

Yaan karibu kuwaza kibinadamu, Kwa miaka 1878, wa Israel kwa mfano walikua Milion 20, Milion 2 watawanyike Nchin Urusi, Milion 5 watawanyike Ulaya , Milion 10 Marekan , n.k.

Kwenye hayo Mataifa, wanakumbana na Tamaduni Mpya, Lugha Mpya, aina ya Maisha mpya, na Dini mpya.

Zaidi ya yote zingatia, ni miaka 1878 yaan vizazi na vizazi na vizazi na vizazi.

Ajabu ni kua mwaka 1958, wanarudi wakiwa vilevile utadhan walikua hawaenda popote, kuanzia Tamaduni, Lugha, Imani, Mfumo wa Maisha n.k

Kibinadamu ni jambo gumu sana hilo, gumu mnoooooo .

Lakini kwakua Yupo MUNGU ,aliowapa Nchi yao, na kuwaahidi itakua Yao hata milele na milele, Hilo likafanikiwa.

BINAFSI NAUNGANA NA TRUMP, WAWATIMUE WAFILISTI KUTOKA NCHI YA KANANI, NCHI YA KANANI NI YA WAISRAEL , NA KAMA WAFILISTI WATAHITAJI KUSALIA KANANI, WASALIE KAMA WAHAMIAJI TU WASOKUA NA URITHI WOWOTE KANANI.

Sifa na Shukrani zilirudi Kwa Mungu wa Israel, Mungu wa kweli !!.
 
Hivi leo hii uwachukue Wandengereko, uwatawanye Ulaya ,hata Kwa miaka 50 tu, alafu Et uwaambie rudini Nchini kwenu Tanzania, wataweza kweli? Na warudi wakiwa na urithi wao uleule wa kuzaliwa kuanzia Imani, Tamaduni?.

Ni ngumu mno !!.
 
Mnataka ku iframe Israel kama taifa la Mungu lakini ni mbali na hicho, ushoga na porn pale ni harven kwao.

Imagine unashadadia mauaji ya binadamu wengine kwa kugezo cha Kupewa nchi miaka hiyo.
 
Mkitaka kuzungumzia uzuri wa ukristo mnatumia agano jipya, mkitaka kuhalalisha mauaji ya wapalestina mnatumia agano la kale.

Mbona hamsemi kana Yesu aliwakataa hawa watu na kuwaita watoto wa ahitani kutokana na matendo yao?
IMG_1672.png
 
Kama ni ardhi yao, kwanini walitaka kupelekwa Uganda?
 
Heheheee, eti taifa la mungu lipo jangwani pasipo na mvua wala rutuba. Pumbaavu S 24 ultra
 
Heheheee, eti taifa la mungu lipo jangwani pasipo na mvua wala rutuba. Pumbaavu S 24 ultra
Waandishi wa Biblia kwasababu zao waliamua kumjumlisha Jehovah kama Mungu muumbaji, wakati yeye alikua ni mtoto wa Adam tu, na alipoachiwa urithi akawa ni mtu mwenye nguvu za kiroho na akashinda vita vingi hadi waisrael wakawa wanamuita Bwana wa Majeshi.

Alipokufa wakamzika katika kaburi walilolijaza mawe makubwa na leo linajulikana kama mlima Sinai ili tuu kuweka kumbukumbu kwa vizazi juu ya huyo Mungu wao wa Israel, walimpa u mungu maana alikua na nguvu za majini kiasi alikua anawafanyia watu miujiza na akawa anaogopwa sana.

sasa wakristo wakalibeba hilo la Mungu wa Israel wakiamini ndio Mungu Muumbaji kumbe sio. Israel ni Taifa la Mungu wa Waisrael ambaye anajulikana kama Jehovah..! lakini sio ndio Mungu Muumba Vyote Mbinguni na Duniani.
 
Hivi leo hii uwachukue Wandengereko, uwatawanye Ulaya ,hata Kwa miaka 50 tu, alafu Et uwaambie rudini Nchini kwenu Tanzania, wataweza kweli? Na warudi wakiwa na urithi wao uleule wa kuzaliwa kuanzia Imani, Tamaduni?.

Ni ngumu mno !!.
Waafrika ni watu rahisi sana kupeteza utamaduni wao. Angalia waliopelekwa Marekani miaka mia tatu mpaka mia nne iliyopita. Pia kwenye suala la umiliki wa ardhi takatifu Waisrael wana umiliki juu ya kiitwacho West Bank ya siku hizi. Toka kwenye biblia haikuonyeshwa kokote kuwa ardhi ya watu wa Kanaani ila Gaza ilipo leo ilikua sio ya Waisrael toka zamani. Naweza kuwaunga mkono wakichukua Jerusalem, Hebron na bonde lote la mto Jordani. Ni lao kihaki ila Gaza sio ya kwao. Hawakupewa umiliki wa Gaza.
 
Mtoa post, naomba kwanza kusema kuwa mimi ni mkristo pure bila chenga.

Unajua israeli haiutambui ukristo kama dini yao ya asili? Unajua kule israel wakristo ni kama robo tu?

Unajua israel ya inatuona wakristo kama wendawazimu pale tunapokomaza mashingo kuiombea nchi isiyo tuhusu!

MUNGU wetu tunayemuabudu anasema na kutuagiza tusiue wala kutesa! Huyu Mungu wa israel wa tel aviv anayewapa mamlaka israel kuua na kutesa wapalestina ni mungu yupi?

MUNGU wetu wa mbinguni anatuagiza tusiondoe au kusogeza mpaka wa jirani yetu wala tusinyang'anye hata kipande cha ardhi cha jirani yetu, huyu mungu wa tel aviv ni yupi?

unajua MUNGU wetu anatuagiza tusimtenge mtu kwa imani yake maana wote tumekombolewa kwa neema zake na hatuko chini ya sheria, huyu mungu wa tel aviv ni yupi?

MPENDE JIRANI YAKO, MPENDE ADUI YAKO{ HAYA MANENO SI YA KWANGU NI YA MUNGU} Huyu wa tel aviv ni yupi?

Acheni kujipendekeza israel ya tel aviv, mtafuteni MUNGU wa kweli miyoni mwenu. HAWA ISRAEL WANA ENEO LAO JEHANUM/PARADISO.
 
Ukute mwamba akiombwa na muisrael fasta anakitoa. Enhe wameteuliwa na mungu kuwa Bora hao unakataaje kwa mfano....
 
Mnataka ku iframe Israel kama taifa la Mungu lakini ni mbali na hicho, ushoga na porn pale ni harven kwao.

Imagine unashadadia mauaji ya binadamu wengine kwa kugezo cha Kupewa nchi miaka hiyo.
Sio kweli mkuu
 
Mtoa post, naomba kwanza kusema kuwa mimi ni mkristo pure bila chenga.

Unajua israeli haiutambui ukristo kama dini yao ya asili? Unajua kule israel wakristo ni kama robo tu?

Unajua israel ya inatuona wakristo kama wendawazimu pale tunapokomaza mashingo kuiombea nchi isiyo tuhusu!

MUNGU wetu tunayemuabudu anasema na kutuagiza tusiue wala kutesa! Huyu Mungu wa israel wa tel aviv anayewapa mamlaka israel kuua na kutesa wapalestina ni mungu yupi?

MUNGU wetu wa mbinguni anatuagiza tusiondoe au kusogeza mpaka wa jirani yetu wala tusinyang'anye hata kipande cha ardhi cha jirani yetu, huyu mungu wa tel aviv ni yupi?

unajua MUNGU wetu anatuagiza tusimtenge mtu kwa imani yake maana wote tumekombolewa kwa neema zake na hatuko chini ya sheria, huyu mungu wa tel aviv ni yupi?

MPENDE JIRANI YAKO, MPENDE ADUI YAKO{ HAYA MANENO SI YA KWANGU NI YA MUNGU} Huyu wa tel aviv ni yupi?

Acheni kujipendekeza israel ya tel aviv, mtafuteni MUNGU wa kweli miyoni mwenu. HAWA ISRAEL WANA ENEO LAO JEHANUM/PARADISO.
Ni kweli, Israel ni Wayahudi, ukristo ni Kwa asilimia kiduchu.
 
Mnataka ku iframe Israel kama taifa la Mungu lakini ni mbali na hicho, ushoga na porn pale ni harven kwao.

Imagine unashadadia mauaji ya binadamu wengine kwa kugezo cha Kupewa nchi miaka hiyo.
Nani kakwambia kuwa karibu na Mungu ndiyo kigezo cha kutotenda dhambi?.
 
Back
Top Bottom