Jaji Bomani apigilia msumari Katiba Mpya

Jaji Bomani apigilia msumari Katiba Mpya

Tusubiri NEC waamue mbona mnataka kujipa madaraka ya NEC? msilete hoja za ajabu zenye kuleta malumbano yasiyo na maana humu ndani, kila kitu kitaenda kadri kilivyopangwa jamani musiwe vihelehele kuwasemea wahusika.

Wewe sidhani kama hata chekechea ulifaulu; Hebu fanya tu hesabu za kujumlisha ambazo ni simple kabisa kwamba Njombe na Ludewa wameana kujiandikisha tangu Mwezi February 2015 na hadi sasa zoezi bado kukamilika. Nchi yetu ina Wilaya 169 na Wilaya 2 zinachukua miezi 2 kufanya registration ya BVR kwa hiyo kwa Wilaya 169 kama spidi ni hii hii zoezi hili litachukua miezi 169 ambayo ni sawa na miaka 14.
 
Wewe kubwa jinga ebu uwe unaelewa kuwa kutangulia sio kufika!! wewe umejiunga hapo zamani lakini huna hoja zozote za maana na unabaki kucopy na kupaste life span za ID za watu humu ndani, hilo wala halikusaidii kitu chochote, we utapost weeee mwisho wa siku utachoka labda uwe umetumwa yaani uwe mchumia tumbo. Endelea tena kwa kasi zaidi kupost hizo ID

Sasa hapa mchumia tumbo nani?? au aliyetumwa ni nani?? Mimi au wewe within 2 days una post 60. Una kazi ya kufanya au ni jobless?? Au ndio mmeshaingiziwa boom la Pasaka huko vyuoni mnakuja kusumbua hapa?? by the way ucngzini, ucjali ni vitu gani?? hiyo inatuonesha picha tosha wewe ni nani.. FOOL
 
Nina wasiwasi mkubwa na uwezo wa kufikiri huyu profesa wa kichina
 
Sasa hapa mchumia tumbo nani?? au aliyetumwa ni nani?? Mimi au wewe within 2 days una post 60. Una kazi ya kufanya au ni jobless?? Au ndio mmeshaingiziwa boom la Pasaka huko vyuoni mnakuja kusumbua hapa?? by the way ucngzini, ucjali ni vitu gani?? hiyo inatuonesha picha tosha wewe ni nani.. FOOL

Wewe ndo FOOL X 1,000,000 unadhani una hoja za maan unazoweka zaidi ya kubwabwaja kama gari la matangazo, kama umetumwa waambie humu hatuhitaji wachumia tumbo kama wewe. Tuko kujua uzuri wa Katiba pendekezwa na sio kuuza sura kama unakofanya wewe.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mstaafu, Jaji Mark Bomani, ambaye pia ni mtaalam nguli wa Katiba, ameonya kuwa iwapo upigaji wa kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa utalazimishwa kufanyika Aprili 30, mwaka huu, wakati dalili zote zinaonyesha kuwa haiwezekani, unaweza kuzua mtafaruku mkubwa nchini.

Ili kuepusha hali hiyo, ameshauri kura ya maoni iahirishwe hadi baadaye, badala yake Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) iendelee na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa ajili ya kutumika katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

Pia, amependekeza kuwa Katiba inayotumika sasa ya mwaka 1977 iboreshwe kwa kuingiza ndani yake mambo mbalimbali, akiwamo mgombea binafsi.

Jaji Bomani ambaye ni mtaalam nguli wa Katiba aliyewahi kuandika katiba za nchi mbalimbali, zikiwamo za Namibia na Burundi, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Alisema nia nzuri ya Rais Jakaya Kikwete, ya kuipatia Tanzania Katiba mpya, iliharibika baada ya kuundwa kwa Bunge Maalum la Katiba (BMK).
Jaji Bomani alisema hilo lilidhihirika baada ya baadhi ya wajumbe wa BMK kujitoa katika Bunge hilo.

"Hili lilikuwa doa kubwa sana kwa mchakato wote. Ilikuwa ni mwanzo mbaya," alisema Jaji Bomani.

Aliongeza: "Kazi yake (BMK) haikuwa nzuri, haikuridhisha, kwani iliwagawa watu."

Alisema licha ya baadhi ya wajumbe wa BMK kubaki kwenye Bunge hilo na kuendelea na mchakato hadi kutoa Katiba inayopendekezwa, bado anaona kuna matatizo mawili.

La kwanza, alisema ni kuwapo baadhi ya makundi na watu wanaoamini kuwa Katiba inayopendekezwa imetupilia mbali baadhi ya mambo yaliyopendekezwa na iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba yaliyotokana na maoni ya wananchi, hivyo wanaipinga na baadhi yao wanatishia kutoipitisha.

"Hili ni jambo la kusikitisha, lakini siyo jambo la kupuuza. Katiba siyo kitu kinachotegemea kura, bali inatakiwa iwe na muafaka. Kitu hicho Katiba za Namibia na Burundi inacho," alisema Jaji Bomani.

Alisema katiba ya nchi ndiyo sheria mama na msingi wa kuendesha nchi na kwamba uzuri wake, sharti iungwe mkono na wengi.
Alisema Katiba inayopingwa na kundi kubwa la watu, ni chanzo cha mfarakano kwenye nchi.

Alisema endapo katiba ya namna hiyo inapigiwa kura nyingi za `hapana' au inapingwa na upande mmojawapo wa Muungano iwe Zanzibar au Tanganyika, basi hatima yake ni kuvunja Muungano na kuhoji: "Je, ni sawa tufike huko?"

La pili, alisema ana wasiwasi mkubwa juu ya uwezekano wa kura hiyo kupigwa Aprili 30, mwaka huu, kwani hadi kufikia jana uandikishaji wa wapigakura katika daftari la kudumu la wapigakura ulikuwa ukisuasua.

"Naambiwa eti mpaka sasa waliokwishaandikishwa hawazidi hata milioni moja. Hapo takriban zaidi ya milioni 20 wataandikishwa katika wiki nne zilizobaki? Nafikiri itakuwa ni muujiza kufanya hivyo," alisema Jaji Bomani.

Aliongeza: "Sasa tufanyeje? Tuendelee na kura ya maoni ambayo ni idadi ndogo ya wapigakura walioandikishwa ndiyo watakaoshiriki, tena kwa suala zito kama la Katiba? Tukifanya hivyo tutakuwa tumefanya kosa kubwa sana ambalo litatuletea mgogoro mkubwa na manung'uniko mengi sana nchini. Hivi kweli tufike hapo?"

"Mapendekezo yangu ni kwamba kura ya maoni juu ya Katiba mpya iahirishwe mpaka baaadaye. Badala yake Tume ya Uchaguzi iendelee na uboreshaji wa daftari la wapigakura tayari kwa uchaguzi mkuu Oktoba 2015. Ikiwezekana hata tuachane na mfumo wa BVR (mfumo mpya wa kielektroniki wa Biometric Voters Registartion), ambao umewapa shida hata wenzetu Kenya na Nigeria."

Hata hivyo, alisema kwenye rasimu ya iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Katiba inayopendekezwa, kuna mambo mazuri, hivyo akashauri yafanyiwe mabadiliko katika iliyopo ili yatumike kwenye uchaguzi wa Oktoba, mwaka huu.

Aliyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na uwakilishi sawa wa jinsia, mgombea binafsi, mgombea urais kupata asilimia 50 au zaidi ili ashinde na Tume Huru ya Uchaguzi.

"Katiba iliyopo inaweza kufanyiwa mabadiliko haraka haraka, tuseme kwenye kikao kijacho cha Bunge tayari kwa matumizi ya uchaguzi mkuu ujao. Litakuwa ni jambo la kusikitisha kuwa hata yale mazuri yasiyo na ubishi yasitumiwe kwenye uchaguzi huo," alisema Jaji Bomani.

Aliongeza: "Unahitajika muda zaidi wa mazungumzo. Kwani Watanzania tunataka nini au Mtanzania wa kawaida anataka nini? Anataka maisha yake yaboreke, hawataki Muungano wa serikali mbili, tatu wala moja, hivyo ni vitu vya uongozi, havitakiwi uhasama."

Alisema kura ya maoni haiwezekani kufanyika Aprili 30, mwaka huu kwa kuwa maandalizi hayajafanyika ya kutosha, kwani wapigakura kati ya milioni 20 hadi 23 wanaotarajiwa wanatakiwa wote wapewe nafasi ya kupiga kura.

"Ukiangalia kwenye maandalizi, hatujafika hata nusu. Nina wasiwasi kama hiyo tarehe 30 itafika wote watakuwa wameandikishwa. Tulipe muda. Tusijiongeze kitu kitakachoongeza mfarakano," alisema Jaji Bomani.

CHANZO: NIPASHE

mzee BOmani tunakuheshimu sana na mawazo yako ila ukumbuke ww sio taaasisi iliopewa jukumu la kusema kuwa kura ya maoni itafanyika au laa! Tuwape nafasi taasisi husika zilizopewa mamlaka kisheria watatupa utaratibu kama kuna mabadiliko au Laa! Imekuwa ni kawaida kwa watanzania wachache kuwa waseMaji wa taasisi husika ili hali wanatoa majibu huku wakisema nadhani........... Yani hawana uhakika,kwa hili la kura ya maoni tuwaachie wahusika tume ya taifa ya uchaguz
 
Wewe ndo FOOL X 1,000,000 unadhani una hoja za maan unazoweka zaidi ya kubwabwaja kama gari la matangazo, kama umetumwa waambie humu hatuhitaji wachumia tumbo kama wewe. Tuko kujua uzuri wa Katiba pendekezwa na sio kuuza sura kama unakofanya wewe.

Join Date : 31st March 2015
Posts : 69

Wakutumwa anaonekana tu.. huwezi kutumia akili nyingi kilijua hilo..
 
Mwambie mkuu na Judge ametoa tuu ushauri hajasema kuwa NEC ifuate ushauri wake au kutekeleza mawazo yake na Judge ana uhuru wa kutoa maoni yake hafungwi kna chochote mradi havunji sheria

Huyo judge kama raia mwingine wa Tz katoa ya moyoni, lakini na yeye namuomba aendelee kuwa mfuatiliaji wa taarifa mbalimbali za Serikali zinzotolewa,Tayari serikali imeshatoa tamko bungeni jana via PM kwa hiyo atulie mchakato huu ni wa watanzania na utakwenda vizuri sana hakuna haja ya mtu kuleta vitisho wala hofu hapa.
 
Tatizo kubwa ni uchambuzi wa mambo, hii kitu hakiwezekani kwa akili ya kawaida ila watu kama wewe hata kwetu wapo. Nadhani umenipata mkuu
 
kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni na ushauri wake kama mtanzania, Nashanga kuna watu wanatokwa na povu kwa kauli ya jaji. Tuweni wapole hata ninyi mna wakati wa kutoa maoni yenu kama watanzania. Acheni dharau na matusi kwa mzee wa watu. Kumbukeni fahari ya wazee ni mvi na ushauri.

Wengine mnapenda ushauri mnaoupenda nyie tu? lazima tushindane kwa hoja na sio matusi
 
Akili yake ina shida kubwa... anasema kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa, sasa sijui wamepanga nini??

Busara hapa inahitajika,zoezi la kuipaigia kura katiba inayopendekezwa haliepukiki hapa cha kufanya ni kuelewa tu na kufuatilia taarifa mbalimbali zinazotolewa na serikali ili tujenge uelewa siku ikifika tukafanye maamuzi yetu.
 
Wewe sidhani kama hata chekechea ulifaulu; Hebu fanya tu hesabu za kujumlisha ambazo ni simple kabisa kwamba Njombe na Ludewa wameana kujiandikisha tangu Mwezi February 2015 na hadi sasa zoezi bado kukamilika. Nchi yetu ina Wilaya 169 na Wilaya 2 zinachukua miezi 2 kufanya registration ya BVR kwa hiyo kwa Wilaya 169 kama spidi ni hii hii zoezi hili litachukua miezi 169 ambayo ni sawa na miaka 14.
Basi kama mimi sikusoma chekechea bora ya wewe uliyesoma NGUMBARO lakini bado akili yako haina akili maana hayo mambo uloyaweka hapo juu yako nje ya uwezo wako waachie wahusika, lakini tambua kuwa suala la kura ya maoni liko pale pale. kama huna hoja lala.
 
Join Date : 31st March 2015
Posts : 69

Wakutumwa anaonekana tu.. huwezi kutumia akili nyingi kilijua hilo..

Wewe ulisoma Ngumbaro una matatizo ya akili nahc ulikimbia Milembe na unahitaji urudishwe tena, alokwambia kujiunga zamani ndo kujua kutoa hoja nani? kubwa jinga tu wewe unapoteza muda wako bureeee wewe na hapo kwenu ndo mmetumwa na ni wachumia matumbo tu.
 
kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni na ushauri wake kama mtanzania, Nashanga kuna watu wanatokwa na povu kwa kauli ya jaji. Tuweni wapole hata ninyi mna wakati wa kutoa maoni yenu kama watanzania. Acheni dharau na matusi kwa mzee wa watu. Kumbukeni fahari ya wazee ni mvi na ushauri.

Wengine mnapenda ushauri mnaoupenda nyie tu? lazima tushindane kwa hoja na sio matusi

NGUDEKELA na wewe uwe na busara naomba uelewe kuwa ufahamu wa watu juu ya mambo fulani unatofautiana, Bomani katoa ushauri na ushauri unaweza kukataliwa kwa kupingwa au kukubaliwa, it depends na ulivyokuja kwa makundi husika,kwa hiyo lugha za matusi sio mahala pake humu kumuambia mwenzio anatoa povu sio ustaarabu jenga hoja ueleze nini ulichonacho maana kila mtu ana haki.
 
Kwa hiyo wewe kwa akili zako, unakataza watu wasitoe mawazo yao? Kama unaogopa mijadala usiende kwenye forums.

Nani kakuambia Judge anawakilisha NeC? Au kwako wewe unataka hata NeC isishauriwe? NEC ndio wamekutuma kwamba hawataki ushauri?

Ikilazimishwa kura kinyume na taratibu, nini mawazo yako tayakuwa?

Tusubiri NEC waamue mbona mnataka kujipa madaraka ya NEC? msilete hoja za ajabu zenye kuleta malumbano yasiyo na maana humu ndani, kila kitu kitaenda kadri kilivyopangwa jamani musiwe vihelehele kuwasemea wahusika.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo kubwa ni uchambuzi wa mambo, hii kitu hakiwezekani kwa akili ya kawaida ila watu kama wewe hata kwetu wapo. Nadhani umenipata mkuu

Sijakupata kabisa,ingekua haiwezekani watanzania wasingekubali kutoa maoni na wasingevumilia kuona fedha zao zikipotea kwa jambo lisilowezekana, Tanzania sio nchi ya kushindwa kufanya mambo ya msingi, hapa suala la lini na wapi hilo endelea kufuatilia taarifa za serikali kupitia mamlaka husika sote tutafqhamu nini kinqendelea ili wajibu wetu uendelee kubaki palepale.
 
Sasa hapa mchumia tumbo nani?? au aliyetumwa ni nani?? Mimi au wewe within 2 days una post 60. Una kazi ya kufanya au ni jobless?? Au ndio mmeshaingiziwa boom la Pasaka huko vyuoni mnakuja kusumbua hapa?? by the way ucngzini, ucjali ni vitu gani?? hiyo inatuonesha picha tosha wewe ni nani.. FOOL
huyu bwana mdogo ana matatizo ya kisaikolojia....hajui lolote humu analeta umuchknow,na ni mbishi kufundishika..hawa watoto ni wakuchapwa viboko..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom