Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

Kwa kweli hiyo ni roho ya ukatili roho mbaya kabisa kila kitu urithi wewe! Wewe ulimuona huyo Mzee ana kila kitu amechuma na mke mkubwa yaani wewe uchukue tu...
Ila sheria nazo zinatakiwa kubadilishwa zaingalie muda ambao mwenza amekaa na mwezie kwenye ndoa. Siyo fair kabisa mwanamke aolewe na tajiri waishi miaka michache halafu akifa arithi kila kitu
 
Kama nimeelewa hoja za jack za kukata rufaa ni kutaka wosia wa mengi ule wa mwanzo ndo utumike

Yote kwa yote jack hawezi kukosa chochote maana ana watoto wa mengi wawili, kama mengi kaacha watoto 4 wanaofahamika na wale watoto mapacha wapo ndani ni lazma watakuja kugawana sawa na ndugu zao.je mama yapo hatopata ?

na ukiangalia mzee Mali zake kila siku zinaongezeka
Sasa kati yako wewe na Mahakama Kuu kisha Mahakama ya Rufani nani mwenye kujua kuitafsiri vizuri sheria? Unadhani hawakuangalia angle zote hadi wanatoa hukumu? Bahati mbaya sana kwake safari yake ya kuisaka hiyo haki ndiyo imegota.
 
Na yeye kafariki usiku wa kuamkia jana.Wanazika jioni hii.Kwa hiyo mama na watoto wote watatu wamefariki
Daaahh...aseehhh...!!!huzuni kwao kapoteza kizazi chote@Victoire hapo ndo kaeleza ilivokua Kuna family haziingiliwi jamani kwenye mambo ya mirathi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Acha uongo wewe.hawazalishi?
Mzee mengi Mali zake zipo tu hata akilala mipesa inaingia.
Tuache unafiki.unajua utajiri wa mzee mengi?acha mzaha wewe
Wanamsomesheaje watoto wakati hawazalishi wanashinda Mahakamani na case ya Msingi ilikua bado haijatolewa hukumu kwa hiyo kulikua hakuna msimamizi wa Mirathi na akawapandishia case Nyingine ya madai ya child support mabilioni ningekua mimi hapa nisingelipa ada pia
 

Jumamosi, Desemba 3 , 2022

Muhtasari:

Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe, wamekwama kutetea wosia ulioachwa na marehemu baada ya Mahakama ya Rufani kutupa shauri lake la kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu.


Dar es Salaam. Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe, wamekwama kutetea wosia ulioachwa na marehemu baada ya Mahakama ya Rufani kutupa shauri lake la kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu.

Jacquiline alifungua shauri mahakamani hapo la mapitio kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu, iliyokataa wosia uliodaiwa kuachwa na Mengi.
Shauri hilo la mirathi namba 39 ya mwaka 2019, lilifunguliwa na watu wanne, wakiwemo ndugu wa marehemu Mengi.

Mahakama hiyo katika uamuzi wake uliotolewa juzi na jopo la majaji watatu, Rehema Mkuye (kiongozi), Dk Paul Kihwelu na Panterine Kente lilitupa shauri hilo kutokana na kasoro mbili zilizoonekana kwenye kiapo cha Jacquiline na cha wakili wake, Audax Kahendaguza vilivyoambatanishwa katika maombi hayo.

Kasoro hizo ambazo mahakama imekubaliana nazo ni viapo kuwa na maelezo yasiyopaswa kuwemo kwa hoja zinazohitaji ushahidi, maoni, mapendekezo na hitimisho na nyingine ni kutokubainisha chanzo cha taarifa ziliozokuwemo kwenye viapo hivyo.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kutokana na pingamizi la awali lililowekwa na wasimamizi wa mirathi hiyo walioteuliwa na Mahakama Kuu ambao ni Abdiel Reginald Mengi akishirikiana na mdogo wake marehemu Mengi, Benjamin Abrahamu Mengi, kupitia kwa mawakili wao, Michael Ngalo na Roman Masumbuko.

Katika uamuzi huo, mahakama imesema kiapo kinapokuwa na kasoro kama hizo, aya zenye kasoro huondolewa kwenye kiapo na kuendelea na aya nyingine zisizo na kasoro.
Hata hivyo, imesema aya zenye kasoro ndizo msingi wa shauri hilo na kwamba, baada ya kuziondoa zinazobaki haziwezi kusimama zenyewe.
“Kasoro hizo zinayafanya maombi haya kutoweza kusimama, hivyo tunayatupilia mbali. Kwa kuwa shauri linatokana na mirathi hatutoi amri yoyote kuhusu gharama,” imesema mahakama hiyo katika uamuzi huo.

Awali, watu wanne, Benson Benjamini Mengi, William Onesmo Mushi, Zoebu Hassuji na Sylvia Novatus Mushi walifungua shauri la msingi la mirathi Mahakama Kuu wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi hiyo, kwa mujibu wa wosia ulioachwa na Mengi.
Hata hivyo, Abdiel na Benjamini waliweka pingamizi dhidi ya wosia huo unaompa Jacquiline na wanawe haki ya urithi wa mali za Mengi, wakipinga uhalali wake huku wakiwasilisha jumla ya sababu nne za kuupinga.
Mahakama Kuu baada ya kusikiliza hoja za pande zote ilikubaliana na hoja za pingamizi dhidi ya wosia huo na kuikataa kuwa ni batili.

Jaji Yose Mlyambina alikubaliana na sababu hizo za pingamizi huku akisema unawanyima urithi wanawe wengine (wakubwa, Abdiel na ndugu yake) bila kutoa sababu.

Pia Jaji Mlyambina katika hukumu yake hiyo ya Machi 18, 2021, aliukataa wosia huo akieleza kuwa ziliiingizwa mali za mke wake mkubwa na kwamba nakala yake alikuwa nayo mwenyewe Jacguiline Mengi ambaye alikuwa mnufaika.
Hivyo Jaji Mlyambina aliwateua Abdiel na Benjamini kuwa wasimamizi wa mirathi na akaelekeza mali za marehemu zigawiwe warithi wanaostahili kwa utaratibu wa kawaida kama wa mtu ambaye hakuacha wosia.

Mwananchi
amekosea mambo ya sheria ya affidavit, anaweza kuomba extension time to rectify the kasoro and to file again....!
 
Kwa hiyooo.. alitaka akimbie nchi? hakuna kutoroka....
Dubai kuna Bwanake. Hata alipokuwa huko marehemu alikuwa anamwacha Mzee mgonjwa anaenda kwa Bwanake. Familia ilipojulishwa kuwa bana Hali iko hatsrini waliosafiri kimyakimya mpaka hospitali hawakumkuta Danga. Wakampigia simu haikupatokana. Yaani hili ni international Danga.
 
Kama nimeelewa hoja za jack za kukata rufaa ni kutaka wosia wa mengi ule wa mwanzo ndo utumike

Yote kwa yote jack hawezi kukosa chochote maana ana watoto wa mengi wawili, kama mengi kaacha watoto 4 wanaofahamika na wale watoto mapacha wapo ndani ni lazma watakuja kugawana sawa na ndugu zao.je mama yapo hatopata ?

na ukiangalia mzee Mali zake kila siku zinaongezeka
Hapa swala la watoto kupata mgao wao lipo wazi na hakuna anaekataa.Mgogoro hapa ni ule usanii wa ule Wosia,why Jack alitaka kuwaondoa kabisa watoto wa Mzee wale wakubwa?

Alikuwa anafikiria nini hasa kichwani kwake? Umeona Mahakama inavyoweza kukuonyesha kuwa ulichotaka kufanya was totally wrong.Yeye Mjane atapata haki yake kulingana na muda aliokaa na Mumewe lakini pia kwa kuzingatia kile alichochuma na Mzee tu.Kumbuka mali nyingi amezikuta tayari zipo.IPP ameikuta Bonite kaikuta,na nyingine nyingi tu.

Atulie sasa asubiri kupata haki yake.Waliokuwa wanamdanganya nadhani sasa amejifunza kuwa mambo si rahisi kama alivyokuwa anafikiria.
 
Tatozo Jack amei
Sawa watoto watajiunga na ndugu zao, je yeye muda aliokaa naye huyo babu utarudi? Hivi kuolewa na mzee unazani ni kazi ndogo? Basi ndugu zake wangemzuia asioe akae tu mwenyewe, hata Jack asiolewa na huyo mzee angekuwa na maisha mengine, msimfanyie hivyo jamani
Aliidhalilisha hii familia. Yaani amelikoroga mwenyewe Ila kwa kuwa waliambiwa warudi Wakae mezani wakubaliane ni kipi cha kugawa na kipi cha kubaki kuendeleza business legacy ya Mzee basi Ngoja tusubiri. Ila kwa kuwa wameshakosana basi Jack atulie apewe chochote.

By the way ana nyumba kinondoni anakoishi ni yake. Japo ilikuwa na mkopo ila ninaamini iko free sasa.
 
Sasa hyo mirathi miaka yote inasubiri nini kugaiwa?
Hao Nia yao wanataka kmdhulumu jack na watoto wake.ndo maana walikataa kuwalipia ada
Hapa swala la watoto kupata mgao wao lipo wazi na hakuna anaekataa.Mgogoro hapa ni ule usanii wa ule Wosia,why Jack alitaka kuwaondoa kabisa watoto wa Mzee wale wakubwa? Alikuwa anafikiria nini hasa kichwani kwake? Umeona Mahakama inavyoweza kukuonyesha kuwa ulichotaka kufanya was totally wrong.Yeye Mjane atapata haki yake kulingana na muda aliokaa na Mumewe lakini pia kwa kuzingatia kile alichochuma na Mzee tu.Kumbuka mali nyingi amezikuta tayari zipo.IPP ameikuta Bonite kaikuta,na nyingine nyingi tu.Atulie sasa asubiri kupata haki yake.Waliokuwa wanamdanganya nadhani sasa amejifunza kuwa mambo si rahisi kama alivyokuwa anafikiria.
 
Daaahh...aseehhh...!!!huzuni kwao kapoteza kizazi chote@Victoire hapo ndo kaeleza ilivokua Kuna family haziingiliwi jamani kwenye mambo ya mirathi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kuna mtoto mmoja wa kiume amebaki kati ya wale aliozaa na huyu mumewe wa sasa,yupo Marekani anasoma.Nadhani atakuwa amekuja kwenye misiba ya ndugu zake.

Ni kweli ukikuta watu wamechuma mali zao za familia uwe na adabu.Ukijifanya mjuaji ndiyo hayo sasa yanakuja kukutokea.
 
Huyu dada tamaa ya pesa itamfanya apoteze uhai. Amuulize yule mama aliyefariki juzi na wanae kwenye ajali ya gari.Infwakti Yule mama Immaculata Byemerwa kabla ya kuolewa na Engneer alikuwa na yuho mwanae Albert ambae ndo alikuwa dereva. Kaolewa kazaa Janet na Jolister.Na kumbuka kwamba alimkuta Josepahat ana watoto wakubwa .Sasa yule mama kapata ajali na kafariki na uzao wake wote. Kaacha watoto wa mzee wafaidi vizuri mali za baba na mama yao mzazi.
Jack acha tamaa.
Duh

Ova
 
Huyu mwanamke alishindwa kula na kipofu
Kabisa mkuu. Yaani ningetulia tuli. Yaani walipokataa wosia kabla ya kwenda mahakami ningekubaliana tu kuwa Mzee alikosea hivyo.twende tukagawane inavyofaa. Yaani angetoka hapo na Mali ya kutosha na monthly allowance ya nguvu na watoto kusomeshwa.

Acha aisome namba
 
Sasa hyo mirathi miaka yote inasubiri nini kugaiwa?
Hao Nia yao wanataka kmdhulumu jack na watoto wake.ndo maana walikataa kuwalipia ada
Sasa wangegawaje wakati kutwa Bibie alikuwa anaranda randa viunga vya Mahakama kutaka ule wosia wake ndiyo utambuliwe? Kwakuwa mambo yamekwisha,sasa ile hukumu ya mwanzo iliyowatambua Abdiel na Benjamin kuwa ndiyo wasimamizi wa mirathi itafanya kazi na mali zitagawanywa.
 
Hapo kazi wanayo.tena watoto mapacha kila mtoto na urithi wake,na mama yao urithi wake.
Mengi alijua kulitafuta
Sasa wangegawaje wakati kutwa Bibie alikuwa anaranda randa viunga vya Mahakama kutaka ule wosia wake ndiyo utambuliwe? Kwakuwa mambo yamekwisha,sasa ile hukumu ya mwanzo iliyowatambua Abdiel na Benjamin kuwa ndiyo wasimamizi wa mirathi itafanya kazi na mali zitagawanywa.
 
Back
Top Bottom