Jafo: Vingunguti, Tandale na Buguruni pavunjwe pajengwe Maghorofa

Jafo: Vingunguti, Tandale na Buguruni pavunjwe pajengwe Maghorofa

Wa US hawawezi kukubali kuingia kwenye kashfa ya kupora kiwanja. Walifika bei. Kama kuna sababu ya maslahi ya umma ardhi inaweza kuchukuliwa. Serikali haiwezi kufanya gentrification na kudai inafanya maslahi ya umma.
Tafuta taarifa. Serikali ikitaka kujenga hapo vingunguti hakuna wa kuzuia.
 
Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo, akizungumza Bungeni Februari 5, 2026, ameishauri Serikali kuvunja maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, yakiwemo Buguruni, Vingunguti na Tandale, ili kujenga maghorofa na kupendezesha jiji hilo.

Kama serikali ina mpunga wa kutosha kuwalipa watu fidia wavunje tu ila wasilete janjajanja kwenye fidia.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Wala huhitaji kulipa watu kodi, kinachotakiwa hapo ni serikali kuwapa miaka miwili tu kila mwenye kiwanja ajenge ghorofa kuanzia tano, atakayeshindwa auze kiwanja au aingie mkataba na watu wanaoweza kujenga hivyo, halafu vibali vipya vya ujenzi vinatolewa kwa kiwanja cha kuanzia square meters 800 tu na lazima kuwepo na barabara.
Tatizo viwanja vimepimwa kizamani avikuzingatia kanuni za mji wa kisasa...Barabara ni za gari tu hakuna njia ya watembea kwa miguu nk eneo lote la buguruni linatakiwa kuvunjwa na kupimwa na kudizainiwa upya...shule zote zijengwe za kisasa nk
 
  • Thanks
Reactions: Lax
CCM huwa hawawezi kushugulika na mambo magumu yanohitaji kutumia akili kubwa na usimamizi thabiti wa sheria, mfano suala la Wamachinga kufanya biashara barabarani limewashinda kabisa kutatua kabisa.
jambo hili walitakiwa kulisimamia haka kwa ubabe au nguvu tusingefika hapa tulipo lakini wao hata kustuka, tumejenga holela kiasi kwamba zile zoezi la anuani za makazi lilipofanyika hata wewe mwenyeji unajiuliza sasa hapa hizi namba watapanga vipi ili ziwe zinaeleweka.

kwenye maeneo mapya wapitishe sheria kali, suala la wamachinga nakuunga mkono kwa asilimia 100. barabarani mtembea kwa miguu anapata tabu sana, hawa jamaa wangekua wanawekwa sehemu moja katika maeneo mbalimbali ili mwenye uhitaji awafate, sasa huku unakwepa daladala na pikipiki ukigeuka huku kuna kalai la mafuta
 
Tatizo viwanja vimepimwa kizamani avikuzingatia kanuni za mji wa kisasa...Barabara ni za gari tu hakuna njia ya watembea kwa miguu nk eneo lote la buguruni linatakiwa kuvunjwa na kupimwa na kudizainiwa upya...shule zote zijengwe za kisasa nk
hata neno "kupimwa" hafai kulitumia, viongozi hawa toka wameanza kwenda ulaya ni kama hakuna kitu wamejifunza
 
Ana hoja. Swali kwa nini hata maeneo mapya hayapangwi bado yanajengwa kiholela. Mfano chanika. Mbande etc
Plus kisemvule,vikindu, Kivule,Msongola,Mbondole,kitonga na Mvuti itafuata soon..
Ila kigamboni,mbweni Kwa sababu hasa wananua wao kidogo walipima viwanja
 
Tafuta taarifa. Serikali ikitaka kujenga hapo vingunguti hakuna wa kuzuia.
Yap ardhi ni Mali serikali/Rais(ujamaa) lakini haki za binadamu tumezisaini mzee lazima zifuatwe, refer bomoa bomoa Kwa hata wasiohusika kule Mbezi Kimara na bomoa bomoa zingine za nyumba kando kando barabara bila fidia nk mpaka kesi zingine zikiwa mahakamani, Bado ishu ya kuwahamisha wa maasai Ngorongoro nk so naimani serikali haitataka kurudia hayo makosa tena
 
Kuna njia za kufuata serikali ikitaka ardhibyako na hutaweza kuzuia. Achana na hizo bomoabomoa anazoamua mtu kwa utashi wake kisa ni waziri sijui diwani. Ila serikali ikilitaka eneo lako mwa maslahi yabtaifa huwezi kuzuia.
 
Mbunge wa Kisarawe, Selemani Jafo, akizungumza Bungeni Februari 5, 2026, ameishauri Serikali kuvunja maeneo ya pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, yakiwemo Buguruni, Vingunguti na Tandale, ili kujenga maghorofa na kupendezesha jiji hilo.

Kwa hiyo kubomoa nyumba za wavuja jasho na kujenga maghorofa ya matajiri ni maendeleo ???
NONSENCE
Mbona huko Oysterbay hawataki kujenga maghorofa kama ndio maendeleo?
 
Hakuna kitu kinacho niuzi ndani ya Jiji la Dar es salaam kama slums na hawa machinga kupanga biashara hovyo.Mpaka Najiuliza hata Kwa PK tumeshindwa kuiga ?
 
Kuboresha miundombinu kuendane na kutoa elimu kwa jamii namna gani bora ya kuitunza.

Isije kuwa kama ule mradi wa Magomeni, wahusika wameshindwa kulipa elfu 30 tu ya maintenance.
 
Hakuna kitu kinacho niuzi ndani ya Jiji la Dar es salaam kama slums na hawa machinga kupanga biashara hovyo.Mpaka Najiuliza hata Kwa PK tumeshindwa kuiga ?
kwenye mambo ya regulations tunafanya vibaya sana, hivi kwasasa tatizo la pikipiki kutofata sheria za barabarani leo hii ukiziuliza mamlaka, tatizo lilianza wapi na way forward ni nini, na wanajifunza nini kwenye jambo hilo, unadhani utapata majibu ya kueleweka?
 
Kwa hiyo kubomoa nyumba za wavuja jasho na kujenga maghorofa ya matajiri ni maendeleo ???
NONSENCE
Mbona huko Oysterbay hawataki kujenga maghorofa kama ndio maendeleo?
Unajua sababu aliyosema ya kuvunja Tandale,Vingunguti na maeneo kama hayo? Oysterbay haina hilo tatizo. BTW Oysterbay sasa hivi wanajenga sana maghorofa kiasi cha kuharibu plan yake halisi. labda kama hupajui.
 
CCM huwa hawawezi kushugulika na mambo magumu yanohitaji kutumia akili kubwa na usimamizi thabiti wa sheria, mfano suala la Wamachinga kufanya biashara barabarani limewashinda kabisa kutatua kabisa.
chalamila aanza na kariakoo kuanzia sasa barabara za kariakoo ziwe nyeupe, tuangalie utekelezaji sasa

kauli imetoka kwenye uzinduzi wa soko la kariakoo
 
Unajua sababu aliyosema ya kuvunja Tandale,Vingunguti na maeneo kama hayo? Oysterbay haina hilo tatizo. BTW Oysterbay sasa hivi wanajenga sana maghorofa kiasi cha kuharibu plan yake halisi. labda kama hupajui.
Bonde la msasani pavunjwe,kinondoni shamba pavunjwe
Pia sehemu zote hizo ni prime area
Maeneo hayo hayawezi kuwa ovyo ovyo

Ova
 
Bonde la msasani pavunjwe,kinondoni shamba pavunjwe
Pia sehemu zote hizo ni prime area
Maeneo hayo hayawezi kuwa ovyo ovyo

Ova
Unapajua pale Ali bin Said? Upande mmoja Obay ukivuka barabara slum za Namanga.
Ni sawa na Kino shamba ukivuka barabara ushuani Ada Estate.
 
Back
Top Bottom