Itanigharimu kiasi gani kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti?

Kwa gari binafsi umesema mafuta ya kuzunguka 300klm

Kilometer 300 ni nyingi sana,huo ni umbali mrefu sana mbona iwapo nitakuja kwa siku moja tu au mbili,wastani angalau nitembee 90kilometer per day
 
Mkuu samahani, urahisi wa kuingia hifadhini ni kutokea Arusha huku au mwanza? Au je wewe unawapokea wateja wako kutokea upande upi?
M nawapokea watu upande wa Ikoma gate iliyoko jirani na mji wa mgm ila kutokea mwanza nikarb maana ukitokea Arusha itakuradhimu kufk mpaka mjin mgm ndipo uludi Tena hifadhini mkuu maelezo zaid 0625818341
 
Kwa gari binafsi umesema mafuta ya kuzunguka 300klm

Kilometer 300 ni nyingi sana,huo ni umbali mrefu sana mbona iwapo nitakuja kwa siku moja tu au mbili,wastani angalau nitembee 90kilometer per day
Nikweli lakin inategemea na wanyama watakuwa umbali gan mkuu
 
Mkuu hongera sema wewe ni wa kampuni binafsi koz naona gharama ziko juu sana. Kwani hao Tanapa hawana guides? Au magari. Na kama hawana magari Ina maana mtu akienda bila gari la kuzungukia ndani wanakubali au wanakataa?
 
Mi naomba kuuliza kwa mfano nikienda mimi mwenyewe binafsi mfano kupanda mlima Kilimanjaro na nikafika nikaanza kuupanda bila kulipia chochote je ni kosa?
 
Mkuu kama sitaki kuzungushwa na gari, gharama zinakuaje? Kuna kitu kinaitwa walking safari, mtalii anatembezwa kwa mguu na tour guide, gharama zake zimekaaje hapo?
 
😂😂😂😂😂😂 aiseee ubahili huu mkuu unatakujaga uliwe tu na simba , kweli mbugani ukazunguke kwa miguu kweli ?
 
Familia ya baba, mama na watoto watatu wa umri wa miaka 9, 5 na 3 tukitaka tours ya kuanzia tarehe 24 hadi 30 ndani ya Hifadhi , minimum budget inaweza ikawa kiasi gani? Ushauri wako kuhusu kulala Lodge, Campsite au Hostel ni muhimu , kumbuka nahitaji minimum cost as much as possible
 
Ah bora Nile zangu bata
 
Million 30 mkuu

Nimesoma mimi

Nisiusishe na lolote mkuuu
 
Tanapa hawana guides, ikitokea ukaenda bila gari hautaruhusiwa kuzunguka hifadhini. Sanasana watakuunganisha na kampuni binafsi Ili upate gari. Gharama zinaweza kuwa kubwa zaidi kulinganisha na endapo utapanga safari mapema na kupat gari.
Karibu.

Mkuu hongera sema wewe ni wa kampuni binafsi koz naona gharama ziko juu sana. Kwani hao Tanapa hawana guides? Au magari. Na kama hawana magari Ina maana mtu akienda bila gari la kuzungukia ndani wanakubali au wanakataa?
 
Samahani Kwa kuchelewa kukujibu mkuu.
Kwa ufupi safari hii itakuwa ya 7 days na 6 nights. Kwa mtazamo wangu naona itakuwa vizuri kama ukilala lodges za bei nafuu. Kwa siku hizo sita ndani ya Serengeti pekee itapendeza kama ukilala kwenye lodges/hotel angalau tatu tofauti katika maeneo tofauti yaani siku mbili utalala Kaskazini mwa Serengeti mpakani mwa Tanzania na Kenya katika maeneo ya Kogatende. Siku mbili utalala katikati ya Serengeti yaani Seronera na Siku mbili za mwisho utalala Kusini Magharibi mwa HIFADHI karibu za Ziwa Victoria.

Chaguo lingine ambalo linaweza kupendeza ni kuunganisha safari Yako katika HIFADHI ya Ngorongoro yaani unakaa siku nne Serengeti na siku tatu Ngorongoro. Gharama hazitofautiani sana na endapo utatumia siku zote ndani ya Serengeti.
Gharama nimekutumia inbox. Karibu sana mkuu.
0625818341
 
Kwa gari binafsi umesema mafuta ya kuzunguka 300klm

Kilometer 300 ni nyingi sana,huo ni umbali mrefu sana mbona iwapo nitakuja kwa siku moja tu au mbili,wastani angalau nitembee 90kilometer per day
Mkuu 90km Kwa Serengeti ni chache sana. Kumbuka Ina ukubwa wa zaidi kilomita za mraba elfu 14. Eneo kubwa ni tambarare tu yenye nyasi ndefu na wanyama wachache. Hivyo basi Ili uifaidi vizuri inakubidi utembee eneo kubwa zaidi.
Karibu sana tukuhudumie msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya.
 
Ukipanda hii mashine kutoka Musoma kwenda Arusha kupitia Mugumu au kutoka Arusha kwenda Musoma kupitia Mugumu utalii utakuwa umemaliza. View attachment 2046152
Hii pia ni chaguo zuri Kwa wale wenye budget ndogo ambapo itakugharimu angalau shilingi elfu 45 ya nauli kutoka Arusha Hadi Mugumu, Musoma au Tarime kupitia Ngorongoro na Serengeti. Tatizo la kutumia njia hii ni kwamba utawaona wanyama wale tu walioko pembeni ya barabara. Kwa vivutio vingine vilivyo mbali na barabara ni vigumu kuviona.
Karibuni Serengeti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…