Isuzu Bighorn vs Suzuki Grand Escudo?

Mkuu magari ya ulaya ni aina gani ya magari unayapendekeza kwa mazingira ya kibongo.
 
Isuzu Bighorn engine zake ni very complex kumaintain hasa hii diesel 4JX1 motor

Hii engine ni commonrail lakini ni tofauti na commonrail za kawaida tunazozijua.

Utofauti upo kwenye high pressure pump na commonrail system kama ifuatavyo.

(1)4jx1 high pressure pump ina press oil kuingia
Kwenye kibuyu, (commonrail) badala ya diesel.
Inatumia hydraulic injector.

(2) ina oil filter mbili, primary na secondary.
( i) primary oil filter ni kwa ajili ya matumizi ya
Kawaida ya kulainisha na kupoza engine

( ii)Secondary oil filter ni kwa ajili ya hydraulic
injection system
kuanzia kwenye high pressure
pump mpaka kwenye hydraulic unit injector

Kuna baadhi ya matoleo ya hizi gari baadhi ya fault code unaweza kusoma kwenye dashboard bila kutumia mashine hasa bighorn ubs73 1998.
Dashbord ina display flashing code unakuwa unazihesabu.lakini lazima uwe na reference chat ya kutafsili hizo code kwa ukipata namba inakueleza ni faut ipi.

Kwa leo ni hayo machache mwenye kuongezea anaweza kujazia.
 
Asante. Ila humu wengi wetu hatujui hizo details zaidi ya kukanyaga mafuta tu
 
Asante. Ila humu wengi wetu hatujui hizo details zaidi ya kukanyaga mafuta tu
Ni muhimu kujua profile kama hizo wakati mwingine huwa zinasaidia, tabia za magari linaweza kukulaza polini kwa kitu kidogo sana.
Anakuja fundi anagusa tu gari inaondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…