hili nalo fikirishi sana,Huyo alikuwa Waziri wa TAMISEMI, atuambie wakati ni waziri alifanya nini kutekeleza hayo ambayo leo anataka yafanyike?
CCM wanatulaghai kwamba wakijazana wenyewe bungeni wanaweza kuikosoa na kuishauri serikali ila ni utapeli mtupu.
wawe makini tu kwenye planning, kusije kua na malalamiko kama ya kota za magomeniBuguruni HAPO vingunguti, huwa pananisikitisha SANA, KWA NINI hao WATU wasilipwe pashushwe ghorofa za KUFA MTU mambo mengine tuweke siasa pembeni hiyo njia ni potential SANA kuelekea airport, taifa, kariakoo, hapapaswi kiwa hivyo, pavunjwe pajengwe kisasa Niko na WEWE jafo, ASANTE kunwakilisha kaka
Hilo ndio tatizo letu sisi waafricaAna hoja. Swali kwa nini hata maeneo mapya hayapangwi bado yanajengwa kiholela. Mfano chanika. Mbande etc
Kuwa positive. Hii ndio njia ya kuondoa makazoi holela. Wakati ujenzi unaendelea wanapewa hela ya kodi muda wote wa ujenzi(wamiliki) ujenzi ukikamilika wanapewa nyumba kila mmiliki..Mwamba mmoja ameishauri kuvunja maeneo ya pembezoni kama Buguruni, Vingunguti, Tandale na maeneo mengine ili kujenga maghorofa na kuupa hadhi Mkoa Dar es Salaam.
Haha swali mkivunja wananchi wakaishi wapi??
Hayo majengo mnayotaka kujenga pamekosekana sehemu nyingine mpaka buguruni vingunguti???
Na je hayo magorofa unayotaka huko kwako hakuna sehemu ya kujenga kwann usishauri waje kukujengea huko najua mapiri yamejazanaa ila wanaweza kuwafikiria[huu ushairo tu]
Kwa style hiii watu wa manzese mjiandaee ila fanyeni yoote wachaga wa kmr msikae hata kuwataja huko mnapoongelea.........
All the best
Ulibadilika uongozi.Naunga mkono hoja serikali inatakiwa ije na mpango mwingine juu ya mpangilio wa makazi ya watu na nyumba bora kwani mbona wakoloni walipangilia vizuri miji yao na walijenga nyumba nzuri nini kilibadilika baada ya uhuru?
Kwani walipovunja Magomeni Kota, wenyeji waliishi wapi?. Sasa baada ya mradi kukamilika si wanaishi wao!.Mwamba mmoja ameishauri kuvunja maeneo ya pembezoni kama Buguruni, Vingunguti, Tandale na maeneo mengine ili kujenga maghorofa na kuupa hadhi Mkoa Dar es Salaam.
Haha swali mkivunja wananchi wakaishi wapi??
All the best
Hizi siyo nyumba bali ni uchafu. Zivunjwe zote na zijengwe nyumba za ghorofa na hao waliovunjiwa wapewe unit hapo. Watakaokuwa wamepewa hizo sehemu, watarudisha pesa yao kwa kupangisha units zingine kufidia gharama. Lakini hivi vibanda vichafu vivunjwe vyote na ziwekwe barabara na sewage systems.
Unanikumbusha mambo ya NERO ya Warumi. " tuchome mji huu kwani unanuka.."Kuwa positive. Hii ndio njia ya kuondoa makazoi holela. Wakati ujenzi unaendelea wanapewa hela ya kodi muda wote wa ujenzi(wamiliki) ujenzi ukikamilika wanapewa nyumba kila mmiliki..
Hizo hapo zilivyo siyo nyumba, wala haifai hata kuita vibanda.......Yavunjwe, na yajengwe makazi mapya, watakaovunjiwa wapewe units kwenye hayo maghorofa. Watakaojenga watajilipa kwa kupangisha watu wengine watakaohitaji makazi ya kupangisha au kama watanunua ni sawa. Hizo siyo nyumba, labda mabanda ya kuku.Kwani walipovunja Magomeni Kota, wenyeji waliishi wapi?. Sasa baada ya mradi kukamilika si wanaishi wao!.
Mandate ndio mitaa yangu, waje wavunje, tuhamie Mbagala kibonde maji kwa muda, pakikamilika turudi, na sisi tukae ghorofani jameni, kila siku kuwaona tuu wenzetu wako juu maghorofani, huku wanatupiga tuu deo za wake zetu kwenye passport size, na mwisho wa siku kuishia kuwatokea !.
P
Tunataka barabara, sewage systems, maji na umeme wa uhakika. Hizo ni slums ambazo hazifai hata kukalika.Zinavunjwa kwa awamu. Hilo ni eneo kubwa sana na wanaishi watu wachache wakati wanaweza kuishi watu mara kumi ya hao na kuwa karibu na huduma za jamii.