Israel wapo tayari kutatua tatizo la maji Tanzania



Yaani ma mamvua na maziwa tukasafishe maji ya bahari ! Gharama ni kubwa kuliko kujenga mabomba
 
Tutasaidiwa mpaka lini
Hahaha subiri mradi ukianza tu utawasikia CCM watabadilisha watasema SSH katoa PESA. Miradi yote tunaambiwa SSH katoa pesa, Hakuna mradi tunatumia pesa za wafadhili nchi hii.

Donor wanachangia bujeti, tunapewa misaada, tunakopa,Makampuni yanatoa gawio, sijui pesa zetu huwa zinaenda wapi.

Tunaambiwa TRA wamevunja rekodi ukusanyaji kodi kila mwezi, lakini deni la nchi la ndani na nje linaongezeka kila siku.

Naomba mnichague niwe rais.
 
Nchi yenye vichwa maji .

Una maziwa makuu matatu , hujayatumia bado unawaza kutumia Mabilioni ya Pesa kutumia Maji bahari??.

Wa Israel wanawafuata Wa Iran hapa Tanzania
Mkuu 'Carlos'; hilo la "maziwa matatu" tusiyo juwa jinsi ya kuyatumia ni moja.

Lakini jambo la kujiuliza na kuona kiasi cha ujinga/upumbavu tulio nao ni kutofikiria ni kiasi gani cha maji huwa hata hatushughuliki nayo kabisa. Hapo Jangwani wanapojenga daraja sasa kwa sababu ya usumbufu wa maji kila mwaka, kwa nini hata hatuwazii jinsi ya kuyahifadhi na kuyatumia maji hayo, badala ya kuyaachia tu na kwenda kuharibu mazingira?

Hayo ya Jangwani ni kiasi kidogo tu, ukitazama yanayo potea nchi nzima na kuharibu mazingira utashangaa.

Israel wao wanatazama tatizo la maji katika mazingira yao ya mahali walipo, kwa nini nasi tusitazame matatizo yetu kwa hapa hapa tulipo na kutafuta njia za kuyafumbua matatizo hayo kwa njia inayo stahiki?

Ujenzi wa mabwawa ya kuhifadhi maji linakuwa ni tatizo kubwa kwamba iwe rahisi kuchja maji ya bahari?
Kwanza mabwawa yatasaidia hata katika matumizi mengine ya maji, kama umwagiliaji, na kunyeshea mifugo, n.k..
 
Naomba mnichague niwe rais.😂 kuna mtu alitaka kuupewa kwa muda akaukataa.. Angepewa madelu sijui ingekuwaje
 
Desalination Ina gharama kubwa sana za kujenga na inahitaji nishati kubwa. Tanzania Bado Ina vyanzo vya kutosha sana vya maji matamu ni kujikita kwenye usambazaji tu
Huyo balozi bwege anaropoka tu
Nami naungana na wewe. Huyo Balozi atakuwa anafurahisha kikao tu na hakuna lolote lililo kwenye mpango wa utekelezaji.

Kuna mambo ya msingi zaidi ambayo tunahitaji msaada wa kujifunza toka kwa hao Israel ili nasi tuyafanye kwa ufanisi; lakini siyo kitu kama hiki kinacho semwa hapa.
 
Yaani walioko kwenye shida ya maji ndio wanakuja kutusaidia sisi wenye maji kupata maji, hivi vyanzo vyote vya maji tulivyo navyo, ni kweli viongozi tunaowachagu wameshindwa kutandaza maji kwa wananchi wake? wananunua ndege wanaopanda wao tu, siasa kila mahali, huku wanaimba Mama anaupiga mwingi, kule loliondo wananchi wanagombania maji na wanyama!!!
 
Naomba mnichague niwe rais.😂 kuna mtu alitaka kuupewa kwa muda akaukataa.. Angepewa madelu sijui ingekuwaje
Hahaha mimi angenipa nisinge vunga, ninge mrudishia baada ya mwezi.

Madelu akiupata mtakoma, anautafuta hata umakamu au U PM kwa nguvu, Ukikutana naye kwenye ngazi huku ofisini usishangae akakupa shikamoo.

Bahati mbaya tu sasa hivi CCM walisema form ni moja tu, ungekuta mawe nchi nzima yameshaandikwa MRN Rais.
 
Viongozi wetu Huwa hawaoni aibu wanapokuwa wanazungumza kusaidiwa na mtu ambaye Yuko vitani na ninyi mnavyanzo vya maji Kila sehemu?
 
Tutasaidiwa mpaka lini
Kwa kweli hii inaweza kuwa ni aibu. Yan tumesaidiwa tangu vyakula vyenye virutubishi, ujenzi wa vyoo na sasa eti hata maji ya kutawadhia? Dah! Mito na maziwa (Lakes) maji yake yanashida gani kutumia?
 
Tuanze kwanza kutumia maji yote ya mito inayoingia baharini, kusiwepo hata na tone la maji ya mto kuingia baharini kisha ndio tuwaze hayo
 
Haruhitaji hawa maharamia wabaguzi. Waende wakasaidie ndugu zao Palestina kwanza. Wanatuona mazwazwa. Maji yote kila mito na maziwa bado tunahitaji maji ya bahari kweli!!! Au ni kwa vile tunatawaliwa na chawa na machawa?
Sasa hayo maji yenu ya mito na maziwa mmetumiaje?kuna wanawake wananamiwa mkojo wa ng'ombe hapo Simiyu hawana maji yoka Uhuru. Unasema wabaguzi. Wangekuwa wabaguzi wangekupa ushauri huo wa msaada? Usipaniki dogo.hujiwezi unategemea misaada. Huna mbele wala nyuma....😂
 
Sijapanga kutumia maji ya bahari kwa sababu ni gharama kubwa.
Nimeainisha vyanzo na vyote tunavyo, kilichokosekana ni akili na maarifa ya kutumia hadi tunategemea misaada (ulemavu wa fikra).
Kilichokosekana ni Utashi wa kuamua kuthubutu kuanza kutumia tulichonacho.
 
Tatizo kuna wenye nafasi za maamuzi wasiotaka, wasiothubutu au kujiongeza.
 
Mashehe watasema si maji Halal
 
Wapalestina wa BUNJU hatunywi hayo maji ya mazayuni
 
Wapalestina wa BUNJU hatunywi hayo maji ya mazayuni
 
Safi kabisa,njooni mfyeke mijusi huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…