Uko sawa kabisa lakini ni hiyo mission ya kuhakikisha miundombinu yote yaharibiwa na itategemea na taarifa za kijasusi kutoka kwa makomandoo wa IDF.
Ila kiukweli hii operesheni ya sasa IDF na Israeli waliichukulia kuwa ni "Case Study" ya ile vita ya 2006 kwamba wapi walikosea na wapi pahitaji kujiongeza.
Lakini tukio la kuanza kuwavunja nguvu Hezbollah kwa kuauwa wale makamanda wao wakubwa laweza kuwa ni moja ya hatua kubwa katika kutaka kuumaliza mbuyu wa Axis of Resistance.
Ni miaka sita ilopita yaani mwaka 2018 kijana mdogo jasusi wa Israeli alikuja na ripoti ya maendeleo ya Hezbollah na akawajulisha wakubwa wake wa kazi kwamba surveillance kwa Hezbollah imegundua kuwa wameamua kutumia "pagers"na na zile radio ndogo za walkie talkies kwa ajili ya mawasiliano. Hivyo ikawa ni suala la matayarisho kwa kuingilia (intercepting uagizaji wa hizo pagers ambazo yakadiriwa Hezbollah waliagiza kama 3000 hivi).
Kilofuata hapo ni story ndefu lakini kukata kidogo tukasikia kumetokea milipuko, watu waulizana na "consignment" imeingiliwaje hakuna anaefahamu ila ni kazi ya miaka zaidi ya sita ya ujasusi na surveillance ya Israeli na upofu wa Hezbollah katika kugundua (infiltration).