T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Iran hana instability yoyote ya maana ndani kwake. Hao wanamgambo wa Balochistan ni wa kawaida kama wa nchi nyingine, kinachowabeba wao ni kushambulia kigaidi-gaidi kama ambavyo Israel inateseka na wanamgambo wengine.Mimi sidhani kama Iran anaweza mshambulia Israel direct maana hapo itakua ni kuingia vitani ambapo kwa tension iliyopo nchini mwake Iran itakua ni risky move kwa sustainability ya utawala wake. Iran anahitaji amani sana nchini mwake kwa sasa. Labda anaweza shambulia tu maslahi ya Israel maeneo mengine duniani.
Alafu Iran ni mojawapo ya nchi chache zenye watu wafia nchi kupindukia, ukizingatia almost wote ni Washia. Na uzalendo wao hauna mambo ya sijui mimi siipendi serikali yani ukiwavamia wakapigwa propaganda nzuri haijalishi unakuja na nini mtatoana jasho. Kuna nchi zina watu wenye roho ngumu na Iran ipo.
Kwa jana nilivyoona hotuba ya Ayatollah na majenerali wake hasa mkuu wa vikosi vya makombora General Amir Hajizadeh hawaonyeshi confidence ya kuchukua hatua. Ayatollah aliongea kama rhetoric tu, ana utu uzima na busara kujua madhara makubwa yatakayotokea. Ila majenerali watakuwa tiyari ingawa wanasubiri kauli yake.
Kwa maoni yangu:
1. Wataalamu na washauri wa usalama wa Iran wanamshawisi Ayatollah asichukue hatua kubwa sana ili kuleta response kubwa kutoka Israel.
2. Majenerali na wanajeshi wa Iran wako tiyari kwa lolote, ni kawaida ya majenerali kukurupuka maana huzingatia vita tu sio siasa za vita hata uwafundishe namna gani. Kila jeshi huwa lina ile kujiamini sana na Iran they are very good kwenye hilo.
3. Ikitokea Iran ikatoa response ndogo ya kawaida, Israel inaweza funika kombe. Kuna ishara za kidiplomasia za "tufanye yaishe" kama ambavyo Iran ilipolipiza kisasi cha General Qasem Soleimani iliitaarifu Marekani wapi itashambulia na lini, Marekani ikajipanga alafu Iran ikarusha makombora kwenye rami na runway za base. Marekani ikashika lake, usalama wa wanajeshi wake uwanjani hakuna aliyekufa wala kujeruhiwa, Iran ikashika lake "ona tumelipiza kisasi" na raia wakashangilia.
4. Ikitokea Iran ikajibu vikali, Israel inajibu vikali maana kwenye masuala ya kusamehe itoe.
Tena kwa huo mtazamo wako ndio uko kinyume, siku ukiona Iran ina mkanganyiko wa ndani ujue ndio iko hatihati kuanzisha vita na jirani.