Unapoandika au kutoa hoja, write as sensible person. Unaweza kuwa a kitu cha maana lakini uwasilishaji ukawa wa hovyo kama ulivyofanya, kila kitu kitaonekana cha hovyo.
Ukweli ni kuwa katika hayo mataifa mawili, Israel na Iran, hakuna wa kumpigia magoti mwingine. Israel inaweza kufanya strategic strikes ndani ya Iran na kusababidha madhara makubwa kwa Iran, lakini siyo rahisi kuifanya Iran isalimu amri.
Iran inaweza kurusha makombora ndani ya Israel kama tulivyoshuhudia mwakajana na mwaka huu, ikaleta hasara ndogo kuliko inavyoweza kusababisha Israel ndani ya Iran, lakini bado Iran haina uwezo wa kuifanya Israel isalimu amri. Kitakachobakia ni kushambuliana tu.
Sababu ya serikali ya Lebanon kutotaka kusaidiwa na Iran au Hezbollah, unatakiwa ujue historia ya hayo makundi ya kigaidi ya Iran, na jinsi yalivyofaya dhidi ya Serikali ya Lebanon.
Setikali za Lebanon, Yemen, Saudia, UAE, Kuwait, Qatar, zote zinaiona Iran ni adui yao.
Mwaka 1979, Ayatollah alipopindua Serikali ya Iran, alitangaza kuwa wasuni siyo waislam, na washia wanatakiwa wahakikishe wanazipindua Serikali zote za ghuba ambazo zinaongozwa na wasuni.. Ayatollah ili kutekeleza huo uharamia wake, alitengeneza makundi ya washia ambayo sasa hivi yanaitwa makundi ya kigaidi, lengo kubwa ni kuwa makumdi haya yaziangushe Serikali zilizokuwa madarakani. Hezbollah kule Iran walimwua waziri mkuu wa wakati huo, Rafiq Hariri. Houthis kule Yemen walimwua Rais Ali Saleh.
Hivyo Serikali ya Lebanon ni wahanga wa makundi ya kigaidi ya Iran, ndiyo maana Lebanon haiwataki Wairan wala Hezbollah. Hata mafanikio ya Israel katika kuwaua viongozi wa kijeshi wa Hezbollah na wale Wairan wakiingia Lebanon, wanasaidiwa sana na wananchi na Serikali ya Lebanon, ambao Iran na Hezbollah, wote ni maadui dhidi ya wananchi wa Lebanon. Kinachoiumiza Lebanon ni mauaji ya wananchi wasio na hatia, kutokana na wapiganaji wa Hezbollah kujificha kwenye makundi ya raia.