IT, ICT, CS students wanaokimbia chuo ili kuwa mabillgates hapa Tanzania hawawi hivyo hata kwa mtaa tu, kwanini?

Kuona ni jambo moja na kitu kuwa kwenye uhalisia ni jambo la pili ingawa linategemea la kwanza simkatishi tamaa na wala asithubutu kukata tamaa kwa maana yeye ni mtu pekee anayeona maono yake swala analotakiwa kujiuliza ni utayari wake kiakili na kiuchumi sio aongozwe na hisia kipindi nipo chuo kuna muda moto unakuwa mkali hadi unatamani kuacha chuo ukafanye mambo mengine
Moto Unakuwa Mkali😂😂
 
Bongo tunadrop chuo kwa kukosa miundo mbinu ya kujiendeleza.

Elimu yetu baaaado sana basically tunafundishwa historia historia za wazungu na baadhi za waafrika.

Baaaado sana Tz kwenye tech. Ndio kwanza awamu ya sita ya uongozi huru wenzetu wapo awamu ya 42 (if im not mistaken).

Siku mamlaka yatarudishwa kwa wananchi ndipo ukombozi utaanzia hapo.

Kwenye ulimwengu wa tech. & science tutaendelea kua wakarabatiji. Mpaka atakapotokea raisi mwanatech. na mpenda tech huenda kuna kitu tutafanya.
 
Siyo familia tu, hata nchi tofauti.

Tanzania haina uchumi wa ku produce a Bill Gates in the true sense of a giant billionaire.

GDP ya Tanzania bado haijafikia net worth ya Bill Gates. Na hapo ni baada ya Bill Gates kugawa hela zake kibao katika charities.

Where are the angel venture capitalist?

Bill Gates Mama yake alifanya kazi IBM. Where is our IBM?

Sawa, labda tuchukue maana finyu ya "Bill Gates" kama tajiri aliyefanikiwa kwenye biashara ya ICT.

Tumekuwa na kina Ali Mufuruki alijaribu hii biashara. Mpaka anafariki alikuwa analalamika mifumo ya kodi ya serikali ilivyombana. Na huyu kafanya biashara ambayo vitu kama computer havilipiwi kodi.

Where is our Silicon Valley? Bill Gates hakujiinua yeye mwenyewe tu, kulikuwa na industry. Industry ambayo ilikuwa subsidized heavily na serikali, tena na jeshi, kwenye research and develooment.

Bajeti ya serikali kwenye research and development kwenye haya mambo ni kiasi gani kwa mwaka?

Hivi Tanzania tuna hata jarida formal (achana na forums) la kutoka kila mwezi la kupashana habari za ICT? Hata la online tu?
Bajeti ya serikali kwenye maendeleo na mambo ya maana ni ndogo mno kuliko hela iliyotengwa kwa "matumizi mengineo"!!!, hayo matumizi mengineo huwa hayaorodheshwi wala kuanishwa ni ya aina gani au ya nini?! Kama siyo upigaji ni nini?!
Lini wanaohusika wataacha huo uhuni na nafasi ya kupiga hela hatujuwi..
 
Yeye amepima akili ameona teknolojia itamtoa kuliko kuuza na kununua au kulima.Kwa muongo tuliopo teknolojia ndio inaweza kuleta urajiri wa haraka kuliko hata wachimba madini.Sasa huoni unamkatisha ramaa kuifikia fursa muhimu.
Tatizo input ya wabongo haithaminiwi, unaweza kuwa na idea nzuri ila hata price ya kuuza idea ikawa bei ya diamond karanga tu!

Kwa wenzetu support ni kubwa mno! Yani ukianzisha app yako tu ukaiuza kwenye soko la mitandao wanunuzi wapo na unatoka kimaisha full!

Yani kibongo bongo platform zingekuwa kama ulaya sahizi harmorapa angekuwa anamiliki mansion na ma rolls royce kwa hit single moja tu!
 
Kati ya washkaji sita walioacha chuo,watano Wana make more than 5 milion kwa mwezi ,last time I check wanaendelea vizuri nanplan zao zimekaa poa..tuliomaliza tupo kazini kilio Cha maslah
 
Siyo familia tu, hata nchi tofauti.

Tanzania haina uchumi wa ku produce a Bill Gates in the true sense of a giant billionaire.

GDP ya Tanzania bado haijafikia net worth ya Bill Gates. Na hapo ni baada ya Bill Gates kugawa hela zake kibao katika charities.

Where are the angel venture capitalist?

Bill Gates Mama yake alifanya kazi IBM. Where is our IBM?

Sawa, labda tuchukue maana finyu ya "Bill Gates" kama tajiri aliyefanikiwa kwenye biashara ya ICT.

Tumekuwa na kina Ali Mufuruki alijaribu hii biashara. Mpaka anafariki alikuwa analalamika mifumo ya kodi ya serikali ilivyombana. Na huyu kafanya biashara ambayo vitu kama computer havilipiwi kodi.

Where is our Silicon Valley? Bill Gates hakujiinua yeye mwenyewe tu, kulikuwa na industry. Industry ambayo ilikuwa subsidized heavily na serikali, tena na jeshi, kwenye research and develooment.

Bajeti ya serikali kwenye research and development kwenye haya mambo ni kiasi gani kwa mwaka?

Hivi Tanzania tuna hata jarida formal (achana na forums) la kutoka kila mwezi la kupashana habari za ICT? Hata la online tu?
Unaakili sana
 
Bill Gates alizaliwa kwenye familia ya mamilionaire msijifananishe.

It can also be an excuse...haina maana kila mtu afanye kazi anazifanya ili kufanikiwa. Kuna fursa nyingi ambazo haziangaliwi ila zina nafasi ya kutengeneza little millionaires. Ila sio wale wa Arusha. Mtu akimiliki nyumba sakina anakuwa millionaire. Njiro, ni bilionea
 
Hahaha Arusha bana inanifurahisha sana ila kuna ma billionaire kweli mkuuu huko
 
It can also be an excuse...haina maana kila mtu afanye kazi anazifanya ili kufanikiwa. Kuna fursa nyingi ambazo haziangaliwi ila zina nafasi ya kutengeneza little millionaires. Ila sio wale wa Arusha. Mtu akimiliki nyumba sakina anakuwa millionaire. Njiro, ni bilionea
Hiyo ndo reality, Gates sio tu alizaliwa kwenye familia ya mamilionaire lakini pia maza wake alikuwa kwenye board ya kampuni pamoja na CEO wa IBM na ndio aliyemuunganishia dili la Microsoft kutengeneza operating system kwa ajili ya computer za IBM.

Hizi stori za "self made" zinakuja kusukwa baadae, mimi na wewe hatuna opportunity za namna hiyo ni bora tubaki shule tu.

Pia kuacha Harvard hakukuwa na risk yoyote kwake, angechemsha na Microsoft angerudi tu Harvard baada ya miaka 2-3 whats the big deal? Jaribu bongo kama haujachekwa.
 
Bongo tunadanganyana lazima kila mtu awe na degree..na sasa mpaka PhD za kuungaunga. Wakati hata kusomea VETA kitu unachokipenda, unaweza kutoboa.
Elimu yetu inatuandaa tukaajiriwe na tunaamini katika ajira tutapiga deals
Bill Gates anastahili sifa...kumbuka, sio kila kwenye miti kuna wajenzi
 
Siyo familia tu, hata nchi tofauti.

Tanzania haina uchumi wa ku produce a Bill Gates in the true sense of a giant billionaire.

GDP ya Tanzania bado haijafikia net worth ya Bill Gates. Na hapo ni baada ya Bill Gates kugawa hela zake kibao katika charities.

Where are the angel venture capitalist?

Bill Gates Mama yake alifanya kazi IBM. Where is our IBM?

Sawa, labda tuchukue maana finyu ya "Bill Gates" kama tajiri aliyefanikiwa kwenye biashara ya ICT.

Tumekuwa na kina Ali Mufuruki alijaribu hii biashara. Mpaka anafariki alikuwa analalamika mifumo ya kodi ya serikali ilivyombana. Na huyu kafanya biashara ambayo vitu kama computer havilipiwi kodi.

Where is our Silicon Valley? Bill Gates hakujiinua yeye mwenyewe tu, kulikuwa na industry. Industry ambayo ilikuwa subsidized heavily na serikali, tena na jeshi, kwenye research and develooment.

Bajeti ya serikali kwenye research and development kwenye haya mambo ni kiasi gani kwa mwaka?

Hivi Tanzania tuna hata jarida formal (achana na forums) la kutoka kila mwezi la kupashana habari za ICT? Hata la online tu?
100% correct
 
Hata Tz unaweza toboa to that extent japo hautokuwa billgates, ila usitegemee msaada kutoka kwa serikali maana hamna atakaekusaidia

Kikubwa ubunifu na kuendelee kujifunza daily ile endless learning halafu kutoboa sio lazima u re invent the wheel unaweza anza na vitu simple mfano ku eliminate ma dalali wote Tz kwa kutumia software
 
Back
Top Bottom