View attachment 3613624
Wakati wa kipindi chake kama Rais wa Afrika Kusini, Zuma alitumia waziwazi historia yake ya uhamishoni kulaani chuki dhidi ya wageni (xenophobia). Hata hivyo, msimamo wake wa sasa wa kisiasa unaunga mkono kampeni za chama cha MK dhidi ya wahamiaji unawakilisha mabadiliko makubwa na yenye maslahi binafsi ambayo yanapuuza mshikamano aliowahi kuutetea yeye mwenyewe.
Jacob Zuma alitoroka Afrika Kusini mnamo Desemba 1975 ili kukwepa kukamatwa na serikali ya kibaguzi. Alikaa zaidi ya muongo mmoja uhamishoni akiwa Swaziland, Msumbiji na Zambia. Alipokuwa Msumbiji, alihudumu kama mwakilishi mkuu wa chama cha ANC na kuwapokea maelfu ya vijana wa Afrika Kusini waliokuwa wakikimbia machafuko ya Soweto ya mwaka 1976.
Alipokuwa madarakani, Zuma alikuwa akiwakumbusha mara kwa mara Waafrika Kusini kuhusu ukarimu wa bara la Afrika wakati wa harakati za ukombozi. Katika hotuba yake kwa Bunge ya mwaka 2015 kuhusu ghasia za xenophobia, Zuma alisema waziwazi kwa Kiingereza na isiZulu:
"Tulipokea msaada kutoka kwa nchi nyingi wakati wa mapambano yetu ya uhuru. Hawakutufukuza wala kutunyanyasa."
Katika jibu lake bungeni mwaka 2011, alilikumbusha taifa kwamba
"Waafrika Kusini walikuwa wanufaika wa urafiki, mshikamano, na msaada kutoka kwa watu wa Afrika na duniani," akisema kuwa historia hii inapaswa kuongoza jinsi Afrika Kusini inavyowatendea raia wa kigeni.
Ninashangaa "usahaulifu" wa Zuma na kuona kuwa ni hatua inayo chochewa na maslahi ya kisiasa na kutafuta fursa. Chama cha MK cha Zuma kinatumia hasira ya wapiga kura kuhusu ukosefu wa ajira, umaskini, na miundombinu mibovu. Kwa kuhamishia lawama mbali na makosa ya kisiasa ya ndani na kuzielekeza kwa raia wa kigeni, Zuma anatumia mbinu ya kawaida ya wanasiasa