Israel yaendelea kupiga kwa hasira Gaza. Maana yake nini

Inarushwaje mzee , idf iko ndani ya Gaza,wakirusha ina maana wanajitambulisha kwa idf tuko hapaaaa njooni mtuue, hawwezi, kufanya hivyo.
Hicho ndo nawasifu,wanatoa info kidogo huku wanatwangatwanga kilakitu.
Unashangaa mtu yuko shelter anazuiliwa kutoka mwisho.
Jamaa wanabonda shelter yote,
Hapo watoto ,wazee na wabibi wanapitiwa.
Na waliambiwa waondoke
 
Kosa lilikuwepo tangu enzi za kina Yoshua

Waliambiwa wawamalize kabisa hao wafilisti, hawakusikia!

Labda ndo wanataka wawamalize sasa???
Kwa hiyo mungu wako anahamasisha mauaji?
 
Baada ya kusita kidogo kwa ule moto wa mabomu mazito kwa wiki moja. Tangu jana usiku mabomu mazito ya kuporomosha majengo yamejirudia. Na si kaskazini peke yake bali mpaka kusini watu walikotakiwa waende kwa usalama wao.

Inajulikana hapo juzi Jeshi la Israel liliingia ndani ya Hospitali kuu ya Alshifa. Pamoja na kutangaza hapo awali kuwa Alshifa ndipo ilijpo command nodule ya Hamas. Maneno hayo yalirudiwa na Rais wa taifa kubwa duniani la Marekani, Joe Biden.

Madaktari ambao wengine wala si waislamu au wapalestina walisisitiza hakuna vitu hivyo. Hatimae Jeshi la IDF lililiingia ndani na hakuna kitu cha maana walichokiona. Kwa aibu wamehojiana na wagonjwa kuhusu habari za Hamas bila kujali majeraha waliyowasababishia.

Kurudia kwa mashambulio hayo na vipeperushi vya kuhofisha watu kuna maana nyingi. Kwanza ni kupata aibu kubwa ya kushindwa kuwapata Hamas na mateka kutoka mahospitali manne makubwa walizozivamia na kuzikalia.

Kwa upande mwengine kunaweza kuwa na maana ya kutaka kumaliza haraka uvamizi wake wa Gaza na kutangaza ushindi kabla mambo hayajazidi kuharibika kwa upande wao.

Washirika na waungaji mkono wa Israel kwa sasa wameonekana kuanza kuligeuka taifa hilo jeuri lisiliosikiliza ushauri wa hata marafiki zake wala kutekeleza azimio lolote la umoja wa mataifa.
Sasa hapo kuna aibu gani?Hiyo ni sehemu ya kumsaka adui.Inaletaje aibu?Au neno "aibu" siku hizi limebadilishwa maana?
 
maelezo yako ni kama umekubali Israel imeshindwa kinamna na huko mbele itashindwa kinmna nyengine.
Inatia huruma ukali wa makombora kutoka vifaa vya kisasa na sifa za kientelijensia kuwa sasa mnataka taarifa kutoka kwa wagonjwa na raia mitaani.
Unamaanisha wameshindwa vita?
 
Unamaanisha wameshindwa vita?
Wameshindwa kinamna.
Wale wanaopima kwa vifaru na kuuwa na kuporomosha majengo wanaona kama ameshinda
Wale wanaopima kwa malengo ya kivita yaliyoainishwa mwanzo mwa vita wanaona wameshindwa.
Wamenasa kwenye mtego.
 
Kwani malengo ya mwanzo yalikuwa ni nini
 
Washirika na waungaji mkono wa Israel kwa sasa wameonekana kuanza kuligeuka taifa hilo jeuri lisiliosikiliza ushauri wa hata marafiki zake wala kutekeleza azimio lolote la umoja wa mataifa.
Hamas wanasikiliza ushauri wa nani?
 
Navyoona kwa sasa Israel inatumia nguvu zote, kuhakikisha Hamas wanasalimisha mateka bila masharti, kitu ambacho Hamas imekikataa mpaka Israel itakapokapostisha mashambulizi, na itakapokubali kuwaachia Wafungwa wa Kipalestina walio katika magereza zao.
Sasa hapo ni nani atakayesalim Amri kwa mwingine?
 
Baada ya kusita kidogo kwa ule moto wa mabomu mazito kwa wiki moja. Tangu jana usiku mabomu mazito ya kuporomosha majengo yamejirudia. Na si kaskazini peke yake bali mpaka kusini watu walikotakiwa waende kwa usalama wao.

Inajulikana hapo juzi Jeshi la Israel liliingia ndani ya Hospitali kuu ya Alshifa. Pamoja na kutangaza hapo awali kuwa Alshifa ndipo ilijpo command nodule ya Hamas. Maneno hayo yalirudiwa na Rais wa taifa kubwa duniani la Marekani, Joe Biden.

Madaktari ambao wengine wala si waislamu au wapalestina walisisitiza hakuna vitu hivyo. Hatimae Jeshi la IDF lililiingia ndani na hakuna kitu cha maana walichokiona. Kwa aibu wamehojiana na wagonjwa kuhusu habari za Hamas bila kujali majeraha waliyowasababishia.

Kurudia kwa mashambulio hayo na vipeperushi vya kuhofisha watu kuna maana nyingi. Kwanza ni kupata aibu kubwa ya kushindwa kuwapata Hamas na mateka kutoka mahospitali manne makubwa walizozivamia na kuzikalia.

Kwa upande mwengine kunaweza kuwa na maana ya kutaka kumaliza haraka uvamizi wake wa Gaza na kutangaza ushindi kabla mambo hayajazidi kuharibika kwa upande wao.

Washirika na waungaji mkono wa Israel kwa sasa wameonekana kuanza kuligeuka taifa hilo jeuri lisiliosikiliza ushauri wa hata marafiki zake wala kutekeleza azimio lolote la umoja wa mataifa.
Kama bado wanaendelea kupiga, itakuwa ni hasira kwasababu bado wanashambuliwa na hao Hamas. Na pia bado hawajui mateka walipo.
 
Back
Top Bottom