Nakubaliana na hoja zako ila hoja ilikuwa kwamba;Mbona unakuwa mkali bila sababu...?
Mbona unaamua kuwa mjinga bila sababu...?
Kama Jaji aliyesikiliza shauri hili amekiri kuwa HATI YA MASHTAKA imekosewa na haiko kwa mujibu wa sheria halafu Jaji anaamua kuamua shauri kinyume cha sheria, unataka uthibitisho gani kuwa huyu ana maslahi katika kesi hii...??
Ameshajitoa sasa. Wewe endelea kulia lia mpaka upasuke...
tuhuma alizo zitoa Mbowe na Mawakili wake dhidi ya Jaji Luvabda eti kuwa amepewa maelekezo kutoka juu kuwa amfunge Mbowe, tuhuma hizi zilipaswa zithibitishwe kwanza kabla ya Jaji kujitoa kusikiliza kesi hiyo.
nasema hivyo kwa sababu zifuatazo;
1. Tuhuma zilizo tolewa dhidi ya Jaji ni tuhuma nzito ambazo sio tu kwamba zinamchafua yeye Jaji Luvanda bali zinawachafua Majaji wote wa Tanzania bara na Muhimili wa Mahakama kwa ujumla wake kuwa hawatendi haki.
Tuhuma hizo zilipaswa zithibitishwe kwanza, huko ni kuichafua Mahakama, na wananchi wa kawaida watapoteza IMANI na MAHAKAMA.
Mahakama ndio Tegemeo la wananchi sasa kama tutaacha uchafuzi kama huu uendelee basi Mahakama inaenda kuangua na haito aminiwa na wananchi.