ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

Hawa wapo vizuri sana kwenye habari, naipenda taarifa habari yao na ile sijui inaitwa sound track
 
Mzee wa pasha pasha pashaaaa moootooooo 😄 kipindi cha watoto wetu hicho
We bado wa juzi enzi hizo kuna kina Eddie ndio presenter.

Kipindi cha watoto tu mnajaa nyomi kwenye mavaranda ya watu kuangalia ila kilikuwa hakiboi maana kuna kipindi kimoja hicho Eddie alifanyia airport kwa kusafiri hadi south Africa huku akiwaoji marubani sijasahau kile kipind hadi leo na ukubwa wangu huu..
 
Mbona wengi wazuri wamepita pale
Mtu kama millard ayo
Sauda simba kilumanga
Betty mkwasa nk..
Ni kweli ila kuna ile kitu tunaita voice quality Gondwe kawazidi wengi hasa akiwa anatangaza

Sauda na Betty walikuwa watangazaji wa kawaida sidhani hata kama wanamfikia Fatma Almasi Nyangasa hasa usahihi na shauku katika usomaji
 
Sasa si namzungumzia huyo huyo au kulikuwa na eddie mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…