Ndio maana kuna watu wengine kabla ya kuchangia hoja zao wanaulizwa alimu waliyonayo!
Ukisema Twitter ifungiwe, kesho pia Facebook, instagram na social platforms zitatumika, na mwisho zoote zitafungiwa! Hadi youtube na google!
Nadhani kunahaja ya kutambua wakati tulionao!
Tunahitaji
1. Inventions
2. Kujifunza vitu vipya kuendana na technologia
3. Kuwa sehemu ya dunia, na si kujitenga
4. Kukubali changamoto zilizoko sasa na kutafuta njia ya kuzitatua
5. Watawala waelewe kizazi cha sasa ni ngumu kukitofautisha na technologia, hapa ntatoa maelezo, leo hii wakifungia social media, watakapo fungua tutaikuta dunia iko wapi? Kiasi kwamba tutaanza kuisha maisha tuliyonayo leo mwaka 2040, na hapo dunia itakuwa imefikia wapi!
Mfano, kipindi wamefungia internet! Watu waliokuwa wana andika thesisi au disertation walipata shida sana! Research inahitaji kusoma mambo mengi sana, na sehemu kubwa ya mambo hayo yanalatikana kupitia internet, sasa jiulize, hawa watu kama ingeendelea hali ya kutokuwa na iñternet ingekuwaje?
Nadhani, sio sahihi kwa mtu wa rika ya miaka 50 kurudi nyuma, kuwa na akili hizi, haijengi!