Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Nakubaliana na hoja zako ila hoja ilikuwa kwamba;
tuhuma alizo zitoa Mbowe na Mawakili wake dhidi ya Jaji Luvabda eti kuwa amepewa maelekezo kutoka juu kuwa amfunge Mbowe, tuhuma hizi zilipaswa zithibitishwe kwanza kabla ya Jaji kujitoa kusikiliza kesi hiyo.
nasema hivyo kwa sababu zifuatazo;

1. Tuhuma zilizo tolewa dhidi ya Jaji ni tuhuma nzito ambazo sio tu kwamba zinamchafua yeye Jaji Luvanda bali zinawachafua Majaji wote wa Tanzania bara na Muhimili wa Mahakama kwa ujumla wake kuwa hawatendi haki.
Tuhuma hizo zilipaswa zithibitishwe kwanza, huko ni kuichafua Mahakama, na wananchi wa kawaida watapoteza IMANI na MAHAKAMA.
Mahakama ndio Tegemeo la wananchi sasa kama tutaacha uchafuzi kama huu uendelee basi Mahakama inaenda kuangua na haito aminiwa na wananchi.
 
SWALI KUU KUHUSU MWENENDO WA KESI HII YA MBOWE NA WENZIE WATATU
Mheshimiwa Jaji Elinaza Benjamin Luvanda kuna swali zito sana toka kwa Askofu Bagonza anayejiuliza yafuatayo katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana imetendeka:

1.Serikali / Jamhuri ndivyo ilivyoshtaki.
2.Jaji E. B Luvanda kakubali mashtaka ya serikali yana kasoro
3.Jaji E.B Luvanda anaelekeza namna nzuri ya serikali kumshtaki Mbowe
4.Kwa hiyo
a) Jaji alipaswa amwachie Mbowe.
b) Mbowe hashtakiwi na Jaji anashtakiwa na serikali kupitia ofisi za mwendesha mashtaka DPP na Mawakili wa serikali, vipi jaji na yeye kujiunga upande wa Jamhuri kuwaelekeza kazi ifanywe vipi kisha wamletee halafu hapo haki kweli itatendeka?

Anawaza kwa sauti Askofu Bagonza.
 
Bwashee mtoa haki ni Mungu pekee!
 


Unamdhihaki au unamkejeli?

Mwenyezi Mungu wa haki na ajue cha kukulipa sawasawa na anavyoona kustahili.

Allah Wakil.
 
.... very funny indeed! Hati ya mashtaka (makosa unayoshitakwa nayo) imeonekana batili (yaani huna kosa) halafu jaji anaamuru hati ya mashtaka ikabadilishwe (yaani ukatafutiwe makosa mengine)! Daah! Hii n ajabu kweli kweli!
 
Hahahaaaa aisee majaji wa majalalani hawa.
 
Hii kesi ina makandokando mengi sana mpaka inatia mashaka, sijui ni lini mahakama zetu zitakua huru
 
Masikini Mbowe anafungwa hivi hivi kutokana na ujinga wa Watanzania kuwapigania watu wasiojielewa ni kazi sana.
Asiejielewa ni nani?
Kasome historia ya Mandela,na Raisi wa sasa hv wa Zambia,ndio utajua hakuna Cha upekee katika kesi ya Mbowe,Mbowe yupo ndani kutokana na utawala dhalimu wa ccm,hawataki aseme ukweli,ambao unaweza kuwatoa Madarakani.
Mandela aliitwa Gaidi miaka ya 60,70,90,sembuse Mbowe leo!!we vipi?
Hii kesi anashinda siku si nyingi,mandela alikaa miaka 27 jera!akatoka akawa Raisi,ungekuwepo wakati anafungwa lazima ungeamini Mandela ni gaidi?
 
Jaji huyu anaitwa "KIHIYO"
 
Wamuite IGP Siro akaandike hiyo kesi Mana alishawahi sema ana ushahidi wote
 
Aibu kwa jaji na mawakili wa serikali waliondaa kesi hapo ndo tunaamin mbowe anaonewa maana jaji kathibitisha Mashtaka ni batili ni suala la kufuta kesi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…