Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Wana Jf kwa jinsi tulivyo katika kipindi kigumu ambacho kimezua hofu kwa kila mtu ni wazi kuwa Waziri wa afya na naibu wake hawastahili kuwepo kwenye hii nafasi mpaka sasa.
Mwaka jana bila kupepesa macho Dk Faustine Ndugulile alieleza ukweli umma wa Watanzania kuwa kujifukisha hakuwezi kuua wadudu wa Covid 19, hii ni sababu hawa virus wakiingia kwa binadamu huingia moja kwa moja kwenye mfumo wa kupumua( mapafu) hivyo hata ukijifukiza ni ngumu kuwaua huko ndani ya mapafu.
Mwaka huu baada ya dalili kuwa hili janga limerudi Tanzania kwa namna nyingine,maana inadaiwa sasa hivi kirusi cha korona kimejibadili. Tumeshuhudia madaktari wawili ambao wanasimamia wizara ya afya wakisisitiza watu kujifukiza. Je hawa watu kwa nini hawakutoa ushauri wa kitaalamu unaozingatia taaluma yao kama Faustine Ndugulile?
Leo hii toka watoe demostrantion namna ya kujifukiza hali inaonekana kuwa mbaya. Maana vifo vya vigogo mpaka makabwela vinazidi kupamba moto. Na tatizo ni hilo la kukosa uwezo wa kupumua.
Karne ya ishirini na moja kuongozwa na wasomi ambao hawezi kusimamia taaluma yao na kumshauri rais namna ya kukabiliana na magonjwa kisayansi ni aibu kubwa. Mawaziri hawa wawili wasisubiri vifo vya watanzania iwe sababu ya wao kujiuzulu.