Jacob Zuma aliishi miaka 12 Zambia na Msumbiji, sasa anaunga mkono Xenophobia

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
18,875
Reaction score
29,427
Wakati wa kipindi chake kama Rais wa Afrika Kusini, Zuma alitumia waziwazi historia yake ya uhamishoni kulaani chuki dhidi ya wageni (xenophobia). Hata hivyo, msimamo wake wa sasa wa kisiasa unaunga mkono kampeni za chama cha MK dhidi ya wahamiaji unawakilisha mabadiliko makubwa na yenye maslahi binafsi ambayo yanapuuza mshikamano aliowahi kuutetea yeye mwenyewe.

Jacob Zuma alitoroka Afrika Kusini mnamo Desemba 1975 ili kukwepa kukamatwa na serikali ya kibaguzi. Alikaa zaidi ya muongo mmoja uhamishoni akiwa Swaziland, Msumbiji na Zambia. Alipokuwa Msumbiji, alihudumu kama mwakilishi mkuu wa chama cha ANC na kuwapokea maelfu ya vijana wa Afrika Kusini waliokuwa wakikimbia machafuko ya Soweto ya mwaka 1976.

Alipokuwa madarakani, Zuma alikuwa akiwakumbusha mara kwa mara Waafrika Kusini kuhusu ukarimu wa bara la Afrika wakati wa harakati za ukombozi. Katika hotuba yake kwa Bunge ya mwaka 2015 kuhusu ghasia za xenophobia, Zuma alisema waziwazi kwa Kiingereza na isiZulu: "Tulipokea msaada kutoka kwa nchi nyingi wakati wa mapambano yetu ya uhuru. Hawakutufukuza wala kutunyanyasa."

Katika jibu lake bungeni mwaka 2011, alilikumbusha taifa kwamba "Waafrika Kusini walikuwa wanufaika wa urafiki, mshikamano, na msaada kutoka kwa watu wa Afrika na duniani," akisema kuwa historia hii inapaswa kuongoza jinsi Afrika Kusini inavyowatendea raia wa kigeni.

Ninashangaa "usahaulifu" wa Zuma na kuona kuwa ni hatua inayo chochewa na maslahi ya kisiasa na kutafuta fursa. Chama cha MK cha Zuma kinatumia hasira ya wapiga kura kuhusu ukosefu wa ajira, umaskini, na miundombinu mibovu. Kwa kuhamishia lawama mbali na makosa ya kisiasa ya ndani na kuzielekeza kwa raia wa kigeni, Zuma anatumia mbinu ya kawaida ya wanasiasa

===========

MK Party President Jacob Zuma has questioned why South African women vendors can’t trade because foreigners “have taken that space”, asking “whose country is this?”

He added that while some call for “grace towards foreigners”, it should be foreigners showing grace when entering South Africa.

“We will be fooled by people who talk too much, saying we must have grace towards foreigners. Foreigners must have grace when entering South Africa.” — Jacob Zuma

Source: newslive_sa
 
View attachment 3613624

Wakati wa kipindi chake kama Rais wa Afrika Kusini, Zuma alitumia waziwazi historia yake ya uhamishoni kulaani chuki dhidi ya wageni (xenophobia). Hata hivyo, msimamo wake wa sasa wa kisiasa unaunga mkono kampeni za chama cha MK dhidi ya wahamiaji unawakilisha mabadiliko makubwa na yenye maslahi binafsi ambayo yanapuuza mshikamano aliowahi kuutetea yeye mwenyewe.

Jacob Zuma alitoroka Afrika Kusini mnamo Desemba 1975 ili kukwepa kukamatwa na serikali ya kibaguzi. Alikaa zaidi ya muongo mmoja uhamishoni akiwa Swaziland, Msumbiji na Zambia. Alipokuwa Msumbiji, alihudumu kama mwakilishi mkuu wa chama cha ANC na kuwapokea maelfu ya vijana wa Afrika Kusini waliokuwa wakikimbia machafuko ya Soweto ya mwaka 1976.

Alipokuwa madarakani, Zuma alikuwa akiwakumbusha mara kwa mara Waafrika Kusini kuhusu ukarimu wa bara la Afrika wakati wa harakati za ukombozi. Katika hotuba yake kwa Bunge ya mwaka 2015 kuhusu ghasia za xenophobia, Zuma alisema waziwazi kwa Kiingereza na isiZulu: "Tulipokea msaada kutoka kwa nchi nyingi wakati wa mapambano yetu ya uhuru. Hawakutufukuza wala kutunyanyasa."

Katika jibu lake bungeni mwaka 2011, alilikumbusha taifa kwamba "Waafrika Kusini walikuwa wanufaika wa urafiki, mshikamano, na msaada kutoka kwa watu wa Afrika na duniani," akisema kuwa historia hii inapaswa kuongoza jinsi Afrika Kusini inavyowatendea raia wa kigeni.
Ninashangaa "usahaulifu" wa Zuma na kuona kuwa ni hatua inayo chochewa na maslahi ya kisiasa na kutafuta fursa. Chama cha MK cha Zuma kinatumia hasira ya wapiga kura kuhusu ukosefu wa ajira, umaskini, na miundombinu mibovu. Kwa kuhamishia lawama mbali na makosa ya kisiasa ya ndani na kuzielekeza kwa raia wa kigeni, Zuma anatumia mbinu ya kawaida ya wanasiasa
I think,
Africans should take that as an opportunity to address their issues at their home countries and rebuild their home countries, instead of blaming South Africans, who are united in defending their country against non South Africans 🐒
 
Hakuna cha kufix their own countries bali kilichopo ni siasa kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Nov 4, 2026.

Kufix problems walipaswa kuimarisha mifumo yao ya kisheria na kiutekelezaji (legal and enforcement) dhidi ya wahamiaji haramu (undocumented immigrants)
 
Memory loss ya kisiasa ni ugonjwa mbaya sana kuliko xenophobia yenyewe.
Wala Jacob Zuma hajapoteza memory bali "amesaliti" imani yake dhidi ya pan africanism na fadhila alizopata kwenye nchi ambazo ziliwahifadhi kwenye miaka hiyo. Na anafanya hivi makusudi ili chama chake kipate kura nyingi kutoka kwa voters
 
I think,
Africans should take that as an opportunity to address their issues at their home countries and rebuild their home countries, instead of blaming South Africans, who are united in defending their country against non South Africans 🐒
Absolutely,
Just like Zanzibaris and Tanganyikans are doing now
 
Madai ya Wasouth ni sahihi kabisa ila njia wanayotumia ni kipumbavu, wao walitakiwa wapambane na ANC waiondoe madarakani waweke chama kinachoweza kusimamia mipaka ya nchi vizuri.
 
Kwa sababu ya mfumo mbovu, dhaifu na corrupt unaoruhusu wageni ku take advantage overe wazawa.
Mbona hata Ulaya magharibi nzima (Italy, France, UK, Germany nk) nao wanalalamika na undocumented immigrants. Lakini Ulaya wana handle undocumented immigrants kiutaratibu

Nchi zisizo na undocumented immigrants kwa Ulaya labda Poland, Albania, Hungary.

Hili ni tatizo la dunia
 
Absolutely,
Just like Zanzibaris and Tanganyikans are doing now
vibaraka na mamluki wa mabwenyenye ya magharibi Tanzania, watashughulikiwa na wananchi wapiga kura wazalendo kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa2029 na uchaguzi mkuu 2030

inaweza kua ni kukataliwa kwa fedheha sana aise kwenye sanduku la kura 🐒
 
Nonsense,
Wacha kurukaruka kama maharagwe jikoni, jikite kwenye mada mezani
 
Mambo ya Xenophobia yameanzia Kwazulu Natal na kiongozi yeyote anaunga hilo jambo anaonekana ni mzalendo ndio maana wamemtumia Zuma ili aunge harakati zao ila kasahau yeye na ndugu zake walitumia Passport za Nchi nyingine ili kuweza kusafiri..
Jacob Zuma ametenda dhambi itakayokitafuna hadi kizazi chake cha 20 miaka ijayo. Of all the people yeye angekaa kimya. Yaani ameishi Moza, Zambia na Swaziland, huku nchi zingine zikiwasaidia kupambana na kaburu.

Kisha akapata Urais wa SA, na worse enough akiwa Rais yeye akawa fisadi baada ya kuwa mfukoni mwa Guptas family hivyo kuwa alama yabkuvuruga uchumi wa nchi.
 
Back
Top Bottom