NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Nashauri laptops za wanafunzi ziwe LENOVO THINKPAD, nje ya hapo mwanafunzi awe ana uwezo wa kifedha, vitu kama matengenezo ama kununua laptops mpya visiwe stress kwake, wale watoto wa kishua wanaopewa pesa bila mawazo na walioajiriwa tayari wenye spare money
Linapokuja suala la wanafunzi kwenda vyuoni kuna maamuzi ya gharama kubwa huwa yanafanyika kuhusu kununua laptop ya kuwafikisha mpaka mwisho wa safari ya chuoni na hata maisha ya baada ya chuo.
Wanafunzi wengi vyuoni hupatwa na dilemna pale laptops zikianza kuzingua, mara laptop imeizngua keyboard, speaker, screen, n.k, na hapo ilikuwa inatunzwa fresh tu, wakifika huko kwa mafundi ni stress za ziada, tatizo kama keyboard tu fundi anaomba laki, hapa shughuli za laptop inabidi zisimame hata mwezi ama miezi hadi hio pesa itafutwe.
Kuna wale laptop zinakufa mother board kabisa, hawa ndio huwa nawaonea huruma, fundi nae unakuta anasema motherboard laki 4, inabidi laptop ifungiwe kabatini tu, hapo hadi laptop ije kununuliwa ni panapo majaliwa.
Kwanini wanafunzi vyuoni wapitie kero hizi wakati kuna solution yenye uwezekano mkubwa kuwafanya wasiumize vichwa kwenye masuala ya kuhangaishana na mafundi ama kununua kubadili laptops,
Well, me naona suluhisho liwe ni LENOVO THINKPADS, hizi ni laptops ngumu sana, ni kawaida kutumika hata miaka 6 bila kumjua fundi na hapo ni hizi za mtumba, kwa wachache wenye uwezo wa kununua zile mpya ngoma inagonga mzigo mpaka utaichoka mwenyewe labda uwe careless sana kwenye kutunza.
Pia suala la battery nazo huwa zina maisha marefu na overall ziko poa kwenye kutunza chaji.
Zimetengenezwa maalum kwajili ya kuwa durable.
Sidhani kama wanafunzi wetu wana haja ya kusumbuka na hizi hp, dell, n.k. ambazo zikitumika ni kawaida kukuta keyboard imefeli, touchpad imekufa, kidogo tu screen ina mstari, n.k.