Ukisoma historia ya waisrael, ni waarabu wenye dini tofauti baina yao na waarabu wenzao ambao ni waislam nao wayahudi. Ila ukaingalia wengi wanaojiita waisrael kama akina Netanyahu, unagundua kuwa ni wazungu tu waliotoka huko kwao na kuja kujifanya wayahudi. Je ndiyo maana wazungu wenzao wanawapa umuhimu ili kuendelea kuwatisha, kuwaumiza, na kuwaibia waarabu hasa ikizingatiwa wana utarjiri wa mafuta?
anue uelewa. Umeleta hadithi takataka!
Tafuta elimu ili usiulize maswali yasiyo na mantiki.
Kwanza ufahamu kuwa waisrael hawajawahi kuwa waarabu. Waisrael ni descendants wa Israel, yaani Yakobo ambaye alikuwa mtoto wa Isaka. Watoto 12 wa Yakobo ndiyo waliotengeneza makabila kumi na mawili ya Israel.
Hapo mashariki ya kati, tangu kale wamekuwepo hao wayahudi, waarabu, waajemi, wafilisti, wayunani, n.k.
Ungekuwa unajishugulisha kutafuta elimu usingeliuliza hili swali.
Kwa ufupi ufahamu kuwa migration ya wayahudi toka Cannani kuelekea Ulaya ilianza tangu kupigwa Yudea kingdom, yaani karne ya pili kabla ya Kristo. Toka wakati huo, wakati wa Roman empire, Ottoman empire, mpaka wakati wa ukoloni wa muingereza, wayahudi waliendelea kuondoka eneo la Cannan, na kuelekea Ulaya. Baada ya vita kuu ya pili ya Dunia, wayahudi wengi walitoka Ulaya na kukimbilia Marekani.
Migration ya wayahudi kutoka Cannan na kwenda Ulaya na America, iliwapa nafasi waarabu kuyachukua na kuyamiliki maeneo karibia yote waliyokuwa wakimiliki wayahudi wa kale. Ufahamu kuwa Cannan ya kale, ambayo ndiyo lilikiwa Taifa la wayahudi lilijumuisha Israel ya leo, sehemu ya Jordan, Misri, Lebanon, Syria na Iraq.
Kitu ambacho kilichochea sana wayahudi waliokuwepo Ulaya kurudi kwenye ardhi ya Baba zao, ni uharamia wa Adolf Hitler aliyedhamiria kuwamaliza wayahudi wote, falsafa sawa na ya Ayatollah wa Iran lakini yenye sababu tofauti.