Issa Haji Gavi Katibu wa Oganaizesheni wa CCM Iringa anaonekana akieleza kuwa kadi ya CCM ina uwezo wa kutoa pesa Benki.
Sikiliza mwenyewe kisha uweke maoni yako.
Your browser is not able to display this video.
---
Kadi za kielekroniki za CCM kutumika kama ATM
Iringa. Katibu wa Oganaizesheni wa CCM, Issa Haji Gavi amesema kadi za uanachama za chama hicho zitaweza kutumika kwa huduma nyingine ikiwamo kufanya miamala ya kifedha.
Amesema mbali na miamala ya fedha, kwa wanaotumia huduma za Bima ya Afya wataweza kuitumia kadi hiyo pamoja na wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Akizungumza katika kikao cha balozi shina namba saba, katika Kijiji cha Ilambilole, Jimbo la Isimani, Gavi amesema huduma hizo ndizo zilizosababisha kuchelewa kwa kadi hizo.
"Mabadiliko ya kimfumo ndiyo yamesababisha zichelewe, tulikuwa tunafanya mabadiliko ya kimfumo ili tupate kadi zenye sifa. Kuanzia mwezi wa nane kila mtu atakuwa na kadi," amesema Gavu.
Amewataka wanachama wa chama hicho kuendelea kuiunga mkono CCM kwa kuhakikisha inashinda chaguzi zote zijazo.
Awali baadhi ya wanachama walilalamika kukosa kazi za kielektroniki licha ya kujisajili.
"Kati ya wanachama wote wa shina letu 42, ni nane tu ndio wanazo kadi," amesema Helena Kiliwa, ambaye ni mkazi wa Kihorogota.
Awali, Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema alisema wanaendelea kusimamia na kuhakikisha yale yaliyoahidiwa yanatekelezwa.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara huko Iringa , kwenye ziara ya Chongolo , kiongozi wa ccm asiyefahamika jina lake , ameudanganya Umna hadharani kwa kusema uongo kuhusiana na kadi mpya za ccm za kielektroniki .
Mbele ya viongozi wastaafu akiwemo William Lukuvi , ambaye alionekana kuchekelea , kiongozi huyo muongo amesema kadi hiyo ya ccm itatumika kila mahali ikiwemo Benki na kwenye sekta ya afya , bila shaka kadi hii yaweza kuwa ni kadi ya miujiza .
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara huko Iringa , kwenye ziara ya Chongolo , kiongozi wa ccm asiyefahamika jina lake , ameudanganya Umna hadharani kwa kusemabuongo kuhusiana na kadi mpya za ccm za kielektroniki ...
Hujawahi kuona zile kadi za Simba za na Yanga za Benki ya posts?
Kadi ya Benki ni chip tuu ambayo Ina mawasiliano na akaunti yako ya Benki hivyo huo urembo wa nje taasisi inaweza ku I brand kwa rangi au nembo yake hivyo hilo linawezekana
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara huko Iringa , kwenye ziara ya Chongolo , kiongozi wa ccm asiyefahamika jina lake , ameudanganya Umna hadharani kwa kusemabuongo kuhusiana na kadi mpya za ccm za kielektroniki...