Setikali hii kwenye uongozi, wamejaa wala rushwa na wevi wakubwa.
Huyu Bashe, bila shaka ni mwovu mkubwa. Mradi wake wa kilimo, ambao Mama aliidhinisha mabilioni ya pesa nyingi kupindukia, hauna lolote zaidi ya wizi mkubwa kupindukia.
Rafiki yake, bwana Rashid, ndiyo mrija wa kupokelea pesa hiyo ya wizi. Tena anathubutu mpaka kutamka kuwa yeye hawezi kuacha kupewa tenda hizo za mradi wa kilimo kwa sababu kila akilipwa, lazima amkumbuke. Wizi unafanyika kwa kumpa tenda za kutengeneza fence za mashamba, kutengeneza kinachoitwa barabara kuzunguka mashamba, na kuandaa mashamba. Ndiyo ile ya kuandaa eka moja ya shamba kwa milioni 7.
Fikiria mtu kama Bitko, aliyekuwa akimiminiwa sifa na Mama. Yeye watu wake wa karibu walisema toka mwanzo kuwa mawaziri wote wa marehemu wataondolewa lakini yeye hataondolewa kwa sababu chochote anachokipata kwenye madini lazima kinamfikia mama. Na kweli, licha ya uchafu mwingi alioufanya kwenye madini, ikiwa ni pamoja na kuyapora maeneo yenye leseni za wawekezaji wa nje, na kuwagawia wanyarwanda wenzake, lakini mpaka leo yupo, na akatengenezewa hata nafasi ambayo haipo kwenywe katiba.
Bashe, kama hiyo rushwa na ufisadi mkubwa alioufanya kupitia sukari, pesa ilikuwa inamfikia mama, basi hana wasiwasi, si ajabu mkashangaa anateuliwa kuwa naibu waziri mkuu wa pili. Hii inatoa picha ya wazi kuwa mama anawatumia baadhi ya mawaziri kama mirija yake ya kumtengenezea yeye mabilioni ya pesa.
Mama hatufai, hatufai hata kidogo. Watanzania tuseme imetosha. Na akishaondolewa, ile sheria ya kuwalinda viongozi wasishtakiwe tuifute kwa kuwa ni batili, inaenda kinyume cha katiba inayosema kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria. Hawa wote itabidi wachunguzwe na wawajibike kwa uhalifu wao.