ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

Sawa vizuri alizijua sana katuni yule jamaa
Aliupamba utoto wa wengi kwa Katuni kama Scooby Doo, Double Dragons ya Billy na pacha mwezie na The Shadow Master [emoji3] , Popeye and Son wazee wa Spinach [emoji3], halafu kulikua na the flintstones[emoji3][emoji3] wanakwambia Iyebedebedooooooooo

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli ila kuna ile kitu tunaita voice quality Gondwe kawazidi wengi hasa akiwa anatangaza

Sauda na Betty walikuwa watangazaji wa kawaida sidhani hata kama wanamfikia Fatma Almasi Nyangasa hasa usahihi na shauku katika usomaji
Sauda Simba alikua anatangaza Habari kwa lugha ya Kingereza saa 5 usiku usimchukulie poa, haikua jambo dogo wakati huo.

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Huo mwaka mzee alinunua tv,kipengele ikawa sauti,tukakomaa nayo mpk iliporekebishwa
Nakumbuka enzi hizo ndio mzee wangu alinunua tv, kativii kadogo kama nchi 14 hivi kanawekwa kwenye kikabati maalum cha matairi. Kikabati kinafungwa mlango na kufuli.. kikabati kinakaa chumbani kwake usiku ndio kinavutwa kuletwa sebuleni kuangalia.. lazima muwe mmeoga ndio muangalie.. mwendo wa sunset beach itv na days of our lives ctn... life was good then!!
 
Aliupamba utoto wa wengi kwa Katuni kama Scooby Doo, Double Dragons ya Billy na pacha mwezie na The Shadow Master
emoji3.png
, Popeye and Son wazee wa Spinach
emoji3.png
, halafu kulikua na the flintstones
emoji3.png
emoji3.png
wanakwambia Iyebedebedooooooooo

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
🤣🤣🤣 bila kusahau ile ya Ed, Edd and Eddy na John Bravo
 
Sauda Simba alikua anatangaza Habari kwa lugha ya Kingereza saa 5 usiku usimchukulie poa, haikua jambo dogo wakati huo.

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
Namkumbuka alikuwa mtangazaji mzuri
sana kwenye kiingereza kuliko yule mzee jina nimelisahau

Ila kweye voice quality bado hakumfikia Fatma Almasi Nyangasa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] bila kusahau ile ya Ed, Edd and Eddy na John Bravo
Naam Naam, Cartoons za Zamani zilikua Nzuri. Kuna moja Naitafuta jina lake mpaka leo Kulikua na mwamba mmoja ana pete wanaunganisha na wenzake nadhani zile pete zinawabadilisha wanakwenda ku save the community

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Kampuni ya IPP Limited mwaka 1994 inatambulisha chaneli ya Analog kwa jina ITV kupitia masafa ya mawimbi ya kawaida kipindi hiko.

Na kipindi hiko ndio mtaa mzima tumenunua TV ya PANASONIC TX iliyotoka 1993 sikumbuki model ikiwa ya rangi.

Kipindi hiko Tv inafunguliwa saa 8 au 10 sikumbuki ila inafungwa saa sita usiku.

Ndipo nilipo jua series kama:
*Family Matters
*Perfect Strangers
*fresh prince of bel air
*The V

Na matangazo kama :
*Revlon
*cocal cola

Kipindi hiko unaamka usiku kushuhudia ngumi za Mike Tyson.

Ila kuna dada mmoja ni kama mwarabu au muhindi fulani alikuwa ndo mtu wa kwanza ITV wanafungua ndo anaonekana sana. Hivi yupo wapi miaka 30 sasa.

Wenye kuijua ITV vizuri

[mention]pasco mayala [/mention] ni moja ya watu wenye kuijua ITV
Mimi naikumbuka Panasonic top dome, nilinunua laki tatu na sitini mwaka ' 93 nilikuwa naangalia KBC kenya, itv ilikuja baadae, na kupata itv ilibidi ufunge kitu kinaitwa crystal!

Sent from my SM-T285 using JamiiForums mobile app
 
Tuliozaliwa 1984 huu uzi hautuhusu japo kipind cha watoto Show niliwahi kwenda
Mimi hatupishani sana cha ajabu sikupenda vipindi vya watoto,nilikuwa napenda hiphop,kipindi cha Reggae ngoma za akina Justine kalikawe,Innocent Galinoma na kipindi fulani kilikuwa kinaitwa footballmundial mambo ya mpira.
 
Mwaka jana nimepita kitaa wazee walipopanga miaka hiyo,kuna mama akaniita wakati nipo barabarani ni rafiki yangu sana bibi yule,akaniita sebuleni,tunasalimiana kuna dada akamuuliza yule mama "bibi huyu kaka ndugu yetu??maana mara ya pili namuona na unamuita ndani, bibi akacheka akamwambia "huyu mtoto wa jirani yangu mama yake mlokole,alikua mdogooo anakuja kuangalia TV sebule hii hadi analala nambeba nampeleka kwao,kanisumbua sana mtoto huyu"hahha pumzika kwa amani mama omary nasikitika sijaenda kumzika...
 
Back
Top Bottom