Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

K
Wana usafi gani? Luvanda ni mchafu, kuna Mtu huko juu amesema mahakamani imewapa jamuhuri haki ya kurekebisha hati ya mashitaka ambayo hawa kuomba! Kwanini awape hiyo ‘zawadi’ kama ni msafi?
 
Kengeza la gaidi DJ haliwezi kumtisha jaji mpaka akubali kujitoa, gaidi ajiandae kula mvua za kutosha!. [emoji1787]
Hata babayako nikengeza alilogaidiwa bila ya kuwa na ushahidi wa hayo uliyoyasema juu yake.
 
Jaji amesema hati imekosewa kama imekosewa suluhisho lake kisheria ni lipi?
 
Ni kipindi gani hiyo hati ya Mashitaka hufanyiwa marekebisho? Ni baada ya Jaji kugundua mapungufu husika au Jamhuri kuomba kwa Jaji kurekebisha mapungufu hayo?????
Tena kwenye hili, siyo Jaji aliyegundua makosa, ni mawakili upande wa utetezi waliliona hilo na kuli address. Sasa badala ya Jaji ku deal nalo kisheria, yeye anawaelekeza upande wa jamhuri kufanyia amendment. Mawakili wa utetezi wakaleta kama pingamizi kwamba liko kinyume cha sheria kwa Jaji kuelekeza upande mmoja. Leo Jaji akaamua kutupilia mbali pingamizi hilo, ndipo upande wa utetezi wakaona hawana imani na Jaji Luvanda.
 
Hati ya mashitaka inapokosewa sheria inatoa mamlaka kwa mahakama kutoa amri kwa upande wa serikali kurekebisha. Jaji alikuwa sahihi kabisa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai inaruhusu.
 
Kesi iendelee. Mawakili wa mbowe wanasumbua mahakama ili kupiga hela ya wafadhili kwamba wanamtetea mteja wao kibaraka wa wazungu.
Unamuona kuelgeza macho anapokwenda anatembea na hayo mabeberu unayoyaona wewe.
 

So ulitaka kuwe na kesi nyingine (ndani ya hii) ya kuthibitisha hizo tuhuma ndipo ajitoe ? Kwa utaratibu upi ?

By the way, ukisikiliza alivyoongea Mbowe wala hajatoa tuhuma zozote. Yeye amesema hana imani na Jaji (swala la kutokuwa na imani na mtu ni very personal na ni haki yake), pili kuongezea hilo la kutokuwa na imani naye kasema kuna maneno yanasemwa huko mitandaoni "Akaya-quate" na kuseme hatuwezi ku-ya-ignore na akamwombwa Judge ajiuzulu kwa heshima yake.

Sasa yeye katoa tuhuma zipi hapo ? Na ndio maana Judge ameelewa na amejitoa.
 
Samahani mkuu; ni wakati gani hati ya mashitaka hufutwa na mstakiwa kuachiwa? mimi niliwahi kuachiwa huru mara tano na hati ya mashitaka inafunguliwa upya.
Mwisho wa siku niliishinda Jamhuri baada ya kushindwa kuleta mashahidi mahakamani licha ya kupewa upendeleo na serikali zaidi ya mara tano.

Swali langu: Ni muda/wakati gani Jaji/Hakimu anatakiwa kufuta hati ya mashitaka?
 
Kabla ya kukujibu naomba nikuulize swali hili. Umesema uliwahi kuachiwa huru mara tano, je katika hizo mara tano ulizoachiwa huko kuachiwa kwako kulitokana na mahakama kufuta kesi kwa uzembe wa jamhuri au kulitokana na maombi ya jamhuri kuondoa hati ya mashitaka?
 
Swali dogo tu ndugu Ni kwanini aliipa jamuhuri kulekebisha hati ya makosa walioikosea bila jamuhuri kuomba kufanya hivyo? Kama uamuzi ulikuwa Ni kukosa uhaalali wa hati ya mashitaka?. Hapo Ni tayari kaonyesha upendeleo wa wazi
Sheria inaruhusu mahakama kutoa amri kwa jamhuri kurekebisha hati ya mashitaka pale mahakama inapogundua hati hiyo inamakosa.
 
Ni hakimu.kufuta kesi kwa uzembe wa jamhuri alafu wakawa wananikamata mlangoni na kunifungulia kesi upya.
 
Ni hakimu.kufuta kesi kwa uzembe wa jamhuri alafu wakawa wananikamata mlangoni na kunifungulia kesi upya.
Hapo walikuwa wanakosea mkuu. Mahakama ikifuta kesi kwa uzembe wa jamhuri, jamhuri haitakiwi kukukama tena na kukufungulia kesi inayotokana na kesi hiyo hiyo mpaka hiyo amri ya mahakama itenguliwe na mahakama ya juu yake.
 
Kesi yenyewe ni ya kudhaniwa na kuhisi kuhisi tu na haina uzito wowote hata kwa yule asiyejua sheria,tatizo siasa ya chama kimoja inapoingia kwenye sheria inafanya wataalamu wetu wa sheria kama Jaji Luvanda kupindisha sheria kwa maslahi ya chama tawala na serikali.
 
Mihimili ya Mahakama na Bunge yote haiko independent. Peleka ujinga wako kijijini kwenu huko.
 
Hapo walikuwa wanakosea mkuu. Mahakama ikifuta kesi kwa uzembe wa jamhuri, jamhuri haitakiwi kukukama tena na kukufungulia kesi inayotokana na kesi hiyo hiyo mpaka hiyo amri ya mahakama itenguliwe na mahakama ya juu yake.
Hapo nimekuelewa; je na hii ya Mbowe hayo marekebisho anayoyapendekeza jaji ni nani angeyatetea kisheria? Mimi ninachojua ni kua jaji alitakiwa kufuta hati ya mashitaka kwani inapelekea kesi kua batili alafu jamhuri iweze kufungua kesi upya.
Watu wengine wanasema umuhimu wa kesi bila kujua pia kesi muhimu inahitaji umakini zaidi.
Kwangu mimi ninaamini kua 90% ya waendesha mashitaka kwa upande wa jamhuri ni corrupted.
 
Nimejifunza kitu, kumbe kama unaona huyu Jaji ama hakimu haelewekia ama hasomeki kumbe naweza kumkataa tu kisha nikachagua Jaji au Hakimu ninaye mtaka na akasikiliza kesi yangu.
Kumbe siku hizi unaweza kuchagua Jaji ama Hakimu wa kusikiliza kesi yangu. aise!!
 
Sheria inaruhusu mahakama kutoa amri kwa jamhuri kurekebisha hati ya mashitaka pale mahakama inapogundua hati hiyo inamakosa.
Unasema pale mahakama inapogundua hati hiyo ina makosa, je katika hii kesi mahakama iligunduaje kwamba kesi ina makosa? Kumbuka Jaji hakuwa na tatizo na hati iliyowakilishwa na jamhuri mpaka pale alipopewa somo na upande wa utetezi kwamba hati hiyo ni batili.

Jaji alikuwa tayari kuendelea na kesi kwa msingi kuwa hakuona tatizo na hati hadi pale utetezi ulipompiga stop kuendelea na kesi kwa kutoa ushahidi kuwa hati ni batili. Na kweli Jaji baada ya kusikiliza hoja ya utetezi na kukubaliana nao alitakiwa kufuta ile kesi mara moja.
 
Kweli ktk hii nchi kuna mhimili uliojichimbia chin zaidi
 
Pole bi.mjane wa mwendazake
 
Ngoja nikutoe tongotongo. Hati ya mashitaka inapokuwa batili kuna njia mbili za kuitibu. Moja, serikali iamue kuiondoa mahakamani na kuleta hati mpya isiyo na makosa au kuomba amri ya mahakama kuirekebisha bila kuiondoa na kesi iendelee. Pia mahakama pale inapoona kuwa hati ya mashitaka inamakosa, sheria inaipa nguvu mahakama kutoa amri kwa upande wa serikali kurekebisha hati ya mashitaka na kesi iendelee.


Alichokifanya jaji ni kutumia hiyo njia ya mwisho ambayo imepewa mahakama na sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ambayo ni , pale mahakama inapoona hati ya mashitaka inamapungufu, mahakama inaweza kutoa amri kwa upande wa serikali kurekebisha hayo mapungufu na kesi iendee bila kuifuta kesi yenyewe. Kwa mlengo huu jaji yupo sahihi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…