Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

[emoji16][emoji16][emoji16]haya dada.
Sasa nakupa swali la mwisho.
Hyo 25 % wamepewa sababu ni watoto wa mengi au sababu walikuwa wanatia wino kwenye peni?
Kwa sababu mengi ana watoto wanne Sasa.kama kigezo ni watoto wake inatakiwa hzo asilimia zirudishwe wagawane sawa na hao Kaka zao wadogo.maana wote ni watoto wa mengi Wana HAKI SAWA.
Alafu dada ukiwa na hasira mahakamani utakosa HAKI YAKO.
Yaan nimegundua najibizana na kiazi.
 
Familia ya media Ila haijawahi hata siku Moja kutumia media kwenye private matters. Hata kwa sasa business matters ziko handed na waliowaajiri katika nafasi zao na wako independent. Kifupi malezi ya watoto wakubwa wa marehemu Mengi ni Exceptional.
Mkuu Asante sana kwa kututambua. Hatupendagi sifa za kijinga
 
Hawakupewa , walichangia ni shareholders company zao binafsi zipo Ndani ya IPP mfano EATV Mutie na Infocom ni Miku
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]wee unaelewa unachoandika???
 
Walitumia sheria ipi kuwapa hizo Mali.au waliamua tu wazazi?
Nikisema mzee mengi alikuwa anaburuzwa na mkewe nitakuwa nakosea?
Dah aisee.... Kwahiyo ukitaka kumpa mwanao zawadi kuna sheria ya kufuata?

Dunia simama nishuke....
 
Walitumia sheria ipi kuwapa hizo Mali.au waliamua tu wazazi?
Nikisema mzee mengi alikuwa anaburuzwa na mkewe nitakuwa nakosea?
We nae kama zuzu vile, ngoja nikueleweshe kama mtoto wa miaka mi3, Mengi, Mercy, Abdiel & Regina walikua wanamiliki kampuni ya familia kwa pamoja kila mtu na shares zake ila Mercy na Mengi ni mke na mume, na wao kwa sababu ya ndoa na kwa sababu wao ndio waanzilishi basi lazima shares zao ziwe kubwa, hivyo wao wakachukua 75%, then Abdiel akawa anamiliki 12.5 na Regina 12.5, na hii ni kwa sababu ya mchango wao katika kuanzisha na kuendeleza kampuni hio, ila sababu ni familia, wakaziunganisha zote pamoja kama familia moja na maisha yakaendelea (wanaojua mambo ya mgawanyo wa hisa za makampuni zinavokua waneelewa).

Baada ya kutoelewana kati ya wanandoa wawili(Mengi na Mercy), ikabidi watengane na kuamua kugawanya shares zao, yani kila mtu amiliki kivyake, isiwe tena ya pamoja ambayo ilikua ni 75% for two, sasa wakati wa kutengana, sababu kampuni ina 100% shares za umiliki wa pamoja , ikabidi kwanza kabla ya kugawanywa, kila alie na hisa zake arejeshewe hisa zake ili zibaki za hawa wawili kisha wagawane.

Hivyo Abdiel na Regina wakaondoa shares zao kwanza ambazo Abdiel 12.5 na Regina 12.5 na ukiziunganisha ni 25% walizokua wanamiliki, sio urith ni mali yao binafsi (kama wewe unaponunua nguo zako hapo nyumbani kwenu, siku mzee wako na mama wakiachana, wakati wa ugawaji nguo, za kwako utaziondoa sababu haziwahusu), na ndipo hapo inabaki 75%, ambayo wagawane sasa hao walogombana waachane kwa amani kila mtu abebe chake.

Hivyo wakagawiwa kisheria, sio maamuzi binafsi, mahakama na wanasheria walihusika, hivyo wakagawana hiyo 75% ambayo kila mmoja alipata 37.5%, hivyo Mengi alipata 37.5% na Mercy 37.5%.

Baada ya hapo sasa, Mercy ambae ni mama wa wale watoto walioondoa share zao, akaamua kuwarithisha share zake zote watoto wake wawili, kumbuka kampuni inaendelea, huo ni ugawanywaji tu wa shares ama kwa kiswahili tuite kugawiana uhalali wa umiliki wa kampuni kisheria, hivyo watoto wakaziunganisha shares za mama yao 35.5% na za kwao 25%, zikawa 65%, hivyo watoto ndio wakawa wamiliki number moja wa makampuni wakiwa na share kubwa kuliko baba yao.

Uhusiano kifamilia ukaendelea, na mzee alipoona hawezi tena, akawaachia watoto wake wamuendeshee kampuni na kulinda shares zake, hivyo wao wakaingia mazima kwenye kuendesha shughuli za kampuni hadi baba yao alipopatwa na umauti.

Hivyo kisheria ni haki yao kama watoto kurithi pia 37.5% ya mali za baba yao, ambapo kila mmoja angepata 18.75%. Lakini ikatokea kwamba baba yao alikua na watoto wengine wawili ambao alipata akiwa na mama mwingine, hivyo mgao wa hiyo 37.5% ya baba, itagawiwa kwa watu wa 5, ambao ni watoto wa mke mkubwa walietengana wawili, watoto wawili wa mke mdogo na mke mdogo wa marehemu. Hivyo kila mmoja atapata 7.5%, (inaweza isiwe sawa sababu mke mdogo anaweza akaambulia maybe 3-5% sababu ya muda alioishi na huyo bwana, ila watoto watagawiwa sawia wote wanne na mke mdogo atapewa % zake japo ni ndogo tu.

Sasa cha ajabu kikaja kwenye ule wosia, ambao bila sababu za msingi (tuassume ni kweli marehemu aliuandika yeye), matehemu akaacha kugawa hizi mali zake kwa watoto wake wawili, tena ambao kwa facts kabisa ni wao walioshiriki kikamilifu hadi baba yao kupata mali zote, ni wao wamekua bega kwa bega na baba yao, ni wao wamekua na baba yao for years, ni wao wanajua siri zote za baba yao, alafu anammilikisha mali zote mke mdogo, ambae mahusiano yao yamekubwa na utata mpaka kifo chake, then amerithishwa kiiiiiiiiiiila kitu, tena akipata shida basi arithi ndugu wa mke mdogo.

Kisheria, kama marehemu aliwaondoa watu halali katika urithi wake, ni lazima aandike sababu ya kueleweka kwa nini watu hao hawarithishi chochote, la sivyo wosia unakua batili, na mahakama itautupilia mbali, na kugawa kwa taratibu za kisheria za mirathi za nchi husika.

Nadhani umeelewa. Kinachomuumiza jacky ni kua atapata % ndogo tu, tena atalua kama mtu baki kwenye makampuni ya mzee, na watoto wake pia watakua na shares kidogo sana, tofauti na wale wengine, ila ni haki yao. Angefaa tangu mwanzo akae na familia waamue mambo kifamilia, wala wasingemtupa, pengine angejishusha hata wangeweza kuwapa wadogo zao % zote za baba yao, ama wakaziunganisha pamoja kama watoto, wakaendelea kula maisha, ndio hivyo mtaka vyote kwa pupa, hukosa vyote kwa mkupuo.
 
Mnajuaje mambo ya ndani kama haya?...

Too much speculation....acheni hizo
Familia yake si ndio inavyosema. Mzee alikuwa hajui chochote ataandikaje wosia, zaidi ya kuandikiwa!?
 
ashinde mara ngapi?
Unadhani jack atatoka mikono mitupu pale?
Shida alikuwa analazimisha wosia wa mengi aliouandika ndo ukubalike mahakamani.
Lakini panga pangua jack yumo.
Balaa kalitafuta mwenyewe mzee mengi.ACHA MAKASIRIKO.
siku zote wakati mengi yupo duniani anatangaza anaoa,akaoa ulikuwa wapi?kwani ulikuwa haujui mzee mengi ni maji ya jioni?Leo kaondoka ndo mnaamka.itasaidia Nini?
Wewe mbona unajichanganya? Tangu mwanzo hakuna anaekataa Jack kupewa haki yake kama Mjane na aliyeishi na Mumewe kwa miaka 8 tu.Atapata kile alichochuma na Mengi kwa kipindi hicho,bahati mbaya sana Makampuni ya IPP yote ikiwemo Bonite huko hapati ndiyo maana alikuwa anahaha kutaka ule wosia upite,maana she knows anachokwenda kukipata ni kidogo nnje ya Wosia wake.
 
kumbe wewe hata kinachoendelea ukijui.
Huyo anachotaka yeye ule wasia wa mengi ndo upite mahakamani.ila sio Kama kashindwa hatopewa urithi.
Urithi atapata tu sababu,aliolewa na mengi kwa ndoa,na ndoa inatambulika,pili mzee akajikanyaga zaidi kazaa nae watoto.
Pale ndo kifungo kipo maana kwa namna yoyote wale watoto lazma warithi.je watoto wakirithi watashindwa kumpa mama yao?
Yaani hapo lazma jack ale.
Mbaya zaidi hao watoto wawili was jack Wana HAKI SAWA KAMA WALE NDUGU ZAO WAKUBWA.
alafu mbaya zaidi watoto wenyewe ni wanaume.
Kweli wewe huna ulijualo,ngoja tukusaidie kufafanua.Ni hivi hilo swala la WATOTO KUWA NA HAKI SAWA lipo hivi,watakuwa na haki sawa tu kwa ile share ya Baba yao basi.Hata kabla Mengi na mkewe mkubwa hawajafariki tayari hao watoto wakubwa walikuwa wana miliki shares 25%.Ile 75% iliyobaki ilimilikiwa na Wazazi wao kwa maana ya nusu kwa nusu.Hawa wakubwa Mama yao alipofariki wakarithi shares za Mama yao pia.Mpaka hapo unaona nani ana majority shares? Ndiyo maana Jack alikuwa anataka hizi za Mengi apewe yeye peke yake na wanae ndiyo maana kwa Millard Ayo alisema wale wakubwa walisharithi kwa Mama yao kitu ambacho hakiwezekani,hapa sasa point yako inakuja Watoto wote wana haki sawa ya kurithi kwa Baba yao.Kwa maana hiyo hawa Wakubwa watachukua na sehemu ya shares za Baba yao,wakichangaya na zile zao kutoka kwa Mama yao na zao nani anakuwa more powerful?

Ndugu yako Jack alijichanganya tu,alipaswa kuwa na mali zake binafsi wakati Mzee yupo hai,ili watoto wake wanachopata kutoka kwa Baba yao angewaongezea na kile alichonacho yeye Mama yao.Sasa hawa wadogo wanapata kwa Baba tu peke yao wakati wale wakubwa wanapata Kote kwa Mama na Baba yao.Mshauri Jack apambane awatafutie pia wanae ili waje kurithi na kwa Mama yao kama wale wakubwa walivyo rithi kwa Mama na Baba.Tumeelewana?
 
Huwa najiuliza sana, marehemu wakati yupo hai na anamkaza huyu sister kwanini hakumpa shea yake kabisa????
Maana kama Mengi angekuwa anampenda na anataka kumpa mali zake si angempa na kumilikisha wakati yupo hai.
Ila kwa wachagga huyu mama atajuta kuwajua. Tujipe muda
Hivi alikua anafanya kweli kwa hali ile?
 
sasa wewe angalia slay kama wema, kajala,mobeto,zari,jack,gigy money, ambalulu, Lina wooote, hamna cha maana wanachofanya zaidi ya kubadilisha mabwana hadi wanazeeka. wengine wanaweza tumia hata 20m kupanga nyumba, ila hawana kiwanja, hela hiyo basi wangeitumia hata kupata elimu tu kichwani lakin hawana akili
Zari huyuhuyu?
 
[emoji23][emoji23][emoji23] hivi hii foundation ilikuaje ikaangukia mikononi mwake? Halafu hata mtu aniue, sintokaa kamwe nibadilishe jina la babangu kuwa mume wangu. Yeye ndo alimkojolea mamangu? Very stuppid. Siku hizi wengi wameamka aisee. Enzi hizo kila mtu kabadili majina ya babake kwenda kwa Mr. Kuna haki zingine unapoteza hivihivi
Hasa kwenye umiliki wa Assets mlizotafuta pamoja.Mimi nimejifunza kwa Aunt yangu,tunaandika majina yetu wote kila mtu na majina yake aliyopewa na Wazazi wake,hakuna cha Mrs flan hapa.
 
Kajimilikisha na wamemuachia akae nayo then lazima atumie jina la Mzee Ili kupa recognition duniani maana unapozungumza Mengi ni taasisi asseehh....sio mtu mmoja hapo lazima ajitangaze hvyo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Msiba wa ajali ya Precision akatoa pole kutumia uongozi wa Mengi Foundation,nikajiuliza kwa hiyo ile Dr.Ntuyabaliwe Foundation ilijifia yenyewe kwa kukosa pesa.Kwanini yule Shimimana Mengi (inabidi tuwaite hivyo maana ndiyo jina wanalipenda hasa)[emoji3]asiendeleze hiyo ya jina la Baba yao au kilikuwa kijifaundation kilichofulia.
 
Alitaka achukue zote... Kachemka

Watoto wakubwa wanashea 25%

Mengi na mke wa kwanza walikuwa na shea 75% ... Kwahiyo watoto wakubwa tayari wanashea 37.5 za mama yao.

Shea 37.5 za Mengi ndizo Jackie na watoto wake wanatakiwa wagawane na watoto wakubwa wa Mengi.... Maana nao wana haki kwa baba yao.

Kwa kifupi Jakie hana cha kuambulia kwenye shea 62.5 za watoto wakubwa wa Mengi.

Kwaufupi majority shares kwenye mali zote ni abdi el na dada yake, jack kalambishwa mchanga ile control ya mali hana na kitachofuata ni makampuni kua yanaseclare hasara kila wakati ndio ujue wachaga akili nyingi
 
Back
Top Bottom