Israel yafanya shambulio baya nchini Lebanon na kuua zaidi ya 50, huku zaidi ya 300 wakijeruhiwa

Hivi hakuna wa kuwapooza hao wayahudi wawasamehe hao waarabu?
Wapo wengi ila lakini ujue Myahudi katika hali iliyopo sasa, amechafukwa, amejaa hasira kali sana kwa hiyo wanasubiri kwanza Myahudi atoe usongo kwa Waarabu walau kidogo halafu ndipo waweze kuongea naye. Kwa sasa Myahudi hasikii la mwadhini wala la mchota maji. Ni kutembeza kipondo tuu.
 
Nimewaita mafala sababu Israel anauwa rai wao wanauwa askari, lakini sina wasi wasi nao kabisa Israel hawezi kuwashinda vita Hezbullah hata siku moja time will tell.

Wewe Israel lini alishinda vita wewe hio kupiga Lebanon sababu America kawapelekea maboom mengi wanadhani kupiga majumba ndio watashinda vita au kuwauwa raia.

Israel ni taifa linalo enda kinyume kabisa na sheria za dunia yote sababu imepandikizwa pale kwa manufaa ya Western.
 
Sasa shida nini waarabu wanashindwa kukafyeka haki ka nchi ka Israel au wanakaogopa maana Kila siku kanatoa dozi ya vilio Kwa wavaa kobazi🤣🤣🤣🤣
 
Hivi hakuna wa kuwapooza hao wayahudi wawasamehe hao waarabu?
Wapo wengi tuu, ila kwa sasa Myahudi amechafukwa sana na ana hasira kali mno na hao waarabu. Hao wenye nia ya kuwapooza wayahudi wanasubiri kidogo myahudi atoe usongo dhidi ya waarabu halafu akishapoa walau kidogo, ndipo waongee naye. Ila kwa sasa mh'! ni ngumu aisee.
 
Duh sasa si watauliwa sana kama makuku
Kuna mtu aliniambiaga kuituliza hasira ya muisraeli sio jambo dogo
 
Hezbollah wameitaka hii vita sana kwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara ndani ya Israel. Nchi husika hazikukemea uchokozi huu bali walipiga kimya, sasa Israel kajibu tunaanza kusema Israel anaua wanawake na watoto. Wewe ni vita gani unaijua ambayo wanawake na watoto hawakufa?
 
Hivi wewe unajua vita havina macho au wewe unaongea tu kwa sababu ya udini. Unajua wakati wa vita vya Tanzania na Uganda Tanzania ilidungua ndege zake mbili pale Musoma na kuua marubani.
 
1. Si kweli Hezbollah wanawalenga IDF tu bali hawana uwezo wa kuwafikia wananchi wa Israel. Nyumba zote za Israel zina mahandaki so wakati wa hatari king'ora kinalia wanaingia. Na leo wamehamishwa na serikali yao. Israel hawalengi raia ndio maana wanatangazia kabisa wahame. Lini Hamas au Hezbollah imewahi kuwatangazia Waisrael wahame kabla hawajashambulia?

2. Kama ambavyo Israel inapata msaada toka USA, Hezbollah wanapata toka Iran, Lebanon na washirika wengine. Ni kwamba wanazidiwa uwezo, maarifa na teknolojia. Wenzao wakati wanachimba madesa, wao wanasoma madrasa.
 
Hawa Hezbullah mafala sana, wao Israel wanau Raia, nyie mnapiga askari pigeni Raia wao pia uwaone kama atagusa tena Lebanon. Hata uislam unakuambia anaye kushambulia mshambulie vile vile.
Pole sana kwa kipigo bado hujasema
 
Bwege wewe kitu usicho kijua bora unyamaze kuliko kuketa uwongo, Mtume Muhammad alikataza watu kuvaa kazi kupita kifundo cha mguu. Hata alisema wanao vaa kanzu zinaburuza chini salaa zao hazikubaliki.
 
Israel hana mamlaka yoyote yale kwa Sheria ya kimataifa kuwaambia raia wa Nchi yoyote ile aondoke Nchini kwao.

Leo Kagame ama Museveni akiwaambia watu wa Mkoa wa Kagera waondoke halafu wa kapiga Kagera itakua wenye Tatizo NI Tanzania?
Wewe unajiongelesha tu ingekuwa we ungebakia ufe kizembe? kisa sheria za kimataifa zitakulinda hizo dhidi ya kipindo cha Israel?
 
Very true, nakubaliana na wewe kuwa waarabu hawajawahi kuwa na huruma na kiumbe yeyote aitwaye myahudi... Iguess hata kakijitabu kao kanakataa.. Ni mwiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…