Uchaguzi 2020 ITV leo hakuna taarifa ya mikutano ya Lissu?

MUSIGAJI

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2014
Posts
2,254
Reaction score
2,715
Wanabodi habari ya majukumu?

Nipo naangalia taarifa ya habari ya ITV naona leo hakuna taarifa ya mikutano ya Lissu. Je, leo Mh Lissu hakufanya mikutano?

ITV ni vizuri muwe mnatupa taarifa mapema siku ambazo hakuna taarifa za Lissu tusiwetunapoteza muda, angalau tuwe tunafanya mambo mengine.
 
Kituo cha ITV nini kimetokea leo ni siku ya tatu mfululizo kwenye taarifa yenu ya habari ya saa 2 usiku hamtangazi habari kuhusu mikutano ya kampeni ya mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo mhe. Tundu Antiphas Lissu.

Mara ya mwisho kurusha habari za kampeni za mgombea huyu ilikuwa ni mikutano yake aliyofanya mkoani Tanga kabla hajakwenda kisiwani Pemba.

Ila ITV mmekuwa mkiendelea kurusha habari za mikutano ya kampeni ya wagombea wengine wote isipokuwa mgombea huyu kupitia chadema. Nini kimetokea ITV?

Naomba kuwasilisha.
 
kituo cha ITV nini kimetokea leo ni siku ya tatu mfululizo kwenye taarifa yenu ya habari ya saa 2 usiku hamtangazi habari kuhusu mikutano ya kampeni ya mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo mhe. Tundu Antiphas Lissu...
Taafadhali ITV ni ninyi mlikuwa mmebaki angalau kutupatia taarifa za Lissu kwenye taarifa za habari.Nini kimewakumba?.
 
Kwani kabla ya taarifa habari si kuna Muhtasari, hukuangalia? huo ndio unatoaga in brief nini kitakachotangazwa, sasa unaposema hukuambiwa unamaanisha nini?
 
Mkuu wamerusha,ila wamerusha kuanzia saa 2:30,pi ameonyeshwa akizungumzia ule uwongo wa kuambiwa kuna kimbunga haruhusiwi kutua,

Labda tujiulize kwanini wanachelewa kurusha
 
Huwezi kuweka taarifa za msaliti.

Tukiwambaia Amsterdam anamharibia Lisu mnakataa
 
Mkuu hapa Kati walijitutumua kidogo ...Ila tangu Mwamba Sheikh Ponda aingie uwanjani ITV wame mute!
Mtumikie Kafiri update mradi wako?!
 
Wananchi nguvu ya umma ngoja tuwahabarishe waTanzania kuhusu kampeni za TunduLissu2020 leo 24/10/2020

24 October 2020
Songea mjini, Ruvuma
Tanzania

WATU WA SONGEA MAGUFULI NI MBAGUZI,MWIZI NA FISADI MSIMCHAGUE” TUNDU LISSU

 
ITV...kwa mikoa ya kanda ya ziwa wanakubalika Sana..na taarifa yao ya Habari inaangaliwa Sana..Ni Bora kituo kikawatendea haki watazamaji wake wote..wasioneshe kuegemea upande wowote..wasimame katikati..na watoe taarifa zao kwa weledi mkubwa kwani zinawafikia watu wengi sana..
Kikubwa watunze maadili yao ya kazi na wawe chachu ya kujenga umoja na amani ya nchi yetu bila ubaguzi..
 
Kwani bado huwa unaangalia


Sent from my Redmi Note 4 using JamiiForums mobile app
 
Kundi la CCM linaloisaidia Chadema ni kundi kubwa kwelikweli mpaka Magufuli ang'oke kwa udi na uvumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…