Jack Pemba na jeuri ya fedha

Jack Pemba na jeuri ya fedha

Ushamba tu. Akina dangote na pesa zao wametulia...

Na Hapa Ndipo Ninapompenda Muwania Urais Kwa Chama Cha REPUBLICAN Donald Trump Kauli Zake Kuhusu WAAFRIKA. Huyu Jamaa Akiwa Rais Wa Marekani NITAFURAHI KUNAKOTUKUKA.
 
Wabongo bana mara dangote mara mo mara bill gates.....yeye kaamua kuonyesha gari zake hao akina mo sijui dangote hawahusiki hapa....btw kajitahidi magari karibu $500k si haba
Mkuu maisha hayaishii kwenye magari. Najua wewe ni mmoja wa wapenzi wa magari. Hata mimi napenda sana magari, lakini anachofanya ni ushamba wa Waafrika, wa kuzuzuka na vimali tulivyonavyo. Hata Wamarekani weusi wana tabia hiyo hiyo. Ameamua kupiga video (naamini ni yeye) na kuonesha watu, hivyo ni haki ya mtu kumsifia kama wewe au kumnanga kama wengi wafanyavyo. Ila huu ni ushamba wa kiafrika katika ubora wake.
BTW mbona hiyo parking haiendani na hayo magari!!!!
 
Mkuu maisha hayaishii kwenye magari. Najua wewe ni mmoja wa wapenzi wa magari. Hata mimi napenda sana magari, lakini anachofanya ni ushamba wa Waafrika, wa kuzuzuka na vimali tulivyonavyo. Hata Wamarekani weusi wana tabia hiyo hiyo. Ameamua kupiga video (naamini ni yeye) na kuonesha watu, hivyo ni haki ya mtu kumsifia kama wewe au kumnanga kama wengi wafanyavyo. Ila huu ni ushamba wa kiafrika katika ubora wake.
BTW mbona hiyo parking haiendani na hayo magari!!!!
Wapi nimesema maisha yanaishia kwenye magari? Nashangaa tu mtu kaonyesha magari yake wengine wanaanza kuwataja akina dangote sijui bill gates kwani yeye kasema ni tajiri kuliko bill gates? Wengi wanaoponda humu ndio wa kwanza utakuta wamepost nyumba zao au magari yao kwenye profile zao mitandaoni. Anyway watu wa jf wako perfect sio tunaowaona mitaani huko.
Naona mstari wako wa mwisho unataka parking yake iwe kama unavyotaka wewe.
 


Aliyekuwa mume wa super star aunty ezekiel, aitwaye Jack Pemba pesa imeonekana ikizidi kumtembelea baada ya hivi karibuni kuonekana nchini Uganda akifanya kufuru ya aina yake , ambapo alikuwa akiosha moja kati ya magari yake ya kifahari aina ya range rover kwa kutumia Mvinyo wa bei mbaya huku akitumia ma dolali kufuta gari lake hilo, hali iliyozua gumzo jijini Uganda na kuwaacha watu midomo wazi.



Mume wa msanii huyo inadaiwa anafanya biashara nchini Uganda ikiwemo ya kumiliki makampuni kadhaa ya magari pamoja na maduka mbali mbali nchini humo

Sawa mdau
 
Kweli mpiganaji hafi bali huzimia tu. .huyu mchizi angekuwa ana roho nyepesi kipindi kile alivyokatiwa mirija yake shavu akapewa kanali kipingu angekuwa mwingine angedata. .au alivyofanywa korongwee na kina msofe. ..hizi fujo kama huna mitkasi nazo hazitakiwi zikuume na kutolea mfano sijui dangote sijui dewji...huyu mtu haya ndo maisha kabla hata ya teknolojia kipindi hiko anajaza makaratasi kwenye wallet akiwa anasoma kinondoni muslim
Sasa hivi utasikia Le Mutuz anakwambia huyo ni long time friend
 
Huyu jamaa wakati anatoka Untie Ezekiel alimfanyia Untie birthday party akanunu maboksi ya shampeni kila alie alikwa akapewa chupa moja ya kw2enda kunywea nyumbani baada ya party, so sifa kazianza kitambo tu.
 
Hayo ndio majukumu ya watu weusi kwenye ulimwengu huu.

Nina imani Wazungu wanaotengeneza hizo Landrover wakiona video kama hizi wanafurahi weeeeee....alafu wanasema "black people are so funny".........kisha wanarudi maabara kuanza ku design model ya 2017, 18, 19,20........

Alafu kesho wanamuona Raisi wako anagonga hodi na bakuli kuuubwa..."saidia baba"
 
Nikifika hapo nakataa Mungu hayupo inakuwaje awabariki watu kama hawa halafu wengine awanyime
 
JAck-10.jpg

Jack Pemba akimwaga shampeni kwenye gari lake jipya.


Stori: Mwandishi Wetu, Risasi

Kampala, Uganda: Kufuru ya matumizi makubwa ya fedha inayofanywa na kijana mwenye uraia wa Tanzania, Jack Pemba nchini Uganda, imewaacha midomo wazi mamia ya wananchi wakati utajiri wake ukitikisa kila kona ya burudani.

JAck-1.jpg

Jack Pemba ambaye miaka michache iliyopita aliibua gumzo ya aina yake katika viota mbalimbali vya burudani Bongo, akiimbwa karibu na bendi zote za muziki wa dansi, aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ambaye kwa sasa amezaa na dansa wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Moses Iyobo ‘Moze’.

AFANYA BETHDEI YA MIL. 100

Mapema mwaka jana, Jack Pemba alifanya sherehe ‘bethidei’ ya kufuru wakati akisherekea kutimiza umri wa miaka 42, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Speke Resort Munyonyo iliyopo pembezoni mwa Ziwa Victoria, nje ya Mji Mkuu wa Uganda, Kampala.

JAck-8.jpg

Katika sherehe hizo, kiasi cha shilingi milioni 100 za Uganda ziliteketea, katika sherehe iliyohusisha wageni wapatao mia moja ambapo keki kubwa ilikatwa huku waalikwa wakiburudishwa laivu na bendi ya muziki.

JAck-9.jpg

Wakati akifika katika sherehe hiyo, Jack Pemba alitinga kwa usafiri maalum wa boti, akiwa ameambatana na wapambe kadhaa. Ilidaiwa kuwa baada ya pati hiyo, baadhi ya waalikwa walipelekwa katika Kisiwa cha Seychelles kujipongeza.

JAck-11.jpg

ENEO LA MAEGESHO LATISHA


Kwa mujibu wa picha za mnato na video zilizopatikana katika mitandao ambazo gazeti hili ‘linazishikilia’, Jack Pemba anasikika akiyataja magari yake ya bei mbaya, yaliyoegeshwa katika nyumba anayoishi, ambayo hata hivyo haijulikani kama ni Kampala au Munyonyo. Anayataja aina ya magari hayo kuwa ni pamoja na 4 Matic, Hammer H3, Aud, BMW X 6, Toyota Alphard na Range Rover Sport 2016.

JAck-6.jpg

MVINYO WA BEI MBAYA WAOSHEA RANGE ROVER


Katika kile kinachoonekana kama kulibariki gari lake jipya, Range Rover Sport 2016, katika video nyingine, Jack Pemba anaonekana akiliosha na mvinyo aina ya Johnnie Walker Black Label, unaotajwa kuwa ni miongoni mwa pombe zinazouzwa kwa bei ghali.

JAck-5.jpg

Range Rover yake mpya.


ALETA NYODO KWENYE TUZO

Mei mwaka jana, Jack Pemba alialikwa katika sherehe za utoaji tuzo zinazojulikana kama Abriyanz Fashion Awards zilizofanyika kwenye Ukumbi wa MTN Arena, Lugogo, MC wa shughuli hiyo, Roger Mugisha aliwatambulisha watu kuwa kulikuwa na mfanyabiashara mkubwa kutoka Tanzania ambaye anaitwa Jack Pemba.

Magari yake yakiwa yamepaki

Alipomtaja jina na kumtaka kusimama ili kuwapungia mikono waalikwa, Jack Pemba hakupunga, bali aliachia tabasamu na kutoa burungutu la fedha na kuzirusha hewani noti za Uganda ambazo zilianza kugombewa na watu wote waliokuwemo ukumbini. Inakadiriwa alirusha kama milioni saba hivi kwenye tukio hilo.

JAck-1-001.jpg

WAGANDA WAHOJI, HUYU NI NANI?


Baadhi ya wadau wa burudani wa Uganda wamekuwa wakihoji Jack Pemba anayeandikwa na vyombo vya habari nchini humo ni nani, ingawa wanafahamu kuwa kijana huyo ni Mtanzania. Wanashangazwa na mbwembwe zake kiasi kwamba anaonekana kuwafunika vijana wanaounda kundi linalojulikana kama Rich Gang, ambalo linamhusisha pia mume wa zamani wa mwandani wa Diamond Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Ivan Semwanga.

Akiwa Uganda, Jack Pemba anatajwa kuwa mtu anayependa sana kuvinjari na wasichana warembo na mara kadhaa, picha zake zimeonekana akiwa na mabinti tofautitofauti.

JAck-2-001.jpg
WANAOMJUA WANAVYOSEMA


Mtu mmoja aliyezungumza na gazeti hili, aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwendapole, alisema anamfahamu Jack kama kijana mpenda starehe na anayetaka uwepo wake kutambuliwa popote anapokuwa.

Mmoja wa viongozi wa bendi ya FM Academia, aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema staili ya maisha ya kijana huyo siyo nzuri, kwani uzoefu wake unamuonyesha wengi huishia pabaya.

“Jack Pemba ni mtu wetu, anawasaidia sana wanamuziki wetu na kwa kweli sijui kwa sasa yupo wapi, wengine wanasema yupo Sauz, wengine UK (Uingereza), lakini ninachokifahamu ni kwamba starehe nyingi zinapofua.”

TUJIKUMBUSHE KUHUSU JACK PEMBA

Jack Pemba ni kijana wa Kitanzania ambaye aliibuka na kupata umaarufu mkubwa mwishoni mwa miaka ya 2000, baada ya kuwasili akitokea Uingereza, inakosemekana ana mke mzungu na watoto.

Akiwa Bongo, Jack Pemba ambaye ni mkali kwa ‘totoz’ alitembea na Aunt Ezekiel, lakini wakaachana miezi michache baada ya kutoelewana.

Jack Pemba ni maarufu miongoni mwa wanamuziki, kwani ni mmoja kati ya mapedeshee wanaofahamika kwa kutunza kiasi kikubwa cha fedha jukwaani, huku akizawadiwa kwa kuimbwa kwenye nyimbo.
 
Huyu ivi ana hata nyumba yake kwa jina lake? wazazi wake wapo hai anawasaidia? anaonekana kama mwenye LAANA mambo yake anayo fanya...........
 
Hhahaaaaa kumbe yule jamaa ni kaka yake duuuh,huwa namshangaa sana anashinda sana segerea mwisho, anapenda sana vilemba na vimini
 
Back
Top Bottom