Pre GE2025 Itigi: Tundu Lissu adai kila Mfanyabiashara alitoa Rushwa ya Tsh Bil 9 ili kupata kibali cha Kuagiza Sukari

Pre GE2025 Itigi: Tundu Lissu adai kila Mfanyabiashara alitoa Rushwa ya Tsh Bil 9 ili kupata kibali cha Kuagiza Sukari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watu watakuja humu kuulizia ushahidi. Yaani the charge of life style pekee haziwezi kuwapa majibu. Mke wa Bashe inasemekana anapokea pesa kwenye mabegi.

Kuna haja ya kuanza kuwafangia viongozi wetu LIFE STYLE AUDIT.
Inasemekana!!?..na mnataka muaminiwe kwa maneno ya kusemekana!?..anapokea hela kwenye mabegi,kila siku,toka kwa nani!?..ni pesa haramu!?..acheni unafikiri na uchakubimbi,haipendezi kwa mtu mwenye korodani na ndevu
 
Akizungumza mbele ya Maelfu ya wananchi huko Itigi, Tundu Lissu, huku akijiamini kupita kawaida, amesema kwamba, baada ya Rushwa hiyo Kabambe, Wafanyabiashara hao wakaruhusiwa kuongeza shilingi elfu 1 kwenye kila kilo na kuvuna hela haramu Bil 27 kwa kila mfanyabiashara, hela hizi zilitokana na kukamuliwa Watanzania ambao mara zote wanaitwa Wanyonge.

Lissu amedai kwamba Vibali hivyo vilitolewa kwa Marafiki na Jamaa zao wa Karibu katika mpango Muruwa wa Nifae leo nikufae kesho .

Kwa vile Sakata hili ndio kwanza limeanza basi Jitahidi sana kubaki hapa JF ili kujua Mnyororo wote wa Waliohusika, kuanzia Serikalini hadi kwenye Bodi ya Sukari.

Liwalo na Liwe

View attachment 3019630

=====

Pia soma:

- Luhaga Mpina na Tundu Lissu, msiishie kwenye sukari tu, bali chunguzeni na biashara ya kukopesha mitandaoni
Duuh basi hiyo biashara ina faida sana
 
hiyo ya kusadikika ndio watu wa Itigi hawataki kama waTz wengine wanavyompuuza hivi sasa 🐒

hiyo ingine ya laki5 ni upotoshaji na uongo wa wazi, ama ni kwa makusudi ama kwa kutokujua lakini ni useless 🐒

hapana fomu CCM ya gharama ya laki5, ya kuchukua ama kurudisha kamanda 🐒
Kwa hiyo wanampuuza hivi sasa kwani Zamani hawakumpuuza? Au unasemaje Chawa?
 
watu wa Itigi ni watu wa maana na wa muhimu sana,

walimpuuza jamaa wakati alijaribu kuzungumza kwa hisia sana, habari ya sukari, alipowasoma hata hawamtazami, ikabidi na kumlazimu abadili hoja kwa haraka sana, baada ya kustudy facial expressions na body languages za hadhira ya wana Itigi, kwamba sukari sio issue kwao....

vinginevyo angeendelea kuwaeleza vitu ambavyo si vya muhimu kwao, wangemuacha aongee pekeyake tu jukwaani 🐒
Mkuu 'Tlaa', una kazi ngumu mno. Na itaendelea kuwa ngumu kwelikweli kadri tunavyo elekea 2025.

Itabidi niwe macho zaidi na kufuatilia kwa karibu zaidi hali yako itakavyo kuwa ikibadilika, kama hutazimia kabla ya kipenga cha mwisho.
 
Akizungumza mbele ya Maelfu ya wananchi huko Itigi, Tundu Lissu, huku akijiamini kupita kawaida, amesema kwamba, baada ya Rushwa hiyo Kabambe, Wafanyabiashara hao wakaruhusiwa kuongeza shilingi elfu 1 kwenye kila kilo na kuvuna hela haramu Bil 27 kwa kila mfanyabiashara, hela hizi zilitokana na kukamuliwa Watanzania ambao mara zote wanaitwa Wanyonge.

Lissu amedai kwamba Vibali hivyo vilitolewa kwa Marafiki na Jamaa zao wa Karibu katika mpango Muruwa wa Nifae leo nikufae kesho .

Kwa vile Sakata hili ndio kwanza limeanza basi Jitahidi sana kubaki hapa JF ili kujua Mnyororo wote wa Waliohusika, kuanzia Serikalini hadi kwenye Bodi ya Sukari.

Liwalo na Liwe

View attachment 3019630

=====

Pia soma:

- Luhaga Mpina na Tundu Lissu, msiishie kwenye sukari tu, bali chunguzeni na biashara ya kukopesha mitandaoni
Hakuna jipya kama mlimchukua marehemu lowassa nazo hizi pia ni porojo kama za mwembe yanga!
 
Watu watakuja humu kuulizia ushahidi. Yaani the charge of life style pekee haziwezi kuwapa majibu. Mke wa Bashe inasemekana anapokea pesa kwenye mabegi.

Kuna haja ya kuanza kuwafangia viongozi wetu LIFE STYLE AUDIT.
Watakuja akina machawa Lucas mwashambwa kukanusha na kuzodoa lakini ukweli ni kwamba tunanunua sukari sh 6000 kwa kilo badala ya nei halisi ya sh 25000
Hi haijalishi ni ccm au ni cdm
 
Naona wasomali wengi mjini wamekuwa matajiri ghafla
Kumbe bashe kawatoa kwa vibali vya sukari
 
SISI WANA CCM KINDAKINDAKI TUKISIA HAYA TUNAVUNJIKA MOYO SANA..., NGUVU ZINATUISHIA, UKIZINGATIA HATA SIKUKUU WENGI WETU TUMESHINDWA KUISHEHEREKEA, MUNGU ANAWAONA!
Pole sana kama kweli we ni mzalendo mwenzangu
 
Hii nchi bila kunyonga hawa majizi, watanzania tutabaki masikini.
kuna wakati majizi haya magufuli aliyatia jambajamba yakaogopa, baada ya magufuli kuondoka yaliibuka upya kwa kasi ya ajabu yanaiba yakijua anaweza kutokea kiboko yao mwingine akawakatisha wizi wao. Uchaguzi mkuu unakuja kama kuna mgombea urais hana ubavu wa kuyakabili majizi asigombee aache wenye uwezo wa kuyakabili wagombee na hatimaye apatikane kiongozi wa kudhibiti rushwa na wizi kwa vitendo
 
Tukiamua tunaweza kuwarudisha, wanapataka sana Africa. Bora Mkoloni mweupe, kuliko Mkoloni mweusi.
mbona wapo wanatawala kwa style nyingine ya invisible wakiwa kwao huko nje, wanatawala kwa kutumia remote, wana wb, imf. Hawaji wenyewe physically tuwaone pale magogoni/chamwino. Tena wengine nao wanataka, akina china na arabuni, wakipata vibaraka wao inatosha kutawala wakiwa kwao
 
Rushwa kwenye vibali vya sukari si jambo geni. Limekuwa likijirudia kila mwaka. Kwa maelezo ya wajuzi kuna kipindi kila mwaka kunakuwa na uhaba wa sukari na hapo ndiyo biashara ya vibali hufanyika.
 
Akizungumza mbele ya Maelfu ya wananchi huko Itigi, Tundu Lissu, huku akijiamini kupita kawaida, amesema kwamba, baada ya Rushwa hiyo Kabambe, Wafanyabiashara hao wakaruhusiwa kuongeza shilingi elfu 1 kwenye kila kilo na kuvuna hela haramu Bil 27 kwa kila mfanyabiashara, hela hizi zilitokana na kukamuliwa Watanzania ambao mara zote wanaitwa Wanyonge.

Lissu amedai kwamba Vibali hivyo vilitolewa kwa Marafiki na Jamaa zao wa Karibu katika mpango Muruwa wa Nifae leo nikufae kesho .

Kwa vile Sakata hili ndio kwanza limeanza basi Jitahidi sana kubaki hapa JF ili kujua Mnyororo wote wa Waliohusika, kuanzia Serikalini hadi kwenye Bodi ya Sukari.

Liwalo na Liwe

View attachment 3019630

=====

Pia soma:

- Luhaga Mpina na Tundu Lissu, msiishie kwenye sukari tu, bali chunguzeni na biashara ya kukopesha mitandaoni
Si wanakula kwa urefu wa kamba zao
 
Back
Top Bottom