Nyie leteni mchezo, kipindi USA anavamia Iraq tulikuwa tunaambiwa kuwa jeshi la USA limeisha na linapigwa sana, mara wanajeshi wamekimbia, lakini baada ya siku Sadam kapotea, baada ya muda jeshi la Iraq ilizidiwa vibaya sana, sasa Hamas wanaojificha ndani ya raia na kwenye mahandaki ndo washinde vita? Utashangaa Gaza inaondoka moja kwa moja, kama ingekuwa rahisi kihivyo basi milima ya Golan ingekuwa imesharudi kwa Syria, na West Jerusalem ingekuwa imesharudi Jordan, hakuna namna Hamas ashinde hiyo vita na kumuondoa myahudi, hata waranu waungane Israel hataki pale.