Jafo: Vingunguti, Tandale na Buguruni pavunjwe pajengwe Maghorofa

Tatizo la Migomigo, baadhi ya nyumba walikutwa wapangaji, ndio wakaandikishwa , nyumba zimekamilika, wanaibuka wenye nyumba kutaka units, huku wapangaji wameisha milikishwa.

Wale waliokutwa, wanapewa nyumba bure na kuendelea kulipa kodi kuzinunua, wale wapya wanauziwa, sasa wenye nyumba wanataka bure, kitu ambacho hakiwezekani
P
 
Ana hoja. Swali kwa nini hata maeneo mapya hayapangwi bado yanajengwa kiholela. Mfano chanika. Mbande etc

Kwa hiyo Chanika na Mbande unapimiwa miguu na kuonyeshwa mnazi kama mpaka, unanunua, unajenga. Hakuna ramani ya kiwanja wala ramani ya mipango miji.

Unapataje kibali cha ujenzi ?
 
ANZA KUVUNJA KISARAWE KWANZA MJE BUGURNI
 
i dont understand, mbunge wa kisarawe anataka magorofa yajengwe dar? kwani huko kisarawe matatizo yameisha hadi aingilie mambo ya mkoa mwingine? kwa nini asijishighulishe zaidi na mambo ya jimboni na mkoani kwake kwanza? ...
Kisarawe na Dar yote ni Tanzania.
 
I'm against this illegitimate government ila unplanned squatters(unplanned settlements) zinapaswa kubomolewa zote kama funds zipo za kujenga maghorofa, tatizo la Bongo maeneo unplanned yanazidi kuongezeka huku serikali ikibung'aa macho tu bila ya kufanya lolote. Mipango miji ni sifuri kabisa Tanzania nzima.
 
Ni wazo zuri sana, lakini kwenye nyumba za urithi kutakuwa na mushkeli kidogo na ningependa pia kumshauri kisarawe asisubiri pawe kama Kariakoo na Magomeni au Tandale yeye asimamiye mipango miji ya kisasa itakayowezesha Kisarawe kuwa kama Rwanda.
 
hilo swali hua najiuliza kila siku shida ipo wapi ya kuamua kwamba ujenzi holela sasa marufuku, maana muda unakwenda na ujenzi holela unaendelea tu kwenye miji mpya inayochipukia, na wakati watu wa mipango watu ardhi wapo
CCM huwa hawawezi kushugulika na mambo magumu yanohitaji kutumia akili kubwa na usimamizi thabiti wa sheria, mfano suala la Wamachinga kufanya biashara barabarani limewashinda kabisa kutatua kabisa.
 
Huyu jamaa huwa namwona kama anajielewa sana, serikali inunue hayo maeneo yote ikabidhi shirika la nyumba wajege
 
Naunga mkono hoja serikali inatakiwa ije na mpango mwingine juu ya mpangilio wa makazi ya watu na nyumba bora kwani mbona wakoloni walipangilia vizuri miji yao na walijenga nyumba nzuri nini kilibadilika baada ya uhuru?
Kilichobadilika ni aina ya watu na uwezo wao wa akili.
 
Wahamie vikindu au homboza wapewe viwanja Bure na fidia juu yake
 
Kwa hiyo Chanika na Mbande unapimiwa miguu na kuonyeshwa mnazi kama mpaka, unanunua, unajenga. Hakuna ramani ya kiwanja wala ramani ya mipango miji.

Unapataje kibali cha ujenzi ?
Hayana vibali vya ujenzi, na zile nyumba zinaweza kubomolewa bila kulipiwa fidia.
 
Mada imetawaliwa na chuki za kisiasa. Njia mojawapo ya kuondoa makazi holela ni hio. Kubomoa vibanda vibovu vilivyokaa bila mpangilio na kujenga makazi ya jumuia huku kila aliekuwa na nyumba hapo anapewa nyumba moja.
Uchumi wa watu wa maeneo hayo hauendani na maghorofa. Hawezi kuuza genge, 'kiosks', gongo, ubuyu, mkaa, miguu ya kuku, uduvi, mamantilie, chips zege, 'kinyozi etc

Happ hakuna kuwajengea makazi, ni kufurusha watu.
 
Uchumi wa watu wa maeneo hayo hauendani na maghorofa. Hawezi kuuza genge, 'kiosks', gongo, ubuyu, mkaa, miguu ya kuku, uduvi, mamantilie, chips zege, 'kinyozi etc

Happ hakuna kuwajengea makazi, ni kufurusha watu.
Hilo ndiyo lengo kuu, pangisha apartment buguruni uende ukaishi Mabwepande au Chanika. There's nothing wrong with that.
 
Mimi sipendelei maghorofa.Ubaya wa mazingira yale umesababishwa na mipango miji mibovu chini ya wizara ya ardhi.makazi yangekuwa yanapimwa kabla ya mtu kujenga kusingekuwa na muonekano mbaya kama maeneo hayo hata kama nyumba ni ndogo.
 
i dont understand, mbunge wa kisarawe anataka magorofa yajengwe dar? kwani huko kisarawe matatizo yameisha hadi aingilie mambo ya mkoa mwingine? kwa nini asijishighulishe zaidi na mambo ya jimboni na mkoani kwake kwanza? ...
Labda bado yuko na mawazo ya uwaziri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…