Jacob Zuma aliishi miaka 12 Zambia na Msumbiji, sasa anaunga mkono Xenophobia

Ulaya raia hawasambulii na kuua wahamiaji, wanazitoa serikali zao madarakani na kubadilisha na nyingine wanazofikiri zitafanya kazi nzuri zaidi. Sasa ujinga wa huko South wanapiga kelele kuhusu Uhamiaji ila kila uchaguzi wanairudisha ANC madarakani.
 
Madai ya Wasouth ni sahihi kabisa ila njia wanayotumia ni kipumbavu, wao walitakiwa wapambane na ANC waiondoe madarakani waweke chama kinachoweza kusimamia mipaka ya nchi vizuri.
Mkuu Yoda hapo umeingia kwenye epicenter ya tatizo. Inastahili unywe mirinda nyeusi na mtori, nitalipa
 
Kwa mwanasiasa yeyote, ni vigumu sana kusimama jukwaani na kukiri kuwa "Chama changu cha zamani (ANC) kimefeli kwa miaka 30." Ni rahisi zaidi kusema "Matatizo yenu yanasababishwa na wageni wanaochukua ajira na rasilimali zenu." maana ndio namna pekee ya kukwepa uwajibikaji
 

Walioenda uhamishoni (into exile) hawakuzidi 50,000 huku mamilioni walibaki nyumbani wakifanya maandamano yasiyo na kikomo ndani ya South Africa kupinga utawala wa kibaguzi


Waliokimbia kwenda nje hata Julius Nyerere aliwastukia watu kama Jacob Zuma n.k waliokuwa viongozi uhamishoni kuwa ni matapeli, viongozi wengine uhamishoni walikuwa informers (wapelelezi) wa makaburu na kuwa hawakuwa serious kutaka mabadiliko. Viongozi na vyama vyao vya kitapeli vyafukuzwa Tanzania, Zambia n.k miaka hiyo ya mapambano ya kuondoa utawala wa kikaburu

Soma uzi huu wa historia ya mapambano ya kuondoa utawala wa kibaguzi na matapeli ya kisiasa yaliyojisimika uongozi kutumia wakimbizi hao 50,000 walikuwa uhamishoni kujinufaisha kwa hela za misaada bila fedha hizo kufika ktk kambi za wakimbizi hao 50,000 waliotapakaa nchi za kusini mwa Afrika.

Na matapeli haya ya kisiasa yaliporejea nchini Afrika ya Kusini 1992 yakaanza kujimegea minyama na kujipendelea vyeo serikalini, jeshini, polisi kujinufaisha , ufisadi wa kutisha wa serikali ya ANC kama Nyerere alivyohisi utapeli kiasi tunaona miaka hii ya 2000 nchi ya Africa ya Kusini uchumi umeporomoka, huduma za kijamii kama shule, afya na mabarabara kujaa mashimo huku magenge ya madawa ya kulevya kuwa na nguvu kwa ushirikiano na matapeli ya ukombozi wanaojibainisha walijioa mhanga kwenda nje kupigania ukombozi
:

 
Upo wapi huko ambako hakuna hao watu mkuu migodi yenu na mbuga zenu wamejaa watu gani sio kutembea kumiliki..
Kwenye nchi kuna kazi zinapaswa kufanywa na wageni na kazi ambazo sura za wageni hazitakiwi kuonekana kabisa isipokuwa kwa sababu maalumu sana kama asylum au ndoa. Ni upumbavu mchina anakuja nchi ya Africa aje kuuza duka la rejareja mtaani au kuchezesha madubwi ya kamari vijijini.

Hao wageni unaowaona kwenye migodi, mbuga za wanyama, bandari, SGR na rasilimali nyingine wanaitwa wawekezaji na experts. Kama ni ukweli ni wawekezaji halisi au wawekezaji uchwara na kama bado tunawahutaji kwenye hizo sekta zote kwa kiwango hicho huo ni mjadala mwingine kabisa.
 
Mmeharibu nchi ya watu kwa kuwapeleka bangi na madawa ya kulevya, Kazi kukaba watu na kuwapora Mali zao. Rudini tuje tubanane hapa bongo yapo mapori mengi ya kulima ilasomu wa kulima ni mara Moja kwa mwaka ,ujifunze kuweka akiba hadi msomu mwingine
 
Wala Jacob Zuma hajapoteza memory bali "amesaliti" imani yake dhidi ya pan africanism na fadhila alizopata kwenye nchi ambazo ziliwahifadhi kwenye miaka hiyo. Na anafanya hivi makusudi ili chama chake kipate kura nyingi kutoka kwa voters
Zuma alisema hawezi kukaa ANC kwa sababu ingekuwa ni usaliti lakini yeye mwenyewe alikuwa mwanachama wa ANC kwa miaka zaidi ya 45 ,chama kilichomfanya kuwa rais mara mbili.

Huu uaminifu wake mpya ni kwa ajili ya chama alichokizindua kwa manufaa yake mwenyewe wala siyo kwa ajili wananchi.
 
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amewahi kuishi Tanzania. Alikaa na kufanya kazi nchini katika miaka ya 1980 akiwa uhamishoni kama kiongozi wa tawi la kijeshi na kitengo cha ujasusi (Umkhonto we Sizwe) cha chama cha African National Congress (ANC) wakati wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi.
 
ANC, MK Party, CCM, FRELIMO, MPLA matapeli wa kisiasa

TOKA MAKTABA:

VYAMA VYA UKOMBOZI VYAKUTANA, COMRADE MIZENGO PINDA AONGOZA UJUMBE WA CHAMA CHA CCM CHA UKOMBOZI WA TANZANIA KTK MKUTANO


 
Kila mtu arudi kwao akatengeneze nchi yake.
Umewahi kuwaona Wajapan, Wakorea, Wa Singapore n.k wakitangatanga nchi za watu??
Wajapani na Wakorea pande za huku niliko wamejazana kama nzige japo hawafikii idadi ya Wachina na Wahindi.
 
Hana tofauti na Samia aliyepachikwa ikulu na Watanganyika lakini anawaua, anawahujumu, anawanajisi, anauza rasilimali zao, anawaibia na anawatesa.
 
Shughuli tofauti, Wakorea mostly ni biashara lakini Wajapani wengi ni kazi za kitaaluma.
Sijawahi kuona Mkorea anafanya biashara za rejareja mtaani. Kama ni biashara kubwa za mabilioni anaajiri watu sioni tatizo hao ndio wahamiaji tunaowahitaji.
 
Umkotho Wesizwe makao yao makuu yalikua Msumbiji Kaburu alivyonusa kuwa wapo huko akakimbilia Lusaka kwa Mzee Kaunda sema ndio hivyo hiyo laana aliyonayo ya Ufisadi bado inamtafuna hadi kwenye ubaguzi sikutegemea kupata kauli za kibaguzi kutoka kwa watu walioishi kwetu kama Zuma na Mbeki.
Mbeki amekua mstari wa Mbele sana kuhusu ubaguzi wa wageni wasibaguliwe anachukiwa hadi na watu wa chama chake kwa sababu hawajui history yao.
 
Hiyo si-ndio siasa

Kwani Huwa unaelewa Nini watu wanapo kuambia ukiwa mwanasiasa lazima uwe kama mwanamke Malaya !?
 
Correct, wanakwepa uwajibikaji
 
Hii ni conspiracy theory tu ya kudogotosha harakati za ukombozi kusini mwa Afrika
 
Mmeharibu nchi ya watu kwa kuwapeleka bangi na madawa ya kulevya, Kazi kukaba watu na kuwapora Mali zao. Rudini tuje tubanane hapa bongo yapo mapori mengi ya kulima ilasomu wa kulima ni mara Moja kwa mwaka ,ujifunze kuweka akiba hadi msomu mwingine
Hili nalo ni neno
 
Laana ya matendo yake dhidi ya wageni itafuna kizazi chake forever
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…