Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Wacha upuuzi, sifa moja kuu ya judge yeyote hapa duniani lazima awe impartial, hatakiwi kupendelea upande wowote, huyo Luvanda kama refarii kujigeuza kocha wa timu nyingine ili iweze kushinda mchezo wake ni wizi kwa taaluma ya sheria.
Mkuu kwenye dunia ya sheria impartiality inabebwa na mazingira, kuna mazingira haiwezekani. Kwa maana hiyo hiyo haiwezi kuwa sifa kuu ya mtu kuwa Jaji, labda useme maamuzi mazuri ni yaliyotolewa bila upendeleo nitakuelewa.

Jaji kuwa huru kutoa maamuuzi ni matokeo ya mazingira ya kesi husika wala haina uhusiano wa moa kwa moja na sifa ya kuwa Jaji. Inaweza usinielewe sababu hili ni swala a kifilosofia zaidi Mkuu.

Jamaa hapo juu wala sio mpuuzi ni umeshindwa tu kumuelewa alichosema Mkuu.

Hivi unaua tu kuwa namna public imepokea kesi ya Mbowe na mambo yanavyoenda mitandaoni yanaweza kumfanya aji akaona hawezi kutokuwa na upendeleo?, upendeleo unatokana na mambo mengi sana hata huruma tu inatosha kuvuruga maamuzi ya Jaji.

Jambo muhimu kujua ni Mheshimiwa Luvanda ni Jaji wa aina gani, sababu kundi la maaji atakalo angukia lina nafasi kubwa kwenye namna atakavyoshughulikia kesi zilizo mbele yake.

mgongano wa kimaslahi ni msamiati mpana sana ndugu.
 
Ni kipindi gani hiyo hati ya Mashitaka hufanyiwa marekebisho? Ni baada ya Jaji kugundua mapungufu husika au Jamhuri kuomba kwa Jaji kurekebisha mapungufu hayo?????
 
Hamjielewi, hapa tunazungumzia sheria sio filosofia; jaji kazi yake iliyokuwa inafuata baada ya mwenyewe kukiri hati ya mashtaka ya upande wa jamhuri ina matatizo ilikuwa ni kufuta kesi, na watuhumiwa kuachiwa huru, hizi ngonjera zenu za mazingira etc ni kuleta story tu hapa.
 
Ni kazi yake Mkuu kusimamia haki, kwani hujawahi kusikia au kuona waendesha mashtaka ofisi ya DPP wakisisitiza mtuhumiwa kuachiwa huru? zipo kesi kabisa bongo hapa hapa, hapa unaweza jiuiza sasa kazi yao si ni 'kukuchongea' ili ukutwe na hatia?, Mkuu haki ni kitu kiguumu sana kusimamia ili kipatikane.

Ila Mkuu mahakamani hauendi kukwepa kosa bali kujitetea kuwa haujafanya kosa unalotuhumiwa nalo, na kuwataka washitaki kuthibitisha kuwa kweli umefanya hilo kosa. Ila pia nadhani ni muda sasa elimu basic kabisa ya sheria itolewe mashuleni.
 
Mwamba akiwa kazini kuwavusha watanzania
 
Haya Mkuu, uwe na jioni njema.
 

Vuvuzela la chama, SSH, serikali hilo na utopolo wake kama kawa. Jumbe Brown nawe vipi tayari ushaachia wako?

Ninapendekeza serikali, CCM au SSH wapitishe hata ka sheria kadogo ka kuwaramba viboko makalioni (kama hamsa wa ishirini hivi) kila asubuhi:



Kwa hakika hamkatai!
 
Jajiii jajiii, aibu gani hii ndugu, yaani unakubali kutumika waziwazi
 
Awasilishe mahakamani kama anao ushahidi juu ya hayo anayo mtuhumu nayo, sio kumchafua Jiji bila ushahidi.

Kama hakuna ushahidi Jaji aendelee...
Tuhuma za uzushi kama zilivyo za ugaidi siyo? Kama hivyo ngoma ni bam-bam
 
Ushahidi wa kuwa mbowe ni gaidi uliwekwa wazi? Sheria ikowazi kama huna imani na mwenendo wa hakimu ama jaji unaweza kuomba kubadilishiwa jaji ama haki juu ya kesi yako kwahiyo kufanyaivo imekuwa nongwa?
 
Huu uonevu wa kijinga hauwezi ukaliinua hili taifa hata siku moja. Wataendeleza huu ujinga wa kubambikia watu vyesi huku nchi ikizidi kuparara tu.

Hii yote ya serikali kupigika hadi kuanzisha tozo kibao ni matokeo ya laana ya dhuluma inayofanywa na huu utawala dhidi ya raia wake.

Magufuli aliyafanya haya haya wananchi wakalia hadi Mungu akawajibu sasa tena kaja Nebukadrezzah mwingine lakini Mungu ni yule yule asiyechoka. Tutaona mwisho wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…