Itashangaza Dunia kama Waziri wa Afya na Naibu wake hawatafukuzwa kazi ya uwaziri

Itashangaza Dunia kama Waziri wa Afya na Naibu wake hawatafukuzwa kazi ya uwaziri

Only kama wangekua wamepita kihalali wangekua na confidance za kufanya hvyo.. washawekwa wanawaza matumbo yao... imewachapa kidogo tu na bunge wanaakhirisha.... mama Anna nae chenga tu eti misiba ipo mingi lkn haitoki hapa inatoka kwingine... yaaani wanatufanya sisi kama hata hatujafika stndard I... yaani akili zao sijui wamezifungia wapi... [emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
Ni kukosa akili tu. Kwani hata kama misiba ya Moshi mingi inatokea Dar es Salaam huko nako si Tanzania? Haimshtui kuwepo misiba mingi Dar au mpaka iwe ya Kilimanjaro tu ndo ataona ni tatizo?
 
Wanataka watanzania wafe kwa wingi ili WHO iwapatie pesa nyingi wapate kuzitumia kujenga SGR ambayo ujenzi wake unasuasua kutokana na ukata
Punguani usie na akili, avatar na na id name yako ni jibu tosha.
 
tulipokua tunakemea haya mambo ya kienyeji yanayofanywa na serikali katili ya CCM nyie mataga mlikua mnakenua kama father Christmas,
sasa leo mmepoteza wapendwa wenu kwa Covid-21 ndiyo akili zimekurudi.
Sahihi
 
Tusitegemee ushauri kutoka kwa Waziri na Naibu Waziri wa Afya kwenda kwa mkubwa wao.

Tusitegemee ushauri, mkakati na ujasiri wa kumshauri mkubwa.

Muda mwingi walikuwa wanazunguka kutafuta kiki kupitia vyombo vya habari.
Kuna wakati walisema Kaguta Museveni alikuwa na washauri zaidi ya mia,lakini badala ya wao kumshauri yeye ndiye alikuwa anawashauri.
Hali iko hivyo hapa.
 
Afe nani ili tushituke? Afe nani tushawishike kufunga shule na vyuo? Wafe kina nani ili daladala na mabasi mengine ya abiria yasijae hadi pomoni? Afe nani tuzuie mashabiki viwanjani na katika kumbi za starehe? Nani afe ili Waziri wa Afya atoke hadharani akiri hatari inayotukabili? Ukimya wetu pengine ni jawabu la kwamba tumepanga sote tufe! Eeee Mungu Baba Tuokoe.

By Manyerere Jackton


WA.jpg
 
Mzee, hata ufukuze nani, sio jambo rahisi kudhibiti huu Ugonjwa kutokana na nature yake kuwa unaambukiza kwa njia ya hewa.

Na pia lazima uelewe kuwa ugonjwa huu umetengenezwa na watu kwa manufaa yao binafsi na sio uzembe wa serikali wala mtu yeyote ila hao walioutengeneza wenyewe.

Jambo la busara hapa ni kila mtu kujifunza kuchukua hatua binafsi na sio kusubiri matamko.

Kufukuza mtu yeyote kwa ajili ya hili Jambo kwangu Mimi naona itakua ni sababu za kisiasa tu ila kiuhalisia hakuna jambo lolote litakalobadilika.
 
Corona inaua watu wenye kinga chache au dhaifu mi binafsi nineumwa na nimepona bila kutumia dawa yoyote tuache kudanganyana Corona ipo lakini sio kama tunavyoaminishwa.
 
Back
Top Bottom