Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuandika kuwa baadhi ya Wanafunzi wa Darasa la Saba katika shule ya Msingi Mitundu B katika Halmashauri ya Itigi DC wanasoma hadi usiku bila kula, hali inayoweza kuahiri afya na uelewa wao, ufafanuzi umetolewa.
Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Kasiga M Yassini amesema kulifanyika vikao vya Wazazi wa Wanafunzi wa darasa hilo wakakubaliana kuwe na michango ya chakula, kilichotokea watatu kati yao hawajaafiki kuhusu mchango huo na hawajatoa.
Pia soma ~ Baadhi ya Wanafunzi Darasa la 7 Shule ya Msingi Mitundu B, Singida wanasoma hadi usiku bila kula
Anasema “Kweli Wanafunzi wanahudhuria masomo ya ziada kama sehemu ya maandalizi ya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi. Utaratibu wa kutoa chakula kwa wanafunzi hao uliafikiwa kupitia vikao halali na vya ushirikiano kati ya wazazi na uongozi wa shule.
“Jumla ya Wazazi watatu pekee kati ya Wazazi wote wa Wanafunzi zaidi ya 100 ndiyo ambao bado hawajakamilisha michango yao ya chakula.
“Hata hivyo, uongozi wa shule na kamati ya wazazi walikubaliana kuwa kutochangia kwa wazazi hao watatu hakuwezi kuwa sababu ya kuwanyima chakula watoto wao au kuathiri mfumo mzima wa ulishaji. Hivyo basi, wanafunzi wote shuleni hapo wanapata chakula bila ubaguzi wowote, wakiwemo watoto wa wazazi hao watatu ambao bado hawajachangia.
Uongozi umesisitiza kuwa mradi wa chakula shuleni ni uendeshaji wa wazazi wenyewe kupitia kamati yao. Walimu kazi yao kuu ni kupokea chakula kutoka kwa kamati hiyo na kukigawa kwa wanafunzi wote.
Jukumu la kuwahimiza na kuwafuatilia wazazi watatu ambao hawajachangia liko chini ya Kamati ya Wazazi yenyewe na uongozi wa kijiji, na wala halihusishi kuwanyima watoto chakula wakiwa shuleni.”